Projects kubwa ziwe na wahandisi wa nje!

Katika masuala ya uhandisi kuna changamoto nyingi ambazo ni kama zifuatazo.
1. Bajeti ndogo sana katika ujenzi wa miradi kwa hiyo miradi inajengwa chini ya kiwango. Au mradi unakuwa na design life ndogo.
2. Rushwa na 10%, pamoja na bajeti ndogo bado hiyohiyo ndogo bado watu wanataka rushwa na mgao na hivyo kuwakandamiza wahandisi zaidi.
3. Kukosekana kwa taarifa za kihandisi katika sehemu husika. Tanzania kuna upungufu wa taarifa ambazo zinatumika kusanifu miradi mfano kina cha maji ndani ya mto kwa kipindi cha miaka 100 au kasi ya maji katika mto kwa miaka 100. Taarifa kama hizo nchini hazipo na hazina usahihi na wengi wanajenga kwa kubahatisha tu.
4. Mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanaleta mvua nyingi kupita kiasi ambazo zinatarajiwa kwa hiyo ikinyesha mvua kama hizo lazima miundombinu lazima iharibike.
5. Formula za kudesign nyingi zimetungwa na wazungu ambazo haziendani na hali halisi ya kiafrika. Mfano mito ya kiafrika ni mito korofi sana kuzidi ya kizungu, mito ya kiafrika mvua ikinyesha mto unaweza kuongezeka kina na pia mto unaweza kupanuka zaidi na hivyo kuvunja daraja kabisa ila katika kusanifu kutumia fomular za kizungu wao wanaanglia kina cha mto pekee ila mpanuko hawaangalii. Pia mito ya kiafrika kutokana na kutotunzwa na shughuli za kibinadamu mito inakuwa na madongo na matope mengi hivyo maji yake yanakuwa na nguvu sana kuliko formular.
6. Wanasiasa wamejigeuza wahandisi kwa hiyo tegemea madudu tu.
7. Uwezo mdogo wa wakandarasi wazawa hasa mitaji na mitambo ya kujengea kwa hiyo inaweza kusababisha ujenzi uwe chini ya kiwango. Hao wakandarasi kutoka nje wanapewa mitaji toka nchi zao na mikopo yenye riba ndogo kama 3% wanapewa mpaka mitambo yenye thamani ya 30B tshs kwahiyo mradi wowote mkubwa wanaweza kujenga.
8. Kusoma kwa kingereza kunafanya watu tukariri kuliko kuelewa. Bora tungesoma kwa kiswahili tu. Hao wachina wanasoma kwa kichina mpaka chuo kikuu ndio wanaojenga madude ya kushangaza ulimwengu. Tusome kwa kiswahili tu.

Sijapinga wazo lako ila kumbuka hata hao wataalam toka nje ya nchi na wenyewe kuna mahali wanakwama tu mfano ni daraja la hapo jangwani hilo daraja limejengwa na Strabag ambao ni wakandarasi toka nje ya nchi lakini bado mafuriko yapo palepale, je usomi wao kwa nini haujasadia? Mimi nadhani ni formula walizotumia ambazo kwao ni sahihi ila kwa mazingira ya jangwani sio sahihi maana pale jangwani ni mdomo wa kupeleka maji baharini na madongo yanajaa pale.



Halafu hao wahandisi wa nje wakija bongo huwa wanakuwa wachoyo kutoa ujuzi wao na uzoefu wao maana wanakuwa na hofu kwamba wanaweza kukosa kazi. Labda watanzania waende kusoma huko nje na uwekwe mfumo wa kuwalazimisha kurudi nchini kufanya kazi maana wabongo ukiwapeleka wanazamia kabisa na wanagoma kurudi.

Nimemaliza.

Nimependa hoja zako mkuu...👍👍👍👍…….

Ila pengine hujanielewa,sijasema wahandisi wa nje waje wa replace wahandisi wetu wa Tanzania, ila waje wafanye kazi pamoja ila kupeana uzoefu...

Hili la shule kutumia lugha ya Kiswahili ni swala tunalopigia kelele kila siku,is either tuwe na lugha ya Kingereza kuanzia shule za awali/kindergarten ,primary secondary hado chou kikuu,.ama Kiswahili kitumike kwenye hizo ngazi zote...tena afadhali uhandisi,mimi naogopaga labda hata madaktari wana kremu material na machache yanaingia..hivyo tunatoa madaktari sio wataalamu…………………………...

Wanasiasa kuingilia utaalamu na budget kuwa ndogo, naona limejitokeza mara nyingi kwenye hii topic,sio swala la kupuuza,viongozi tunawaomba mlifikirie hili,tunalipa high price pale mambo yanapoenda kombo,kumbe tungeweza ku avoid if nmngetoa budget inayoendana na mradi..na kutoingiza siasa kwenye mambo yanayohitaji utaalamu!
 
Back
Top Bottom