Propaganda za CCM ndani ya ch 10 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Propaganda za CCM ndani ya ch 10

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mohamedi Mtoi, Sep 5, 2012.

 1. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #1
  Sep 5, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Waziri Nchimbi anatoa maelezo jinsi chadema inavyo hatarisha hali ya amani ya nchi.

  Angalia ch 10
   
 2. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Hahahahahahaa!!!
  Ukitaka kucheka siku hizi we angalia makada wa ccm tu, komedi tosha.
  Amejisahau ni waziri? Hakuna sheria nchi hii?
   
 3. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #3
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Anasemaje wengine hatuna TV!
   
 4. MBWA HARUKI

  MBWA HARUKI Senior Member

  #4
  Sep 5, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyo ndio Dr.Love Nchimbi bwana, ila kitu ambacho kinanipa faraja ni kuwa nina uhakika muda wa CCM kukaa madarakani umekwisha kwahiyo tutasikia na kuona mengi ila ule mwisho waja! 2015 CCM ndio bye bye!!!!!!
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Yaani Channel ten bado wanampa airtime huyo kiongozi wa wauaji wa mwandishi wao.
  Shame on Channel ten na ukibaraka wao.
   
 6. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #6
  Sep 5, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,638
  Likes Received: 2,065
  Trophy Points: 280
  Tatizo hawaangalii tatizo la msingi ambalo ni kuuwawa kwa mwandishi Daudi kulikofanywa na police, wao wanakuja na hoja kama CDM asingefanya ufunguzi Nyororo kifo kisingetokea (hizi ni kauli zisizo za kisayansi) na ukiona mtu anatumia neno NINGE, ANGEfanya hivi, NINGEjua huyo mtu ana kila dalili ya kujuta kwa kile kilichotokea,

  Kinachoangaliwa ni kifo cha mwandishi kwani hata vitani ambapo mataifa mawili maadui yanapigana lakini waandishi wa pande zote mara nyingi huwa hawapigwi na marehemu kwa Iringa ni mtu ambae shughuli zake zinajulikana hata kama asipovaa nguo au beji inayomwonyesha kwamba yeye ni mwandishi wa habari.

  Kama ingekuwa ni mwananchi mwingine labda wangejitetea kwa kusema walikuwa wanawatanya ndipo miongoni mwao wakawa wanarusha mawe hivyo polisi wakatumia nguvu ya ziada, sasa kwa mwandishi tatizo lilikuwa nini mpaka wakawa wanampiga na hata kama walitoleana maneno si mazuri kwanini wampige wakati kwa idadi yao ni wengi kiasi cha kumdhibiti tu na kumpeleka sehemu husika, Nchimbi na jeshi lake hawakwepi hapa wasihamishe hoja kwa CDM,

  Hoja ibaki palepale ya kumuua mwandishi kwani WAMETUNYIMA HAKI YETU YA KUPATA HABARI kwani kwa Iringa mara nyingi coverage za video huwa anafanya yeye na ndio maana hata yatokanayo na ule mkutano hayajaonekana kwenye vituo vingi vya TV (huenda alikuwa na picha nyingi za video ambazo zimekwenda zote baada ya kufariki)
   
 7. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #7
  Sep 5, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Nchimbi ni janga la Taifa
   
 8. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #8
  Sep 5, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Huyu Nchimbi kweli alighushi huo udaktari wake wa mashaka. Kama siyo jina la baba yake, kama Januari Makamba, Hussein Mwnyi, Ridhiwan Kikwete na wengine wengi wanaobebwa na majina ya baba au mama zao, asingefika hapo alipo. Ni ajabu kwa nchi yetu kukuta watu wenye kila tuhuma wakipewa nyadhifa ambazo hawaziwezi.

  Hebu angalia walioghushi kama Didace Masaburi meya wa jiji la Dar, Makongoro Mahanga, Mary Nagu na wengine wanavyopewa nyadhifa nono wakati wameoza. Kinachohatarisha amani ya Tanzania ni serikali dhaifu na fisadi ya Kikwete iliyotokana na wizi wa EPA na kuchafuana.

  Huwezi kuilaumu CDM wakati CCM ndiyo wanaoamrisha polisi waue watu na kutowashughulikia. Ni ajabu kuwa serikali chafu kama hii bado inaendelea kukaa madarakani ikinyanyasa na kuua umma. Tuseme kwa lugha nyingine wanaohatarisha amani ya nchi ni watanzania wanaovumilia uoza na ufisadi huu wa kutisha.

  Amkeni wananchi mjitetee badala ya kungoja miujiza kutokea. Kama watu makatili kama Gaddafi walianguka wao CCM ni nani hadi watusumbue?
   
 9. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #9
  Sep 5, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kwani anasema nini huyu mpuuzi?
   
