Mwawado
JF-Expert Member
- Nov 2, 2006
- 993
- 252
Huu mradi kwa manufaa ya nani haswa?Hawa Viongozi wetu watatupeleka pabaya!,wamekuwa walafi mno kwa kujali matumbo yao binafsi na kuwaacha wananchi wa kawaida maskini!.Hivi kweli tumefikia wakati wa kuhitaji Green Ethanol?kwa magari gani tuliyonayo?Hapo kuna pesa za nje nje na sasa viongozi wetu walafi akina Karamagi wameanza kutolea macho.Tumeshindwa kutoa huduma muhimu kwa wanachi kama matibabu na Elimu,sasa tunataka kuwapokonya na Ardhi?
Wanavijiji wa huko Bagamoyo na Rufiji ni vigumu kuwaelewesha hili jambo wakalijua vizuri(walio wengi upeo wao wa uelewa ni mdogo),bali watakubali kupewa pesa kidogo na kutafutiwa sehemu kame wakaishi.
Ni wakati sasa wa kuwapigia kelele Viongozi wetu waache kufikiri kuwa kila uwekezaji utainufaisha Nchi.Hakuna kosa baya tutakalofanya kama hilo la kuuza ardhi yetu!Hao wawekezaji wawaelimishe wananchi na kuwaelekeza kilimo hicho cha miwa ili Wana-Rufiji na Bagamoyo wapate pesa kwa kuuza zao hilo kwa hao wawekezaji.
Kwa mara nyingine nakupongeza Mzee Moshi kwa Taarifa hii.Kuna kila sababu ya kuzungumza na Magufuli kuhusu mradi huo haramu.