Profile ya Dr Slaa

Status
Not open for further replies.
Tunaona wazi huyu Slaa Ilmu yake ina mushhkeri kidogo kwani inatambuliwa na kanisa pekee. Angukuwa amesomea kwenye vyuo vya umma basi tungeona ni jambo la kawaida kwani amekaa uswahilini na kuona watu wanaishi vipi

- Mnaona? Wewe na nani?
- Kwa hiyo wewe na wenzako mnawatambua waliosoma vyuo vya 'umma' pekee? Ukisoma chuo cha umma ni lazima ukae uswahilini? Je waliosoma nje, private schools/universities nao hamwatambui?

Ataleta amani kweli au ataleta vurugu kama Chadema

Naona kama unachanga mambo hapa! Kwani Chadema "ina ilmu inayotambuliwa na kanisa pekee"?

Nina wasi wasi anaweza kuwa kama Rais Chiluba wa Zambia pale aliposema wazi kuwa Zambia ni taifa la Kikristo.

Kwa hiyo shida yako hapa ni elimu ya Dr Slaa au dini yake? Kwa vyovyote vile, katiba ya nchi yetu haimzuii Dr Slaa kugombea urais wa JMT hata kama PhD yake inatambuliwa na kanisa pekee.
 
Sijui asili ya majadiliano haya, lakini kwa mtazamo wangu wengi wa viongozi waliopo madarakani, na pia wanaofanya mambo makubwa sio lazima wawe wana hayo madegirii ya masters and doctorates. Ni kweli elimu inatakiwa, lakini alimu peke yake haina maana. kuna madokta wengi na maprofesa, lakini sio viongozi wa kisiasa, wa kutawala nchi. Ila angalia viongozi wengi wa nchi hawana hayo mambo ya udaktari, lakini wanaweza, na wamekuwa viongozi.

Hoja ya kuwa Slaa ni daktari au sivyo, sio gumu kulielewa. Kuwa na Doctorate hakuhitaji lazima uwe kwanza na Masters, yategemea aina ya elimu na mahali gani unachukulia taaluma yako.

Kuweza au kutokuweza kwa slaa kuwa raisi wa nchi kunategemea mambo mengi. Kwa mfano, huenda huyo anachongo kati ya vipofu. Je utachagua kipofu au mwenye chongo? Kama wakiwemo wenye macho kamili, timamu, na ukamchagua chongo, basi utakuwa wewe ndiye kipofu hujui unachagua nini?

Amani Nyoni.
 
Experience has shown that the country like ours no need to be so academically/proffesional to be a leader. Only you need is to be lucky like KIKWETE.
 
Kadri siku zinavyo enda naona vibaraka wa mafisadi madau yao yanapanda lengo ni kupumbaza vita ya ufisadi na kujadili sijui hajasoma amesoma PHD tunajua lengo lenu lipo wazi mnataka kuvuluga vichwa vya watu tu.
 
Huu ni uongo mkubwa sana. Hujui kitu wewe waseminari wanafundishaje. In fact kama Seminari wakianza form one 20 basi watamaliza 8 au chini ya hapo. Kwani wao huwa wanataka wale a div one tena zile kali tu. wengine huwa wanawaamisha waende mashule mengine.

Sasa wanafunzi hawa hawa wanaopata one za kutisha toka Seminary ukikutana nao UDSM hakuna kitu ni wa kaaida sana na mara nyingi wanafeli.

Ndio maana Seminari kwa kuliona hilo, wanaamua kuwapitisha kiujanja ujanja ili wapate Degree zisizoeleweka kwa kuwapitisha vyuo vya st...st colleges na st..Universities kama walivyofanya Kwa Slaa.

Kwa kupita njia hii utaona wao wanaandaliwa kuwa watumishi wa kanisa tena Katoliki maisha yote.

Sasa tatizo linakuja pale wanapoamua kuasi.

Pole sana Dr wa kanisa Catholics Slaa. Sababu Doctorate yako Duniani haitambuliki zaidi ya kanisa Catholics

Oh! Hivi mseminarist akisoma UDSM unapitwa na wengine na huenda anakuwa wa mwisho kabisa? Inawezekana, maana sifa za kujikombakomba kwa lecturers unakuta mseminari hana na hivyo hali hiyo inaweza kumponza.

Lakini kusema wanapitishwa shule za St... St... tu siyo kweli. Mbona wengi tu wanasoma secular universities na wanafaulu vizuri au hawa wanatoka wapi? Si wengine wanafundisha hapo UDSM mbona hawajafukuzwa kwa kukosa elimu inayoendana na ubora wa UDSM?

