Katika kusoma kwangu repory zooote za CAG, PAC sijaona mahali popote ambapo Prof Muhongo ametajwa kwamba amekula pesa yoyote! Na hata ukimwangalia machoni huoni dalili hizo kabisa! Sasa nakereka watu kutoa mishipa ya shingo kummwingiza mtu kwenye kashfa ambazo hazina mbele wala nyuma!Sasa wewe ulitaka push mobile watoe matokeo unayotaka wewe au? Kwanini na wewe usiandae tafitiukatoa matokeo yako? ? Unaumiza kichwa na tafiti za wenzako ambao walikaa, wakaandaa hadidu, wakakusanya maoni na mwisho wakatoa taarifa!
Am cimpletely against this ideology! Kabisa! Fanya na wewe yako! Una uhuru huo mbona!
Pamoja na kwamba mimi ni mkereketwa wa maendelo lakini namkubali sana Prof. Muhongo! I think the escrow issue was just a political accident! We can still utilize him as our think tank na hasa katika dunia ya leo tunayoenda ya uchumi wa gas na mafuta. Hii Inaweza mtokea mtu yeyote! Mbona ilimtokea Rais mstaafu Ali Mwinyi na baadae akaja kuwa Rais wetu!
Huyo Mhongo hajawai hata kuomba kura za Ubalozi wa mtaa leo tunaambiwa ni mwanasiasa bora.
Samahani lakini naomba kuelimishwa ndugu zangu "PUSH MOBILE" ni nini?
Muhongo katika matambo yake alisema yeye sio mwanasiasa na kwamba yeye ni msomi nambari moja duniani, badala ya kupewa tuzo la msomi bora anapewa la mwanasiasa bora sasa nani kati yao ametudanganya?
hivi ni nani anaiamini push mobile nchi hii ? waache wajifurahishe tu .
ALAFU HAO MAJUHA WA PUSH MOBILE NA BAADHI YA WADAU WA MUZIKI TZ WANAAMINI KUWA MAKAMBA JR ATAKUJA KUWA RAIS WA TZ. Makamba is a disaster like other disasters.
Huu ujinga wao wabaki nao wenyewe hao vilaza wa Push Mobile!
Rejea CV na Mafanikio yake.
Wamejipigia tu kura wenyewe kwa wingi kadri ilivyowezekana;
Wewe usiandike kwa kufuata mkumbo, kama huna elimu kichwani kaa kimya! Unajua maana ya mwanasiasa! ,? Unajua siasa ni nini! ? Unajua vigezo gani walitumia ili kufanya tafiti yao? ? No research no right to speak! Weka na wewe vigezo vyako andaa tafiti then toa matokeo! Watu lazima tubadilike, hii ni dunia nyingine, karne nyingine hamjitambui tu! !
Eti unamzungumzia Gwajima! Wewe unamjua Gwajima! Unajua katokea wapi na ameshafanya nini mpaka sasa nchini kwetu! Usione watu watu wanatembea na mabaunsa mia! Ukadhani lazima ni msafi! Wanausalama nao wana vitu pia wanatafiti, usiwaingilie! Kila siku nasema wajameni tubadilike! Tusiende na mikumbo ambayo hatuijui!
Jamani hivi sospeter muhongo ni mwanasiasa? Kama ninakumbukumbu vizuri huyu alikuwa hajihusishi na siasa, akapewa ubunge na rais ambapo sio mwakilishi wa mtu yeyote isipokuwa mamlaka iliyomteua, akapewa uwaziri pia. Sasa siasa amefanya lini? Mtofautishe na kina lowasa, wasira, ambao wapo kwenye siasa muda mrefu, tanzania kila kitu ni ubabaishaji. Makamba nae duh, itakuwa wao ndio waandji wakazuga kuwashindanisha na wengine. Makamba na zito wapi na wapi, au kwa kuwa ni naibu waziri wa mb 8 ndio mafanikio au kwa kuwa muhongo ameteuliwa mbunge, waziri amepaa ndio umahiri wao. Fyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu* Ni kupitia Tuzo za jamii
* January Makamba akaangwa
Usistaajabu ya Musa kabla haujaona ya Firauni ndivyo yalivyojitokeza kwenye tuzo za jamii ambazo zimeacha maduwazo na maswali kede wa kede.