 10. F

  Froida JF-Expert Member

  #10
  Sep 5, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Wanaogopa nini si wanasema Chadema ndio wameua,wameshahukumu tayari kwa nini wasiwapeleke mahakamani na kufuta chama chao mara moja eti walisema nchi haitatawalika sasa kwani ni uongo watu hawajiwezi zaidi ya wizi wa rasilimali hakuna hat Think tank wa serikali na CCM au ndio wote wana malaria ya ubongo
   
 11. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #11
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Anatoa maelezo mengi ya nini angesubiri tume aliyounda italeta majibu.
   
 12. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #12
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Niliposikia Waziri wa Uchukuzi wa Zanzibar anajiuzulu baada ya Boti kuzama, Nikasema amefungua mlango wa uwajibikaji. Yule waziri hakuwa na kosa hasa ukizingatia ile Boti ilikuwa inatoka Dar-es-salaam, lakini alijua what is responsibility about.
  Leo kumsikia PhD holder anatumia lugha za If condition.

  Kama Chadema wengehailisha mkutano wao, Mwandishi asingekufa. Nani nakuuliza Mh Waziri na IGP
  Mh Nchimbi! what if Police wangesubiri mpaka mkutano kuisha na kuwakamata Viongozi wa CDM, Mwandishi asingekufa
   
 13. M

  Makupa JF-Expert Member

  #13
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  nchini kenya zile Phd zenye utata huwa zinaandikwa hivi 'Phd' je Nchimbi ya Phd yake ni ipi
   
 14. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #14
  Sep 5, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  huu ndo ukenge wenyewe sasa.
  Umeunda tume ili ilete majibu, kama una majibu kwanini umeunda tume?

  Hivi hawa makada wa ccm wana problem gani? Vichwa nazi au akili imeingia mchuzi?
   
 15. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #15
  Sep 5, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Nimshukuru Nchimbi maana leo ndio nimejua vifo na propaganda zilizoko nyuma ya chadema kuhusu vifo vilivyotokea kwenye mikutano! Ameongea mengi lakini hakugusa kabisa kuwa polisi wamehusika kumuuwa Mwangosi! Kama kawaida kauli niza jumla jumla, eti "Chadema wajitasmini upya maana mikutano yao mitatu WAMEUWA WATU WATATU.

  Kauli zake ukiziangalia kwa undani hazitofautiani sana na kauli za Shigella alipo sema kuwa "Hawa ni chadema tu, mbona kila siku polisi wapo morogoro mauwaji hayakutokea?" Lakini pia kauli zake na kauli kwenye tamko la Nape hazina tofauti sana maana zote zinalaumu Chadema badala ya wahusika halisi walio uwa raia wasio kuwa na hatia.

  Kauli iliyonifanya ni mdharau Nchimbi. "Hakukuwa na haja ya chadema kufanya mkutano wakati zoezi la sensa linaendelea" lakini wakati huohuo hakutoa kauli kuwa ccm siku hiyohiyo walizindua kampeni bububu wakati chadema wakifanya mkutano wa ndani Iringa, hakusema kuwa chaguzi za ccm zimefanyika ikiwa ni pamoja na kuibuka kwa vurugu uchaguzi wa uv ccm wilaya ya Kinondoni.

  Akiendelea kumwaga propaganda kuwa chadema walizuiwa kufanya mkutano akasahau kusema kuwa siku hiyohiyo Fiesta ilinguruma Mwanza na ikalondwa na polisi kama ulivyo llindwa uzinduzi wa bububu.

  Kwa haya machache kama unafikiri kwa akili za kawaida bila kuwa na shahada za udaktari kama Nchimbi lazima upate jibu moja kubwa kuhusiana na propaganda zake na wenzake (Nape na Shigella), yaani mauwaji + kauli zao (nchimbi+nape+shigella) + zile tuhuma alizotoa Dr Slaa kuwa kuna mbinu chafu za kuvuruga mikutano na taswira ya chadema = Mpango maalumu wa kuiangamiza chadema.


  Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums.
   
 16. V

  Van Dickson Member

  #16
  Sep 5, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nchimbi hewa tu..
   
 17. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #17
  Sep 5, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,571
  Likes Received: 571
  Trophy Points: 280
  mbinu za kuuwa watu zimeidhinishwa na cc ya ccm kabisa, maana hata mtu reputable kama prof mwandosya sings the same song
   
 18. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #18
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mkuu kama unadhani ulikuwa unawajua hao wapuuzi Channel 10, sasa basi ulikuwa hujawaona...

  We tuangalie hili sakata hadi mwisho.... Wameshaanza kumkana hadi marehemu eti "alikuwa hajaajiliwa" unaweza tu ukajiuliza kama hilo lilikuwa na umuhimu wowote kulitangaza kwa kiherehere vile!
   
 19. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #19
  Sep 5, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,571
  Likes Received: 571
  Trophy Points: 280
  Shigela, nape, mwandosya, nchimbi nk woote wanasema cdm wanaua watu! Kweli hamna aliyenusurika ccm! Wote akil 100% -100%
   
 20. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #20
  Sep 5, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,817
  Likes Received: 36,921
  Trophy Points: 280
  Too late, watanzania wameshajua kuwa ccm wanafanya kila namna kubaka demokrasia.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
Loading...