Hata mimi ningesoma UDSM nige'fail' maana baadhi ya papers za wengine tunaziona humu mitaani zikifanywa na watu wengine kwa malipo. Si umesikia pia yaliyotokes Open University kuwa baadhi ya wanafunzi wenye maksi za chini walikuwa wanabadilirishiwa na walimu wao ili wapate 'flying colours'.

Hawa walikuwa waseminarists? Pole sana. Argument zako ni weak! Inawezekana baadhi ya wanaosoma seminari ni 'weak students' lakini hii siyo sawa na kusema ukisoma seminari utakuwa 'weaker' kwenye secular universities!

Lete evidence: toa mifano ya waseminarist 3 na mimi nitakuletea 12.
 
Kama angekuwa Smart enough basi angejiunga japo na UDSM akakumbane na vichwa pale. Yeye kapita kwenye St colleges ndio maana kapita hiyo PhD.

Mimi nakubaliana kabisa na wengi Huyu ni Sawa tu na Dr Remmy Ongala, Au Dr Cheni.

Wasiwasi wangu Kwa hii CV yake na degree za ujanja ujanja atafaa kuwa Rais wa nchi.

Kuna vichwa gani hapo UDSM? wamegundua nini? what have they invented? what have they contributed towards technology in this world? wachana na hizi faculty za blah blah I mean contribution kwenye fani za engineering, computer science, medicine etc where results are tangible. What I see is academic prestige lakini hakuna vichwa pale.
 
Wengi wa wachangiaji katika mada hii wamejikuta wanadondokea katika ushabiki ima wa Chadema au Ukatoliki katika kutetea.

Tunaona kuwa Ilmu yake ni ile inayotambulika zaidi Kikatoliki na wala si vinginevyo. mazingira aliyokulia na kusomea ni yale ya Kikatoliki zaidi na hata PhD yake ni ile ya kuungaunga kiujanja ujanja kwa mfumo wa katoliki na wala si kwa mifumo tulio zoea,

Jambo kubwa mbele yetu ni kujiuliza kuwa SLAA ANATOSHA KUONGOZA NCHI.

Mkiweka mbele maslahi ya Taifa.

Utaona amepata ubunge wa karatu sababu yeye amekaa pale muda mrefu kama kiongozi wa Kiroho na kwa kupitia kanisa katoliki ameeza kujijenga sana katika kutoa misaada.

Ukisoma vizuri CV yake unaona wazi yeye amesomea na kupikwa na amelelewa katika mfumo wa Kikatoliki zaidi kama mtumishi kuhudumia wakatoliki.

Sasa najiuliza

1.mtu huyu ata prove vipi kwa jamii kuwa yeye anaweza kuongoza jamii yenye mchanganyiko wa Imani. Mind you ndani kuna mahasimu wakubwa wa catholics Duniani yaaani waislam.bila upendeleo

2.Je hataigeuza Tz kuwa nchi ya Kikatoliki.


3.ana mtaji gani kisiasa kuwa eleza waTz wamchague.

Hayo maswali yako si mwuulize Mu-Islaam mwenzio ZITTO KABWE??

Mwisho ni kwamba mwaka 2005 tuliahidiwa vitu kibao na sasa nini kinaendelea?

Hatutaki tena AHADI HEWA. Kiongozi atachunguzwa kwa HISTORIA yake na si AHADI zake feki.

Na hii haijali awe na dini gani au mtu wa rangi gani? Kabila gani? Mkoa gani? Maumbile yake nk.
 
Hayo maswali yako si mwuulize Mu-Islaam mwenzio ZITTO KABWE??

Mwisho ni kwamba mwaka 2005 tuliahidiwa vitu kibao na sasa nini kinaendelea?

Hatutaki tena AHADI HEWA. Kiongozi atachunguzwa kwa HISTORIA yake na si AHADI zake feki.

Na hii haijali awe na dini gani au mtu wa rangi gani? Kabila gani? Mkoa gani? Maumbile yake nk.

Mkuu mbona siku hizi post zako zimekua za udini sana? maana kila kona naona ni wewe na Tumaini mnaandamana.
 
sio lazima ufanye masters.
ukipata degree unaweza kuunganisha moja kwa moja kwenda kwenye PHD, ila kuna somo linalohusiana na kufanya research inabidi ufanye.


