Ya, 29/10 Haiwezi kusafishwa na propaganda

Ya, 29/10 Haiwezi kusafishwa na propaganda

Joined
Dec 18, 2019
Posts
76
Reaction score
137
Muda unaweza kusonga mbele. Kauli za kisiasa zinaweza kubadilika. Ripoti za ndani zinaweza kutungwa kwa lugha laini.

Lakini 29/10 ni kumbukumbu ya kudumu ndani na chamber za kimatifa

Na sasa dunia inaanza kuonyesha kuwa haikusahau.

Wiki hii, maseneta wa Marekani kutoka pande mbili tofauti za siasa zao wamewasilisha muswada wa Reassessing the United States–Tanzania Bilateral Relationship Act.

Hizi si story ya kijiweni au Twitter.
Si porojo za “wazungu wanaingilia.”

Ni hatua rasmi ndani ya Senate ya Marekani inayotaka:
  • mapitio ya mahusiano ya Marekani na Tanzania
  • kutajwa kwa waliohusika na ukandamizaji
  • uwezekano wa visa bans na asset freezes
  • kusitishwa kwa baadhi ya misaada hadi mageuzi yaonekane
Na msingi mkuu wa muswada huo ni nini?
Matukio ya 29/10.
Hapa ndipo propaganda inapogonga ukuta wa ukweli.

Unaweza kuspin narratives ndani ya mipaka yetu.
Unaweza kutumia vyombo vya habari kujisafisha.
Unaweza kuita kila sauti pinzani “wachochezi.”

Lakini huwezi kufuta rekodi ambayo tayari imeingia kwenye meza za sera za kimataifa.

29/10 sasa si doa la kudumu mitaani.
Ni rejea ya kidiplomasia kimataifa,
Ni kumbukumbu ya kisheria.
Ni hoja inayotumika kujenga miswada ya vikwazo.

Hii ndiyo maana nasema:

29/10 haiwezi kusafishwa na propaganda.

Ukweli una tabia moja ya ajabu:
Unaweza kuuchelewesha, lakini huwezi kuuzima.

Kama kila kitu kilikuwa safi kama ilivyosemwa, kwa nini Senate ya Marekani leo inajadili sanctions?


Kama kila kilichotokea kilikuwa “udhibiti wa kawaida wa usalama,” kwa nini dunia inauliza accountability?

Maswali haya hayawezi kujibiwa kwa press conference za masheikh na wachungaji wahuni.

Historia hujiandika yenyewe.

OVER!
 
Back
Top Bottom