Youandme
JF-Expert Member
- May 6, 2013
- 200
- 113
- Thread starter
- #61
Mkuu sijawahi kukuita si m-Tanzania na wala sijawahi kuhoji uraia wako kwani hata mimi nimeshatuhumiwa uraia wangu kwa kuwa tu nauliza maswali ya msingi kuhusu huu uhasama kati ya Tanzania na Rwanda. Ndugu yangu nchi ya Israel inafanya biashara ya silaha na nchi nyingi sana duniani. Nadhani hata sisi tunanunua baadhi ya vifaa kutoka Israel. Kuuzia silaha nchi haina maana Israel inahusika kupepea moshi wa mgogoro huu. Umesema mwenyewe kuwa suala ni wakimbizi wa ki-uchumi kutoka Eritrea na Sudan kupewa hifadhi Uganda in exchange of arms/military aid. Mbona huisemi China ambayo inauza silaha kwa nchi zote za maziwa makuu? Mbona huwasemi wa-Faransa, wa-Ingereza, wa-Afrika ya Kusini ambao wote ni wauza silaha wakuu duniani? Mbona huwasemi wa-Tanzania wenzako (mnawaita mafisadi) ambao ndio wauza silaha wakuu katika uwanda huu wa Afrika ya Mashariki, Kati na Kusini? Hivi unafikiri hizo silaha zinatumiwa na majeshi ya nchi hizi na hayo makundi yote ya waasi zinatoka na kupitia wapi? Fanya uchunguzi ujue major arms brokers ni nani ndio uje kujua huu mchezo ni mkubwa kuliko watu wanavyofikiria. Vita mbaya muungwana.
Ndugu yangu, ukisoma zile topic mbili , utaona analyze yangu juu yaa Israel na nchi jirani, hasa hasa kuhusu maji ya Nil. Tanzania haijawahi kua kibaraka ya Israel hasa hasa kuhusu Israel-Palestine, lakini majirani vibaraka tupu.