To make things clear, nenda kapekue CV ya Prof Mark Mwandosya uone kama kuna mahali alisoma Masters
 
Ukipata first class au upper second degree,unaweza kwenda kufanya Phd moja kwa moja bila masters.Most masters in conversion.Mtu unaweza kusoma sociology Undergraduate,then ukasoma Msc say in finance,then Phd finance.
I assume Mwandosya alifanya vizuri kwenye Bsc.Ila napinga mpaka sasa ajiite Proffesor wakati ni full time politician.anyway hii ni Bongo
 
Hii inakuweje wadau??? Prof. Mwandosya naambiwa ni kichwa sana, ilikuwaje akaruka Masters degree???

Napenda kuchangia kwenye hili kwa kusema kuwa... ni ufinyu wa mawazo kufikiri ati mtu kupata PHd lazima afanye Masters.Tukiacha hii ya Dr Slaa, FYI kuna watu wako very bright kiasi inakuwa ni kupoteza muda kupambana na masters hivyo hushauriwa ku enroll moja kwa moja kwenye PhD na ni chuo hushauri.Unaweza kuuliza recipients wa Commonwhealth Bright Students Scholarships Programme watakujuza kuwa wametoa sponsoships kwa watu wa namna hiyo mmoja wapo ni ndugu yangu wa damu. Hana Masters lakini alichukuliwa moja kwa moja kujiunga na PhD japo yeye alitaka Masters.
 
Mkuu mbona siku hizi post zako zimekua za udini sana? maana kila kona naona ni wewe na Tumaini mnaandamana.

Nafikiri umegundua kuwa NAMWANDAMA Tumaini na Barubaru.

Hawa wanaacha thread za DINI na kuleta DINI zao kwenye thread za SIASA.

Sasa nitakula nao sambamba hadi KIELEWEKE.

Nikiingia JF tu, natafuta POST zao na kuanza kazi...... teeteeeeee....

Wakiacha na kuhamia kwenye DINI, huko zowafuati maana huwa siingii kabisa. Huko acha watukanane na MaxShimba. Huko ni eneo lao la kujidai na ukiingia huko umeyataka mwenyewe. Sasa hawa jamaa wameshindwa vita na MaxShimba na wameamua wahamie huku.

Nashangaa kwa nini Mods wasiwafungie kwa kubadili mijadala yote iwe ya kidini. Kama huamini basi hebu angalia POST zao zote.

Sasa ntawasaidia kila mjadala wanaochangia kuubadili uwe wa dini ili waone KARAHA wanayoifanya.
 
Ukipata first class au upper second degree,unaweza kwenda kufanya Phd moja kwa moja bila masters.Most masters in conversion.Mtu unaweza kusoma sociology Undergraduate,then ukasoma Msc say in finance,then Phd finance.
I assume Mwandosya alifanya vizuri kwenye Bsc. Ila napinga mpaka sasa ajiite Proffesor wakati ni full time politician.anyway hii ni Bongo

Mkuu,
Maneno mazito sana hayo juu.

Mtu ni Mwanasiasa wa miaka kibao na hafundishi wala kufanya kazi za kitafiti zozote na bado anajiita Dr.
Dr. Mwakyembe, Dr. Nagu, Prof. Mwandosya, Prof.......

Huu ni UPUUZI na kutumia hizo TITTLE vibaya. Wao na Dr. Remmy hawana tofauti kabisa. Na wengi ni Wasomi wanaotakiwa kufahamu kuwa haya ni MAKOSA.

Bahati mbaya hili hata Slaa anafanya.

Please Slaa, kama umeacha kazi za kufundisha na sasa umekuwa Mwanasiasa, inabidi hiyo TITTLE uitundike ukutani.
 
Mkuu,
Maneno mazito sana hayo juu.

Mtu ni Mwanasiasa wa miaka kibao na hafundishi wala kufanya kazi za kitafiti zozote na bado anajiita Dr.
Dr. Mwakyembe, Dr. Nagu, Prof. Mwandosya, Prof.......

Huu ni UPUUZI na kutumia hizo TITTLE vibaya. Wao na Dr. Remmy hawana tofauti kabisa. Na wengi ni Wasomi wanaotakiwa kufahamu kuwa haya ni MAKOSA.

Bahati mbaya hili hata Slaa anafanya.

Please Slaa, kama umeacha kazi za kufundisha na sasa umekuwa Mwanasiasa, inabidi hiyo TITTLE uitundike ukutani.

I beg to differ on this one.

MTU ANA UAMUZI KUTUMIA AU ASITUMIE.