Vipengele ama tuzo mbili zimetokea kuwaacha watu midomo wazi. Tuzo ya kwanza ni ile ya Mwanasiasa bora ambayo imechukuliwa na aliyekuwa Waziri wa nishati na madini aliyejiuzulu kwa kashfa ya ufisadi wa Escrow, Prof. Sospeter Muhongo.
Tuzo hizo ambazo zimefanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere zilizua gumzo kubwa kuwa ile kashfa ya ufisadi wa bilioni zaidi ya 300 ambayo ilitikisa nchi kutokana na kuchukizwa wengi hali iliyopelekea Baraza la mawaziri kuvunjwa, mawaziri kujiuzulu akiwemo Prof. Muhongo leo hii anapewa tuzo ya mwanasiasa bora. Haya ni maajabu ya Dunia.
Kashfa ile ya ufisadi wa Escrow iliyosababisha wahisani kuifungia misaada Tanzania katika bajeti ya nchi, kashfa iliyosababisha hali ya kifedha nchini kuwa mbaya, ndio hiyo hiyo ambayo Push mobile wameamua kubariki ufisadi huo kwa kumpa tuzo ya Mwanasiasa bora mtuhumiwa wa kashfa hiyo aitwaye Prof. Muhongo ili waisafishe kashfa hiyo chukizo kwa watu.
Watu ukumbini wakaanza kuhoji, hakuna mwanasiasa msafi asiye na kashfa wa kupewa tuzo hiyo mpaka wampe Prof. Muhongo? Ni kweli Watanzania wamepiga kura zao kumpigia mtuhumiwa wa ufisadi wa Escrow?
Tuzo ya pili iliyozua gumzo ni tuzo ya mwanasiasa kijana anayechipukia ambayo alipewa January Makamba.
Maswali mengi yaliibuka kuwa January Makamba ni mwanasiasa bora kijana kumzidi Zitto Kabwe, kumzidi John Mnyika, ama kumzidi Mwigulu Nchemba? Kwanini push mobile wampe ushindi January Makamba?
Kwa muda mrefu January Makamba ambaye ni Naibu waziri wa sayansi na teknolojia amekuwa akihusishwa na uhusiano wa karibu na kampuni ya push mobile.
Mahusiano haya yalianza kuibuliwa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ambapo walituhumiwa kuiibia CCM Tsh. bilioni 8 za uchaguzi, leo hii wameamua kuuainisha wazi ushindi wa January Makamba na uhusiano wake na push mobile.
Kila mtu amechukizwa na usanii uliofanywa na push mobile na waandaaji wa tuzo za jamii na kuhoji kama walikuwa tayari na washindi wao mifukoni kwanini wachukue pesa za watu kupitia njia ya upigaji kura, huu ni ufisadi uliopitiliza kiwango.
Ikumbukwe washindi wa tuzo za jamii wamepatikana kupitia upigwaji kura kupitia huduma ya push mobile lakini mtangazaji wa tukio hilo alisema wazi wazi kuwa washindi hao haamini kama kweli wamepatikana kupitia kura za wadau. Na hili ni kweli kabisa kuwa ushindi ule ni dhahiri ulikuwa wa mezani na si kura za watu.
Siku hizi nikiisha ona uzi umesifiwa na lizabon tu, basi najua hiyo maada au kilichofanyika ni full ujinga, kitendo tu cha kusifia hizo tuzo tayari najua kuna ujinga umefanyika, kwa ufupi humu ndani kipimo changu nachokitumia kwa ujinga ni LIZABONIAliyeibuka mshindi ni Prof Sospeter Muhongo ambaye licha ya kudumu kwenye siasa kwa muda mfupi, amefanya mambo makubwa sana. Kubwa zaidi ni kusambaza umeme vijijini na kusimamia nidhamu na kuziba mianya ya rushwa kwenye sekta za nishati na madini. Uwekezaji katika gesi umempaisha Muhongo hadi kwenye level ya juu sana na kuwapiku wenzake.
Kwa upande wa Mwanasiasa Kijana mwenye mafanikio katika jamii, aliyeibuka Mshindi ni Januari Makamba. Huyu naye amemudu vema nafasi yake ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia. Kawapiku wenzake akina Zitto Kabwe, Mnyika na wengineo. Hongera Makamba.