Push Mobile wampa Tuzo ya Mwanasiasa Bora Prof. Sospeter Muhongo

Push Mobile wampa Tuzo ya Mwanasiasa Bora Prof. Sospeter Muhongo

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2008
Posts
10,942
Reaction score
437
* Ni kupitia Tuzo za jamii

* January Makamba akaangwa

Usistaajabu ya Musa kabla haujaona ya Firauni ndivyo yalivyojitokeza kwenye tuzo za jamii ambazo zimeacha maduwazo na maswali kede wa kede.

Vipengele ama tuzo mbili zimetokea kuwaacha watu midomo wazi. Tuzo ya kwanza ni ile ya Mwanasiasa bora ambayo imechukuliwa na aliyekuwa Waziri wa nishati na madini aliyejiuzulu kwa kashfa ya ufisadi wa Escrow, Prof. Sospeter Muhongo.

Tuzo hizo ambazo zimefanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere zilizua gumzo kubwa kuwa ile kashfa ya ufisadi wa bilioni zaidi ya 300 ambayo ilitikisa nchi kutokana na kuchukizwa wengi hali iliyopelekea Baraza la mawaziri kuvunjwa, mawaziri kujiuzulu akiwemo Prof. Muhongo leo hii anapewa tuzo ya mwanasiasa bora. Haya ni maajabu ya Dunia.

Kashfa ile ya ufisadi wa Escrow iliyosababisha wahisani kuifungia misaada Tanzania katika bajeti ya nchi, kashfa iliyosababisha hali ya kifedha nchini kuwa mbaya, ndio hiyo hiyo ambayo Push mobile wameamua kubariki ufisadi huo kwa kumpa tuzo ya Mwanasiasa bora mtuhumiwa wa kashfa hiyo aitwaye Prof. Muhongo ili waisafishe kashfa hiyo chukizo kwa watu.

Watu ukumbini wakaanza kuhoji, hakuna mwanasiasa msafi asiye na kashfa wa kupewa tuzo hiyo mpaka wampe Prof. Muhongo? Ni kweli Watanzania wamepiga kura zao kumpigia mtuhumiwa wa ufisadi wa Escrow?

Tuzo ya pili iliyozua gumzo ni tuzo ya mwanasiasa kijana anayechipukia ambayo alipewa January Makamba.

Maswali mengi yaliibuka kuwa January Makamba ni mwanasiasa bora kijana kumzidi Zitto Kabwe, kumzidi John Mnyika, ama kumzidi Mwigulu Nchemba? Kwanini push mobile wampe ushindi January Makamba?

Kwa muda mrefu January Makamba ambaye ni Naibu waziri wa sayansi na teknolojia amekuwa akihusishwa na uhusiano wa karibu na kampuni ya push mobile.

Mahusiano haya yalianza kuibuliwa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ambapo walituhumiwa kuiibia CCM Tsh. bilioni 8 za uchaguzi, leo hii wameamua kuuainisha wazi ushindi wa January Makamba na uhusiano wake na push mobile.

Kila mtu amechukizwa na usanii uliofanywa na push mobile na waandaaji wa tuzo za jamii na kuhoji kama walikuwa tayari na washindi wao mifukoni kwanini wachukue pesa za watu kupitia njia ya upigaji kura, huu ni ufisadi uliopitiliza kiwango.

Ikumbukwe washindi wa tuzo za jamii wamepatikana kupitia upigwaji kura kupitia huduma ya push mobile lakini mtangazaji wa tukio hilo alisema wazi wazi kuwa washindi hao haamini kama kweli wamepatikana kupitia kura za wadau. Na hili ni kweli kabisa kuwa ushindi ule ni dhahiri ulikuwa wa mezani na si kura za watu.
 
Hivi ni nani anaiamini push mobile nchi hii ? waache wajifurahishe tu .
 
January makamba amezoea kuiba aliiba mitihani na kufeli kila kidato eti awaongoze watanzania

Kwa mujibu wa Katiba Pendwa Inayopendekezwa anatakiwa ajue kusoma na kuandika kiswahili tu, Yatosha!
 
Lowasa nae kapewa ipi tena?Kweli MACCM wananajisi kila kitu,kuanzia vyuo,waganga,makanisa,PHD,Uprof..etcsasa tuzo,
 
Tanzania kila kitu ni usanii, Muhongo amekuwa mwanasiasa bora?

Inawezekana mimi ndiye sijui maana ya siasa bora au inawezekana pia kuwa hakuna 'common definition' ya neno ' siasa bora' kiasi kwamba kila mtu ana judge kulingana na vigezo vyake.
 
