Pugu Boys Secondary School a.k.a Pond boys

Hahahahaha!
Nakumbuka kipindi kile mchezo wa tausi wa kina mjuba na siti ulikuwa unapendwa kishenzi bongo na tulikuwa tunaangalia kila jumapili usiku pale mbele na dining hall karibu na bweni la ujamaa.
Jamaa alikera kichizi!

Daaah enzi za tausi ilikuwa tausi kweli.......ilikuwa kale ka intro ka tausi kakianza tu....utasikia machizi wanakimbia mabwenini kulekea pale nje bwaloni ha!ha!ha!..Tausi ndege wangu, ndege wangu wa fahari.......acha tu!.....Sitasahau pale mahali aiseee!
 
MImi nilimuacha mkandawire dada pale miaka ya mwanzo ya tisini, alikuwa anajitahidi aisee!!

I wish tungekuwa na alumni ya Pugu kwenye yahoo groups na vilevile tungefanya bash moja la karne hasa katika kipindi cha kumuenzi nyerere

Hivi yule ticha nyoka yuko wapi?

Nakubaliana na wazo lako Mkuu na kama kuna nia kweli basi nitafanya juu chini kuwatafuta ex pugu students wote ninaowafahamu.
Huyo Mkandawile dada sikumkuta.Labda wana undugu na huyu Mkandawile mwingine au ni majina tu?
 
Sikusoma pugu najua ni boys skul, ila nilisoma tution za Mkandawile alipokuwa anafundisha mtendeni primary school na mchikichini, alinipatia elimu nzuri sana kwenye organic chemistry. Ila Siku hizi ana shule yake binafsi ipo mitaa ya Pugu. Inaitwa jina lake Mkandawile high school. Mambo yake siku hizi yapo swafiii.

Pretty kumbe na wewe ulikuwa mwanafunzi wa chemistry wa Mkanda,saafi sana!Sisi Pugu boys alikuwa anakuja kutufundisha tuition shuleni usiku mpaka akaja kuwa mwalimu kamili wa Pugu.Kipindi hicho tena kama sikosei alikuwa anafanya Bsc.Ed Mlimani.Wakati wa likizo nilikuwa nakwenda tuitions zake pale Buguruni.
Unakumbuka ile sheria ya Markovnikov kwenye organic ya Mkanda?Anakwambia 'kijana ni rahisi tu Markovnikov rule ni rahisi...unakumbuka tu yale maneno ya yesu kwenye biblia..mwenye nacho anaongezewa'.hahaaha
Long live Mkanda!
 
Mkuu P53 Respect! Hapo kwenye bold nimecheka sana mzee......lile lijamaa lilikuwa noma sana!

Ha!ha!ha!haaaaa.....Mama Pendo + Pendo mwenyewe we acha tu....ile miandaazi yake ilikuwa poa kweli si tulikuwa tunampiga bao kweli.....ila kale ka Pendo.....mzee kalikuwa kametulia........! mzee unawakumbuka wale chokoraa...watoto wama ex Pugu boys.....hawana baba now? ...wakuu yeyote aliyegonga demu pale, si tulikuta vitoto vingi sana vya ma ex Pugu boys so please rudini mkacheki kuna damu zenu pale!

Mzee nilikuwa next to your class....EGM na mzee Msungu, Shire na yule teacher Mhaya wa Hesabu! Mkuu utakuwa ulikuwa na kina Mwatebele, Matobogolo Masalu etc sio?

Mwabaks lilikuwa kama dudu flani hivi.!Ile staff ilikuwa noma.Hapo hujamuongelea Songombingo.Jamaa mrefu kishenzi na ukiingia anga zake basi adhabu yako anakwambia ukachimbe shimo yeye akiingia akasimama na kunyoosha mikono yake apotee!

Hahahaha!Nakakumbuka kale Ka Pendo,sema sidhani kama kuna mshkaji alikapitia kale.Nakumbuka wale kina mama/vibibi wauza mboga washkaji walikuwa wanajipigia kwa sana tu.Utakuta jioni baada ya dinner vikiwa vinarudi nyumbani washkaji walikuwa wanavisaidia kubeba masufuria yao halafu uko njiani usiulize tena Mkuu nini kitaendelea!
Yale matoto nayakumbuka.Kuna mshkaji sijui kama unamkumbuka nadhani alikuwa kwenu EGM anaitwa Kamugisha.Jamaa alikuwa mlevi wa pombe ya mnazi na gongo kijijini.Basi mara kibao tu wanakijiji walikuwa wanamrudisha bwenini hajitambui kama mzoga!
Unawakumbuka wanafunzi wa taasisi>?

Sikuwa lile darasa karibu na kwenu Mkuu.Nilikuwa haya mengine karibu na Maabara kama unakumbuka kulikuwa na PCB kama 3 hivi.Mimi nilikuwa na kina Mkufya,Gwamaka,Marius kama unawakumbuka.Ila darasa lenu nawakumbuka kina Allain,Ahmed(head boy)
Matobogolo na Mwatebele nawafahamu.
 
Nakubaliana na wazo lako Mkuu na kama kuna nia kweli basi nitafanya juu chini kuwatafuta ex pugu students wote ninaowafahamu.
Huyo Mkandawile dada sikumkuta.Labda wana undugu na huyu Mkandawile mwingine au ni majina tu?

Thanks p53, yule dada sidhani kama alikuwa na uhusiano na yule ticha wa kitaa. dada alikuwa anaishi masaki na wazazi wake, alinipenda sana mpaka nikajua kwao kwasababu kipindi hicho eti na mie nilikuwa mashine ya chemistry.

Kuhusu alumni, we have to do it...
 
Daaah enzi za tausi ilikuwa tausi kweli.......ilikuwa kale ka intro ka tausi kakianza tu....utasikia machizi wanakimbia mabwenini kulekea pale nje bwaloni ha!ha!ha!..Tausi ndege wangu, ndege wangu wa fahari.......acha tu!.....Sitasahau pale mahali aiseee!

Kudadadeki!! yaani nyie mliona mpaka michezo ya tiviiii!!!!!!!!!!! nimemaind, sie tukiwa na akina nzowi tuliiishia kupokea wageni wa wizarani na mbio za mwenge tu!!! hakukuwa hata hivyo tivii...

Damn!!!! you lived in another world and not pugu

DOCEBIT VOS OMNIA!!!
 
Last edited:

MTM.....Usitake tucheke ndugu yetu...ha!ha!ha!ha!aaaaa!.......Hako kaTV kaliwekwa pale nje ya bwalo...just for Tausi na habari...then Juma wasi wasi...kang'oa kapeleka nyumbani kwake...tokea hapo no TV nafikiri mpaka leo mkuu!
 
Aisee nimecheka mpaka basi, yaani jamaa kaona mnafaidi siyo?? hivi Juma wasiwasi yuko wapi?
 
Aisee nimecheka mpaka basi, yaani jamaa kaona mnafaidi siyo?? hivi Juma wasiwasi yuko wapi?

Kati ya mwaka 2002 hadi 2005 nafikiri alikuwa UDSM - FPA, then nikawa na mwona mwona sana Hakielimu......sijui bado yupo nao or kasepa! Alikuwa mnoko sana yule jamaa,....akijifanya anajua sana kiswahili.....na nywele zake alikuwa anaweka BLACK.....si unajua kichwa chote kilikuwa kama EL!
 
Naskia Charwe walimchapa makofi huko Kilosa... alizidi kuwaibia Tambaza na wattoto wa mjini wakija tuition kule pugu, jamaa alikuwa kama anakula ganja aisee jinsi alivyokuwa mpuzi
 
Naskia Charwe walimchapa makofi huko Kilosa... alizidi kuwaibia Tambaza na wattoto wa mjini wakija tuition kule pugu, jamaa alikuwa kama anakula ganja aisee jinsi alivyokuwa mpuzi

Charwe ganja ilikuwa inapanda na pia alikuwa anapiga na gongo vile vile! Lakini jamaa Biology ilimkaa kichwani kwa kweli... Nzoi yuko wapi? Na mama wa Biology A level pamoja na mumewe?
 
Yule ticha Mhaya aliitwa Rwezaula!

Yes you got it bombii nyumbii! Kale kajamaa kalinipaga 21% kwenye test ya kwanza kabisa ya Mathematics........kalikuwa na mkwara sana kale kajamaa! bt really hesabu zilikuwa zinapanda....ila alikuwa mchoyo kumwaga utirio wote!
 
Yes you got it bombii nyumbii! Kale kajamaa kalinipaga 27% kwenye test ya kwanza kabisa ya Mathematics........kalikuwa na mkwara sana kale kajamaa! bt really hesabu zilikuwa zinapanda....ila alikuwa mchoyo kumwaga utirio wote!

Duh... Aisee hizo tulikuwa tunaita namba za viatu!!
 
Duh... Aisee hizo tulikuwa tunaita namba za viatu!!

Hapo nilikosea mkuu 21% ilkuwa ...daah niliconfuse kabisa, O level wakati huo nilikuwa kipanga wa namba aisee, nilijiona mdogo kama piliton aisee.....bt thanks, ilinipa nguvu sana ya kula ma Backhouse, ma Shayo etc...at the end of the story katoka na B!
 
