Project Funga Mwaka! 3D animation

Project Funga Mwaka! 3D animation

Kaka, nakuheshimu, unaonekana ni mtu mzima, lakini kuambiana "weken makalio chini" kwangu mm ni offensive, halafu naona ume assume mambo mengi kweli, unajuaje kama mm sijifunzi modelling, hata ukienda kwenye studio kubwa ILM for example sio kila mtu ni modeller, kuna wanaofanya hvyo, kuna wanaospecialise kwenye RnD, kuna wanaospecialise kwenye animation, kwenye lighting, rigging, na mengine kibao. Sasa acha kuongea as if kila mtu anafata unacho amini ww. MM binafsi nataka kua VFX artist, sio mtu wakutengeneza katuni. So stop ku assume mno, be real. And dont criticize what you dont understand!

Na mm hyo yote ni mikono yangu, Kosa moja ulilofanya mkubwa wangu niku under-estimate mtu, i`m just 18, and believe me i use my time well, nikija kufikia umri Mungu anijalie tu, ila....


Wickerman,

Umri wangu mimi ni miaka 34. Nimeshtushwa sana na response yako juu ya comment yangu. Sasa naomba nijitetee.

OFFENSE YA NENO MAKALIO
Sijui kanuni za JF zinasemaje specifically juu ya neno hili. Nadhani halina shida kwa kuwa makalio ni neno jepesi mbadala wa neno m*t*ko ambalo kwa kawaida ndilo huwa offensive. Pili, makalio linaweza kuwa tusi ikiwa linakusudiwa kuwa hivyo, mfano ukiwa na ugomvi na mtu halafu akakwambia "makalio yako!!" au hata "mdomo wako!" basi amekusudia kukukasirisha hata kama katumia maneno ambayo si matusi. Sikutaja makalio pekee nimetaja na migongo nikimaanisha kujitesa/kufanya bidii/kutenga muda/kukaa kitako kujifunza kwa kuwa wewe ni shahidi mchakamchaka ulivyo katika haya tuyafanyayo. Hivyo neno makalio sikulikusudia kuchambua makalio kama kiungo ila kama utaratibu wa binadamu kukaa chini kujifunza. Kwanini nikutukane? Kwa miaka yangu 34 sijajiona mzee wa kuogopa kusema neno hili, tena katika muktadha huu, haujawahi kusikia Saratani ya matiti?

ASSUMPTIONS KUWA HUJIFUNZI MODELLING/ILM, WETA, DIGITAL DOMAIN na SPECIALIZATION
Kwanza nakubaliana na wewe juu ya specializations za watu katika studio kubwa. Ni kweli kabisa. Hata hospitali kuna madaktari wa mifupa, meno, wanawake, watoto n. k. Hata katika mpira kuna washambuliaji, wakabaji, viungo n.k. Ni specializations hizo. Uko sahihi kabisa. Na pia hakuna mtu duniani anayeweza kila kitu kwa kiwango cha juu. Haiwezekani. Lakini niseme tu kuwa hata hao madakatari bingwa wana idea juu ya tiba zingine na mambo ya msingi/basic/fundamental. Hata wahsmbuliaji katika soka wana idea ya ukabaji. Hata specialists wa modelling wanai dea na animation kwa kuwa kuna models ambazo ni nzuri kwa kuziona ila ni mbaya kwa kuanimate.
Mojawapo ya thread zako https://www.jamiiforums.com/tech-gadgets-and-science-forum/558784-you-gotta-watch-this.html umesema mostly huwa unadownload models nakunukuu "........ and no sija model mwenyewe, i download models mostly." Sasa je hili ni kosa? HAPANA SIYO KOSA kwa kuwa hakuna anayeweza kufanya kila kitu. Hata Andrew Kramer hawezi kumodel binadamu na ana modellers wake, na hana mpango wa kujifunza lakini makali yake we mwenyewe unajua. Hollywood wanamjua.

Ila kwa mazingira yetu ni vizuri sana kujua kumodel vitu vya msingi na huenda hata wewe unajifunza kama ulivyohoji "najuaje kuwa hujifunzi modelling" ila ni mtego unaowanasa wengi kutotenga muda wa kutosha katika modelling kama ambavyo nimekutuhumu na mwishowe moto wote huu umewaka.

Kuhusu wewe kukusudia kuwa visual effects artist nina mengi ya kusema ila kwa presha uliyonibebesha nalazimika kuwa mpole.

AND DONT CRITICIZE WHAT YOU DONT UNDERSTAND, UMENI-UNDERESTIMATE
Narudia kusema, ndiyo maana nikakuuliza wewe unafanya haya ili iweje? Unataka kufanya nini katika animation? Hata Good Guy nimemuuliza hivyo. Kwa hiyo kwa kujua kuwa unataka kuwa visual effects artist maybe next time ninge-comment basi ningeweka wazo kuwa najadili kazi za visual effects aspirant.

Kumu-underestimate mtu ni kujipa mawazo "Huyu hawezi na hatafanya lolote." Ndivyo nijuavyo. je ndivyo nilivyosema au hata kuashiria indirectly? Ndivyo kweli?
wickerman si mimi niliyekwambia, ".....
siku nyingine nitakudai...." katika post namba 12 hapo juu nikimaanisha siku nyingine nakudai maboresho kwa maana nategemea utajifunza na kwenda hatua nyingine? Hii si ishara kuwa najua mambo yatakuwa mazuri zaidi? Na hata katika sentensi ya kwanza ya post hiyo ya 12 nimesema hivyo juu ya models?

