Labda nikuulize swali nililomuuliza pia
Good Guy ...
Kwanini unafanya yote haya? i.e. Unataka katika maisha yako ufanye animation zipi? Nakuuliza haya
ili uzito/makali ya comments zangu yaendane na makusudio yako. Kama
hukusudii kufikia viwango vya juu sana si sahihi kwa mtu kukosoa kana kwamba anawakosoa Pixar.
Kwa mfano mimi binafsi napigania nifikie si chini ya 50% ya Pixar na DreamWorks. Kwa kweli nakusudia 100% ya Pixar japo
najua wazi ni kama ndoto au haiwezekani ila aisee nisipungue 50% vinginevyo bora nikauze maji! Kabisa sitanii.. nikishindwa iwe kwa kuwa ubongo wangu umefikia mwisho
ila si kwa kuwa sikujaribu.
Sasa ili kuachieve hili nafanyaje?
- Kwanza nafuatilia kujua Pixar wana nini na skills zipi kuwafanya wafanye hayo wanayoyafanya. Hii inajumuisha idadi ya watu, skills zao, softwares zao na bidii zao.
- Pili, najiuliza sasa mwenyewe (bila kujidanganya) ninaweza kufanya nini na nini siwezi ukilinganisha na yale nayotaka kufanya. Na je, hayo nisiyoyaweza naweza kujifunza na nikayafikia kwa kiwango gani, na je nikiyaacha napungukiwa nini? Kuna Altenatives?
- Tatu, baada ya kujua nachotaka kufanya sasa nini utaratibu mzuri wa kujifunza? Nijifunze kwa mlolongo gani? Kimsingi 3D animation inapitia hatua hizi: 1. Modelling 2. Texturing 3. Lighting 4. Rigging 5. Animating 6. Rendering na bonasi ni 7. Compositing.
KWA FAIDA YENU (KAMA IPO)
Binafsi siwezi kumodel kila kitu. Hata binadamu/wanyama siwezi kabisa
kwa sasa ila
nitaweza baadaye. Nimeahirisha kuanza kuumba na kuhuisha (model and animate) binadamu
kwa kuwa nataka kukifanya vizuri sana. Naweza kuumba vitu vingi lakini zaidi nimeweka nguvu katika mazingira (environments) na objects ambazo si curved sana kama ndege na magari, hata hivyo naweza kumodel
nikilazimika ila si kwa kiwango nikitakacho (watu fulani wanaweza kusema mbona nzuri tu, mimi nataka zaidi).
Nitajifunza kumodel vitu vyote vya msingi: watu, magari, nyumba (naweza kwa kiasi nachoridhika, angalia hapo chini), wanyama, miti (isiyo na majani, yenye majani kuna softwares kama SpeedTree japo ni expensive), mawe (si mbaya kwa sasa) n.k. Hata kama nitakuwa nanunua models lakini ningependa kujua kuzimodel kama nitapata nafasi (Itabidi tu ipatikane). Kwa sasa nimebanwa na majukumu ya hapa na pale, animation nimeweka pembeni kidogo!
Watu wengi including wewe
wickerman,
leo nawachana live, mnakimbilia kuanimate bila kutaka kujifunza kumodel hata vitu
basic tu kwa kuwa motion ni kitu kinachofurahisha sana. Ninyi vijana, wekeni makalio yenu chini, pindisheni migongo mjifunze
misingi.. mambo si rahisi sana! Hata hivyo
muwe realistic na uwezo wenu, mnajijua wenyewe.. kinachonibeba mimi ni
passion/upenzi wa kupindukia na
perfectionism hivyo sisalimu amri kirahisi. Wakishindwa washindwe Pixar siyo mimi (joking!/not joking!). Lakini nikiri tu kuwa skills zingine kama kuchora zinanisaidia nifanye vizuri.
PICHA
View attachment 128960
View attachment 128961
NB. UKIWEZA DOWNLOAD HD version Uiplay offline ni better quality, binafsi nikiiplay youtube hata kama nta-turn on HD switch naona vituko tu. Hii si final version, ya mwisho huenda itatofautiana kidogo na hii. Sijamodel gari na mimea, vilivyobaki plus animation na compositing ni mikono yangu. Muziki nilipewa.
KILA LA HERI.