Kwani HUJUI ukistaajabu ya MHONGO utayaona ya LOWASA.
 
Ndio maajabu ya Firaun haya maana Muhongo hata bungeni kateuliwa na rais hajawahi katika maisha yake kugombea nafasi yoyote ya Kisiasa nchini. Hana uzoefu wa kisiasa ktk uongozi wa chama chochote nchini, hajawahi kusimama jukwaa lolote la kisiasa, sasa hii kupewa tuzo la mwanasiasa bora ni mchezo gani huu ama pengine jamaa ni mwekezaji kwa hisa au kamwaga mifedha hapo Push Mobile....
 
Huu ujinga wao wabaki nao wenyewe hao vilaza wa Push Mobile!
 
Ndio maajabu ya Firaun haya maana Muhongo hata bungeni kateuliwa na rais hajawahi katika maisha yake kugombea nafasi yoyote ya Kisiasa nchini. Hana uzoefu wa kisiasa ktk uongozi wa chama chochote nchini, hajawahi kusimama jukwaa lolote la kisiasa, sasa hii kupewa tuzo la mwanasiasa bora ni mchezo gani huu ama pengine jamaa ni mwekezaji kwa hisa au kamwaga mifedha hapo Push Mobile....
Tanzania ni kila kitu usije kushangaa mwaka kesho Mwadhama Kadinari Polycarp Pengo ndiye mwanasiasa bora Tanzania.
 
Taifa la wajinga kwa idhini ya majuha,

Muhongo tangu lini amekuwa mwanasiasa? Alishawahi kushiriki siasa wapi?

Tangu azaliwe hajawahi kuwa mwanasiasa mpaka juzi alipoteuliwa kuwa mbunge, hivi tayari anaitwa mwanasiasa mpaka kupewa uanasiasa bora?

Hizi tafiti za kizandi vyombo vya dola vishughulike nazo kuliko kupoteza mda na watu wema akina Gwajima.
 
Taifa la wajinga kwa idhini ya majuha, Muhongo tangu lini amekuwa mwanasiasa? Alishawahi kushiriki siasa wapi? Tangu azaliwe hajawahi kuwa mwanasiasa mpaka juzi alipoteuliwa kuwa mbunge, hivi tayari anaitwa mwanasiasa mpaka kupewa uanasiasa bora? Hizi tafiti za kizandi vyombo vya dola vishughulike nazo kuliko kupoteza mda na watu wema akina Gwajima.
Km tumekula wanyama waliochinjwa kishirikina,tumeongozwa na kuwaapisha walioua na kutambika mshetani yao kwa damu za Albino na waliokufuru kila nyumba ya ibada njema.Kwanini tusiishi km misukule?Ndio kinachotokea nchini.Huwezi jua kwanini kila msomi akifika TZ anarudia unyani aliouvua, kila akirudi TZ anavuka uprof, udr..etc.Mara atakapokula kiapo cha laana?
 
ALAFU HAO MAJUHA WA PUSH MOBILE NA BAADHI YA WADAU WA MUZIKI TZ WANAAMINI KUWA MAKAMBA JR ATAKUJA KUWA RAIS WA TZ. Makamba is a disaster like other disasters.
 
Wivu wa kike nao ni tatizo.mwanasiasa bora ni yule aliyeweza kujutana na changamoto kibao na akazimudu. Mfano kati ya marais wote wa tanzania iliyopita ni kambarage tu ndiye aliyewahi kuiongoza nchi kupigana vita kwa msingi huo ni shupavu. Sasa unataka mwanasiasa bora awe wenje ambaye hajawahi kuongoza hata wizara hata kijiji !?
 
Maaabu huwa hayaishi nchi hii.
Laini ni vigu,u sana kuwasafisha mafisadi wa escrow kwani nWatanzania wengi walifuatilia hatuakwa hatua.
 
Aliyeibuka mshindi ni Prof Sospeter Muhongo ambaye licha ya kudumu kwenye siasa kwa muda mfupi, amefanya mambo makubwa sana. Kubwa zaidi ni kusambaza umeme vijijini na kusimamia nidhamu na kuziba mianya ya rushwa kwenye sekta za nishati na madini. Uwekezaji katika gesi umempaisha Muhongo hadi kwenye level ya juu sana na kuwapiku wenzake.


Kwa upande wa Mwanasiasa Kijana mwenye mafanikio katika jamii, aliyeibuka Mshindi ni Januari Makamba. Huyu naye amemudu vema nafasi yake ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia. Kawapiku wenzake akina Zitto Kabwe, Mnyika na wengineo. Hongera Makamba.
 
Back
Top Bottom