Ni kweli usemavyo "i'm just 18" kwani kuwa na umri huo ni dhambi? Kwamba huwezi? Kwa lipi? Kwamba wewe ni mdogo? Kwani mtu wa 18 years ni mdogo ki-hivyo kweli? Mi nakuona mkubwa.

LAWAMA ZANGU KWAKO WICKERMAN

Kweli wickerman kwa muda niliotenga kujadili thread yako, kutype (niko slow) na kusema nini nimependa na kwanini hatimaye inaishia una-pick offenses? Kwanini umefanya hivi?

Nikwambie tu mi naona uko lucky. Kwa kawaida watu hawacomment kwa details zaidi ya kusema good or bad. Nilipojiunga JF September 2010 kwa ID ya 3D. post yangu ya kwanza niliuliza juu ya mambo ya 3D lakini sikupata response nzuri na wengine walipost mambo mengine hadi wakaja akina kotinkarwak kuokoa jahazi then baadaye wakaja aspirants wengine kama Lukansola. Ni rare kupewa long comments positive na negative.

Mi nawish kupata watu wa kunicriticize ila wengi wanaogopa kuni-disappoint. Mi napenda kuambiwa sababu za kupongezwa au kulaumiwa.

NAOMBA RADHI
Natumia nafasi hii kukuomba radhi wewe binafsi wickerman pamoja na wengine ambao wamekwazika na yale niliyopost. Nikiri tu kuwa nilisita sana kuweka picha na video kwa kuwa huwa zinadiscourage baadhi ya beginners (hasa kama wameweka efforts sana na hwajafanikiwa) pia ni rahisi kuonekana unajisifu katika thread za watu wengine.
NAOMBA RADHI.

Mwisho, nimeamua kujiondoa katika thread hii na kama watu wangekuwa hawaja-niquote basi ningedelete kila nilichopost. Leo Jukwaa la Sayansi na Teknolojia limeni-disappoint sana.

NIMESIKITIKA SANA.
MUNGU ATUSAIDIE.

NAKAA PEMBENI..
 
Last edited by a moderator:
Wickerman, I can feel in the presence of your position! it was not supposed to be like that, pole just be humble and keep moving!

Mzee Malima, yamalize mkuu tusonge mbele huenda mkafikia mahala pa kushirikiana kibiashara na mkafanya mambo makubwa sana, beyond imagination trust me!

Hapana mjomba Kiresua, nimejisikia vibaya sana. Mwenyekiti wickerman hajanitendea haki. Kanitimua kamati kuu bila kuniruhusu kujitetea. Huwa ni rare sana mimi ku-comment mambo JF. Siko Facebook wala Twitter. Na normally na-comment huku Sayansi na Tech. Huku nako nimewashiwa moto. Hapo nina changu kweli? Mambo ya mitandaoni nadhani mnayaweza nyie bana.
 
Last edited by a moderator:
Hapana mjomba Kiresua, nimejisikia vibaya sana. Mwenyekiti wickerman hajanitendea haki. Kanitimua kamati kuu bila kuniruhusu kujitetea. Huwa ni rare sana mimi ku-comment mambo JF. Siko Facebook wala Twitter. Na normally na-comment huku Sayansi na Tech. Huku nako nimewashiwa moto. Hapo nina changu kweli? Mambo ya mitandaoni nadhani mnayaweza nyie bana.
Mkuu, MM kama binadamu, i have temper, na when i feel offended, it rises, Forgive me kama i made u feel that way. I felt angry haswa uliposema "Leo nawachana Live!" kichwan kwangu mm hii kitu haikukaa sawa kabisa. I dont really really like to quarrel with people (unless u offend me). kwahyo, plz usiseme kwamba nimekutimua, u raised my temper. So mkuu, mimi kama utasema kwamba haujitena thread hii, its okay, ila i hold no grudge towards u baada ya kusoma post yako, and once again, ukiamua one kutoa suggestions kwenye my works plz ur welcomed, lakini usitumie phrases like "Leo nawachana Live!" I`m really really sorry.
 
Hapana mjomba Kiresua, nimejisikia vibaya sana. Mwenyekiti wickerman hajanitendea haki. Kanitimua kamati kuu bila kuniruhusu kujitetea. Huwa ni rare sana mimi ku-comment mambo JF. Siko Facebook wala Twitter. Na normally na-comment huku Sayansi na Tech. Huku nako nimewashiwa moto. Hapo nina changu kweli? Mambo ya mitandaoni nadhani mnayaweza nyie bana.

hahaha Mkuu umetimuliwa kamati kuu? LOL

Dah nakuwa mediator sasa lakini Worth it kuwaweka w2 pamoja ni jambo jema!

Nimesoma kwa makini sana post yako, na nimekuelewa natuaini pia kila mmoja aliyesoma!

but naomba kuwaeleza watu kuwa bear with all type of people kwa maana wapo ili dunia niwe pahali pema pa kuishi! Mkuu nakusihi for the sake of this industry usikae pembeni tunakuhitaji sana sana.

Mm sina clue ya hii fani ila napenda kazi zenu na natamani TZ tuwe na magurus kwenye hii fani.

Mkuu nimekusoma kwa makini na kama utakumbuka nilielewa post yake na mambo mengi aliyosema na hata kueleza umri kn! YAH, lets go on! muelewe na tusonge mbele.... LAKN nakuomba UCITUMIE TENA Maneno ya mtaani yanakwaza watu

Wickerman, tafadhali rudi kundini naona LUGHA IMEGONGANA, Maneno yaliyotumika yakakwaza wengine
 
Back
Top Bottom