Ha!ha!ha!ha!haaaaaa! Kumbe MC nawe ni walewale wa DOCEBIT VOS OMNIA heeee!

Mkuu Mwal. Msungu alishatangulia mbele za haki.......! Kamanda Mabagala aka Mabags aliendaga UDSM......sijui yupo wapi now! Ila huyu jamaa alikuwa noma.....bed check, akikuta mmelala wawili anauliza cheti cha ndoa kipo wapi....h!ha!ha!haaaaa! Aliwatukimbisa hadi Pond ya kule Mapinduzi.......!tukala forest, noma sana yule jamaaa!

Yeah, mimi nilikuwa pale form 5/6 1994 - 1996, Mabagala alikuwa mwalimu wangu wa bweni, Azimio.

RIP Msungu (Majiman and Umememan)

Hii thread inanikumbusha mbali sana, Siku ya kwanza nilipofika tu ilikuwa siku ya Ubwabwa aka Uchele, kwa kuwa ilikuwa ndio tumefungua wanafunzi tulikuwa wachache kwa hiyo siku hiyo share ikamtosha kila mtu, mimi nikala kidogo kisha mwingine nikaumwaga, aaaa Madenti wa siku nyingi hapo wakanishangaa na kusema unamwaga uchele Pugu, wewe hauko serious na Utaukumbuka. Tehe tehe tehe ....... niliukumbuka wiki iliyofuata
 
You got it MC .....yule jamaa (Msungu) aisee alikuwa very committed kny issues za maji na umeme pale kilimani! Mpaka anafariki, alikuwa anafuatilia mradi wa maji kutoka Kisarawe....sasa naona tangie atoweke hakuna linaloendelea.....!
 
Yeah, mimi nilikuwa pale form 5/6 1994 - 1996, Mabagala alikuwa mwalimu wangu wa bweni, Azimio.

RIP Msungu (Majiman and Umememan)

Hii thread inanikumbusha mbali sana, Siku ya kwanza nilipofika tu ilikuwa siku ya Ubwabwa aka Uchele, kwa kuwa ilikuwa ndio tumefungua wanafunzi tulikuwa wachache kwa hiyo siku hiyo share ikamtosha kila mtu, mimi nikala kidogo kisha mwingine nikaumwaga, aaaa Madenti wa siku nyingi hapo wakanishangaa na kusema unamwaga uchele Pugu, wewe hauko serious na Utaukumbuka. Tehe tehe tehe ....... niliukumbuka wiki iliyofuata

Nakumbuka sana tuligoma siku moja halafu tukawekwa assembly usiku aisee!! Watu walikula usiko wa manane siku hiyo
 
Mabagala alikuwa na kiduka karibu na Nyumba za walimu, siku moja watu wakaamua wamkasirishe kwa makusudi, bahati mbaya walifanya hivyo kwa kutumia kijana wa form one (sorry for him) ambaye alikuwa ni mgeni.

Walimpatia Sh 100, wakamwelekeza kiduka cha mabagala kilipo wakati huo mabagala mwenyewe alikuwa dukani, wakamwambia "We dogo nenda kwenye lile duka katununulie Mabagala tatu, mwambie muuzaji na chenji irudi.

Dogo kama alivyoelekezwa. "Shikamooo... Naomba Mabagala tatu na chenji irudi"

Jamaa alifunga duka, fikiria mwenyewe nini kilitokea.......
 
Weweeeeee!
Kumbe mpo wengi? Hata mimi nlikuwepo miaka ya mwanzo ya 2000
Ebwanae, maendeleo yalikua kidogo maana kuna wauza maji ya Sim tank japo
TZS100 kwa kandoo, mambo hayakuwa magumu ka enzi za mwl
Kuna mama alikua anaitwa mama Pendo alikua anauza wali,na tunabadili mlo pia makande na ubwabwa vilikua vikitolewa shule kimtindo,
Aaaar, umeniumiza wakati hou Head alikua magamba kuna jamaa mmoja, alale pema peponi, alipigwa risasi na majambazi yalotaka kupora hela pale account, jamaa alikuwa
anapiga msuli kwenye coridol( alikuwa F6) anajianda na necta-akatoka kuangalia nani anagonga mara akatwangwa risasi mguuni akafa baadae baada ya kupoteza damu nyingi-risasi zilikua zinalia ka-iraki, Keshoye tuliandamana mpaka wizarani hatimae magamba akahamishwa-leo hii ina ukuta ila imefurika wanafunzi- bed moja mtu 2 au kulala kwa timing mmoja naenda kwenye msuli mwingine analala
Dar inaniuma sana nikikumbuka enzi hizo
 
Back
Top Bottom