These people earned their titles..hivyo ni haki yao kutumia Dr.

UKIWA NA MAWAZO HAYA, UTASEMAJE KWA AKINA DR KIKWETE, DR ANNA MKAPA, DR MALECELA - Hawa ni honorary yet they have a right to use the titles?

FYI hizi titles za Phd NI BOngo tu watu wanapapatika sana kuzitumia.... wenzetu nchi nyingine wala siyo deal...if anything mtu anaweka jina lake na mwisho anamaliza ( PhD)..MFANO VERA.....( PhD)

Tz TUNAANZA KUWA KAMA WANIGERIA...Kama wewe siyo Dr, basi ni Sheikh, Al Haj, Chief, Bishop... na siyo kubaki tu Mr, Mrs, Miss, Ms.
 
VeraCity,

Hakuna anayesema ni MAKOSA ya kufungwa mtu.

Ila kama kweli ULISOMEA hii kitu na wewe ni MSOMI ULIYEELIMIKA, utagundua kuwa kama umeacha kufundisha, hii tittle hutakiwi kuitumia.

Sasa unasema wewe ni Prof. na unaulizwa unafundisha wapi unasema ahh sasa hivi mie ni Waziri. Mbona akina Angela Merkel hawajiiti ma Dr na akina Obama hawajiiti Maprofesa?

Ni uamuzi wa mtu. Kama mtu ameelimika atagundua na kuliondoa hilo tatizo. Kama hataki wala hakijaharibika kitu ila kwa wataalamu wa mambo tunakuwa tunaona kama vile kavaa suti na koti la suti KACHOMEKEA.
 
I beg to differ on this one.
MTU ANA UAMUZI KUTUMIA AU ASITUMIE.
These people earned their titles..hivyo ni haki yao kutumia Dr.
UKIWA NA MAWAZO HAYA, UTASEMAJE KWA AKINA DR KIKWETE, DR ANNA MKAPA, DR MALECELA - Hawa ni honorary yet they have a right to use the titles?
FYI hizi titles za Phd NI BOngo tu watu wanapapatika sana kuzitumia.... wenzetu nchi nyingine wala siyo deal...if anything mtu anaweka jina lake na mwisho anamaliza ( PhD)..MFANO VERA.....( PhD)
Tz TUNAANZA KUWA KAMA WANIGERIA...Kama wewe siyo Dr, basi ni Sheikh, Al Haj, Chief, Bishop... na siyo kubaki tu Mr, Mrs, Miss, Ms.

Kwa kuongeza tu: PhD ni shahada wakati Professor (ship) ni academic rank. Kwa hiyo mtu anaweza kutambulishwa hivi "Dr. Es Em Yu - Professor of Mathematics". Kama mtu hafundishi pengine kuna sababu ya kuhoji uhalali wa kuendelea kujiita Professor. Labda pengine wajiite Retired Professor (Rtd Prof.) kama vile wanajeshi wanavyofanya ikiwa wameshastaafu jeshi.
 
wengi humu ndan hamjui uzito a masomo ya falsafa na theolojia ndio maana mnang'aka bure. someni acheni kubishi kipuuuzi, magobe T heu wasaidie hawa wajue hivi vitu.
 
Labda wenzangu mnifafanulie kidogo kwa mtazamo wenu.

1. Dr W Slaa anafaa kuitwa Doctor.
wapi kafanya Post Graduate, Masters?

2. najua bila kuna wengi sana humu wa CHADEMA labda wamfikishie ujumbe huu kuwa Utafiti wake katika PhD alifanya khusu nini?

3.mnazionaje hizi degree za st.st.st?

Kwani PhD holder anaitwaje?na kwani wewe ukipata PhD au Degree pale St.Augustine utataka tukuiteje??mambo ya thesis yake sisi yanatuhusu nini??.... Mbona Profesa maji marefu hamumuulizi thesis yake?
 
Ndugu yangu tatizo hapa sio masters, watu wengi wana phd hawana masters kama ulifanya nice publications kwenye strong journals then ukaweza ku upgrade ukapata phd, tatizo hapa zitazame hizo miaka vizuri, eti Slaa anafanya phd kabla hata ya advance diploma huku akiwa na certificate fulani tu hapo.
Pia wadau mmeweka ana PhD tupeni publications zake basi na mtupe ni journals gani amepublish?

Kwa nini usitafute mwenyewe mpaka uatafutiwe. Uvivu wa namna hii ndio unaoturudisha nyuma.
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom