zege la nyasi
JF-Expert Member
- Sep 18, 2018
- 928
- 1,242
waswahili wanasema utamu wa ngoma, ingia kati ucheze. kwa mtu alie nje ya hii sekta ni rahisi sana kuwatupia lawama wahandisi wa ndani. ila walioko ndani wanaujua ukweli. Daraja linavunjika kwa kukosa ukarabati ambao budget yake ni mpaka wanasiasa waamue kuitenga kwa muda wanaopenda wao. Then wakija hapo eneo la tukio unasikia 'hakikisheni daraja linakamilika ndani ya siku saba'. Anaetoa hayo maagizo ni mwanasiasa ambae pengine amesomea ualimu wa kemia na hajafanya utafiti wowote kujua mchakato mzima unahitaji muda kiasi gani. Kitakachofanyika ni bora liende!
Nafikiri bongo wanasiasa wanashiriki kuharibu taaluma