Propaganda: KItabu Cha Abdul Sykes Kinauzwa Misikitini

Propaganda: KItabu Cha Abdul Sykes Kinauzwa Misikitini

Hiki kitabu kimeelezea kinagaubaga jinsi wazee wetu wa Gerezani walivyopigania uhuru wa Tanganyika?
Kyenju,
Kitabu kina historia ya wazalendo kutoka kila pembe ya Tanganyika waliopigania uhuru wake kwa waume.
 
Mzee Mohamed Said..

Huyu Ali Mwinyi Tambwe Kuna mahali nilisoma alikuwa askari wa Siri wa Uingereza (Spy), vipi ahusike tena kumuingiza Nyerere ndani ya TAA?
Proved,
Alikuwa Special Branch na kuingia TAA ndipo anapopata taarifa zote.

Abdul Sykes alipomchukua kwenda Nansio hakuwa anaijua kwani alikuwa Secretary wa Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika (Umoja wa Waislamu wa Tanganyika).

Hii ilikuwa siri kubwa sana hakuna aliyemuhisi kuwa akipeleka taarifa serikalini.
 
Kamanda...
Haya niandikayo hapa nimeyatoa katika Seminar Paper ya Daisy Sykes aliyowasilisha University of East Africa Dar es Salaam Campus akiwa mwanafunzi wa History and Education mwaka wa 1968.

Daisy anaeleza katika paper hiyo maisha ya babu yake Kleist Sykes (1894 - 1949).

Na Daisy hayo kayapata katika mswada wa kitabu cha maisha ya babu yake aliyoandika kabla hajafariki mwaka wa 1949.

Paper hii ipo Maktaba Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, East Africana.

Kleist Sykes hawezi kuandika uongo.
Paper ni mawazo ya mtu tu.
 
Paper ni mawazo ya mtu tu.
Kamanda...
Hakika ni kazi ya mikono ya binadamu kama yalivyo yote ya sisi binadamu.

Jambo la kushukuru ni akili uliyopewa na Mwenyezi Mungu.

Unasoma paper na akili yako itakusaidia kujua haki na batil, ukweli na uongo.

Hapa ilikuwapo historia iliyokuwa imejaa matatizo.

Ndipo nikaandika yale yaliyokuwa ndani ya ubongo wangu niliyohifadhi toka utoto wangu.

Haya mmeyasoma na mnaendelea kuyasoma.

Akili zenu zinashughulika kutafuta ukweli.
 
Kamanda...
Hakika ni kazi ya mikono ya binadamu kama yalivyo yote ya sisi binadamu.

Jambo la kushukuru ni akili uliyopewa na Mwenyezi Mungu.

Unasoma paper na akili yako itakusaidia kujua haki na batil, ukweli na uongo.

Hapa ilikuwapo historia iliyokuwa imejaa matatizo.

Ndipo nikaandika yale yaliyokuwa ndani ya ubongo wangu niliyohifadhi toka utoto wangu.

Haya mmeyasoma na mnaendelea kuyasoma.

Akili zenu zinashughulika kutafuta ukweli.
Ungekuwa unajitambua kiakili. Mbona tangia uelekeze juu ya uslamu na wapigania uhuru wa Tanganyika. Hakuna mwana Tanu au MwanaCCM anayekukubali. Historia yako ni tofauti ya Tanu na CCM.
 
Ungekuwa unajitambua kiakili. Mbona tangia uelekeze juu ya uslamu na wapigania uhuru wa Tanganyika. Hakuna mwana Tanu au MwanaCCM anayekukubali. Historia yako ni tofauti ya Tanu na CCM.
Kamanda...
Nifahamishe kipimo cha kukubalika.
 
Hicho kitabu kinamhusu Sykes au waislamu? Itoshe kusema wewe mzee ni mpumbavu uliyejaa udini wa kishenzi. Umeacha tabia yako ya kula nguruwe kwa siri?
 
Mama...
Naelewa hamaki zako.

Kitabu kinaitwa: "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika," Minerva Press London (1998).
 
Kwa kipindi kirefu kitabu cha Abdul Sykes kilikuwa hakipatikani kwa kuwa nakala zilikuwa zimekwisha (out of print).

Hiki ni kitu cha kawaida kwa kitabu kukosekana.

Kitabu cha Abdu Sykes ni kitabu kilichozingirwa na ubishani mkubwa toka mara ya kwanza kilipochapwa kwa Kiingereza mwaka wa 1998.

Sababu kubwa ya msuguano huu ni kuwa kitabu hiki kilieleza mchango wa Waislamu katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Majibu yakaja nikashutumiwa kwa kile kilichoitwa udini na kuandika uongo na uchochezi na maneno mengi yakasemwa.

Hapa JF tukawa na mjadala uliochangiwa na watu karibu milioni moja na ukadumu kwa miezi sita bila kusimama hata siku moja mwandishi akikabiliana na watu wenye hamaki.

Hatimae mjadala ulifungwa na maisha yakaendelea.

Juma hili nikawatangazia jamaa hapa ukumbini kuwa kitabu cha Abdul Sykes kimeingia nchini na nikaeleza wapi kinapatikana.

Vita vikarejea upya haba jana nikishutumiwa kuwa kitabu hicho ni cha udini na kuwa kinauzwa misikitini.

Kila aliyenyanyua kalamu hicho ndicho kilichoelezwa.

Mimi niliwajibu kuwa kitabu hakiuzwi misikitini na nikaeleza maduka ambayo kitabu kinauzwa lakini hakuna aliyenisikia.

Nyimbo ikawa ni hiyo kitabu kinauzwa misikitini hili likisemwa kwa hamaki pamoja na maneno mengine yasiyopendeza.

Leo ssubuhi kwa bahati napita Maktaba nikakutana na picha ya kitabu cha Abdul Sykes picha niliyopiga kitabu kikiwa duka maarufu la vitabu Mtaa wa Samora - Mkuki na Nyota Bookshop.

Picha inazungumza maneno 1000.

Picha hiyo hapo chini ya kitabu cha Abdul Sykes kikiwa Mkuki na Nyota kinauzwa.

Naamini hili litamaliza mjadala na propaganda iliyokuwa ikienezwa dhidi yangu na kitabu changu:

View attachment 3627431View attachment 3627435

"Baada ya Iddi Faiz Mafungo kwenda Tanga kupokea fedha kutoka kwa Mwalimu Kihere fedha za safari ya Julius Nyerere kwenda UNO zikawa zimekamilika.

Iddi Faiz yeye alikuwa Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika na pia Mweka Hazina wa TANU na ndiye aliyekuwa akikusanya michango ya safari ya Nyerere UNO.

Bwana Abdul akaniambia, "Abbas safari ya Nyerere UNO imewiva na atahitaji kudungwa sindano ya chanjo kwa ajili ya safari.

Mimi hawa Waingereza siwaamini hata kidogo kwa hiyo hakikisha kuwa hadungwi sindano lakini tupate cheti kuwa kapigwa sindano kwa ajili ya safari.

Hili jambo ni siri yetu sisi watu watatu mimi, wewe na Nyerere mtu yeyote asijue."
(Mazungumzo na Abbas Sykes miaka mingi kupita baada ya kitabu kuchapwa)
Miaka ilee naanza kusoma makala zako nilikuwa miongoni mwa wanaohamaki.

Nilijipa muda kusoma kwa umakini kila chapisho na nikaja kugundua kuwa mengi uliyoyaandika yana mantiki na ukweli usiopingika.

Wapuuze wanaokushambulia, hauna haja ya kujitetea wala kujieleza kwa sababu chapisho zinajenga hoja. Ni wajibu wa wanaokuhamaki leo kujenga hoja dhidi ya machapisho unayoweka kwa kuweka wanayoona ni sahihi.

Kizazi chenyewe kinakwepa usomaji.

Mzee Saidi, endelea kuandaa machapisho yanayoibua ukweli na usahihi wa Tanzania yetu. Punguza kuwajibu wanaobamaki.

Nakuunga mkono Mkristo mimi
 
Wazee kama Hawa wana mchango mdogo sana kuendelea Kwa hii nchi
Walitaka nchi ya Al Islamia fi Tanganyika.

Yaani wanaume wote tufuge mindevu na kupaka ina.

Wote tuvae kanzu na makobaz.
Wote tuna na akili mbovu kama Sheikh Mwaipopo na Mazinde.

Halafu tuanze kulipuana kama huko Yemen.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom