sina uhakika na hili, kama uganda wanapata hizo silaha toka israel, kwanini na sisi watz tusifanye dili tupate silaha toka hukohuko israel au toka mataifa mengine kama china na kwingine, kwani kupata silaha ni jambo la kutisha sana? kama wenzetu wakipata silaha toka israel, sisi pia tunaweza kupata silaha toka ufaransa, china etc, na nchi huru kama ugana na tz kufanya makubaliano ya kupata silaha si jambo la ajabu. tungekuwa na hela hata sisi leo hii tunatakiwa kununua tank mpya na nyingi, ndege za vita mpya na nyingi, silaha lazima tuwe tunanunua. lakini sidhani kama tz ipo kwenye hali ya hatari ya kutumia mipesa kununua silaha kwasasa hivi, kwasababu bado sijaona threat yeyote ile toka nje. rwanda haitakuwa na sababu yeyote kkupigana na tz, uganda haitakuwa na sababu yeyote kupigana na tz, kenya vilevile, malawi hawatakuwa na sababu. jua kwamba, hata kama nchi yeyote majirani iwe rwanda au malawi ikiishambulia tz, its just a matter of weeks or months hata kama watakalia maeneo yetu, tutajioganise na kuwaondoa wote. wala tusitishwe. hata hizi hali ya hewa kati yetu na wenzetu wa east africa ni hali ya hewa ya kupita tu, nchi na nchi kupigana si kitu rahisi. hata nchi za nje zikiona tunaelekea kupigana kweli zitakuja kutupatanisha tu kwasababu wanajua tutasababisha madhara makubwa. china haiwezi kukubali hata siku moja maslahi yake tz yapotee, hata marekani na uingereza.
kuna watu wanasema malawi iko supported na uingereza kwasababu kampuni inayotafuta mafuta na gesi nyasa ni ya waingereza, wamesahau kuwa mojawapo ya makampuni yaliyogundua gesi mtwara ni ya waingereza, hivyo waingereza wagawe silaha malawi ili kuiipiga tz ambayo hukuhuko wanataka kuvuna gas watakuwa na akili kweli? tz tungekuwa hatuna maslahi yeyote na uingereza wangeshawasapoti malawi mda, lakini uingereza imewekeza sana tz pia imegundua gas.
way forward kwa watz kwa leo hii ni kujizatiti katika miundo mbinu ya reli, bandari na kielimu mashule na vyuo vikuu watoto wetu wasome, tuwe na wasomi wengi ili wa serve kwenye secta za mafuta na gas, na tuwe na ushindani kwenye east africa community au sadc. tukiendelea kupoteza muda kujadili vita na rwanda au wivu na ushindani wa jadi na kenya, wenzetu hawana muda huo wanapiga kazi, sisi porojo tusiziendekeze.