Profesa Sospiter Muhongo

Labda unabahati mbaya me nilifuatilia wiki2 ya tatu umeme ukawaka kwangu,kwa hiyo usipende kuhitimisha vitu bila kufanya tafiti za kutosha.
 
Inabidi ukaulizie ngazi ya juu zaidi kama hapo wanakuhangaisha pengine wataka BAKSHISH! jaribu kuongea na wakubwa kidogo hapo ujue tatizo nini kama hawaeleweki unawawekea mtego unaongea na PCCB wanakuja kuchukua watu wao tumeshachoka sasa kama noma na iwe noma maana bongo rushwa ni kama imekuwa jadi!!!
 
Toa kitu kidogo mkuu,bila hivyo utasubiri sana si unajua nchi yetu
 
Mambo hayaendi kama wewe unavyotaka. Serikali inafata ratiba.
 
Nimeshafika ngazi ya wilaya wakanirudisha kule kule...
Inabidi ukaulizie ngazi ya juu zaidi kama hapo wanakuhangaisha pengine wataka BAKSHISH! jaribu kuongea na wakubwa kidogo hapo ujue tatizo nini kama hawaeleweki unawawekea mtego unaongea na PCCB wanakuja kuchukua watu wao tumeshachoka sasa kama noma na iwe noma maana bongo rushwa ni kama imekuwa jadi!!!
 
Huyo profesa niliwahi kumsikia akihojiwa Radio Tanzania wakati ule kabla hajawa mwanasiasa, akasema eti madini yaliyopo tanzania hayawezi kubadili hali ya maisha ya wanainji. Alivyoteuliwa kuwa waziri wala sikutarajia mapya. By the way, wataraji vipi jipya toka kwa waziri wa serikali ya chama chetu kinachoongozwa na Jakaya Mrisho Kikwete?
Mmoja wa mawaziri wataalam waliobobea kwenye masuala ya nishati na gas. Wakati anateuliwa na Raisi nilifurahi sana kwani alianza kutoa ahadi za wananchi kufungiwa umeme kwa muda wa mwezi mmoja kama umelipa. Nilijitahidi sana kutafuta hela ili nikaunganishiwe kwenye kibanda changu kilichoko eneo la usariver maeneo ya ngaresero nilijitahidi kukamilisha taratibu zote.

Hatimae zilikamilika januari 2013 chakushangaza mpaka leo hakuna kitu! Wananchi wa eneo lile tulijitahidi ili tujiunge wa 3 ili tupatiwe nguzo 1 tu ili iweze kutufikia wote lakini wapi! Kila ukienda ofisi ya Tanesko iliyoko maeneo ya usariver majibu ni kwamba subirini mpaka tumalize vijijini! Hivi hii ni haki kweli? Tangu january mpaka leo! Huu si ungwana hata kidogo.

SAME TIMES TUNAWASHUTUMU MAWAZIRI KUMBE HUKU CHINI WATENDAJI NI BOOM..

Waziri ebu fanya kazi
 
Muhongo ni mtaalamu wa dharau na majigambo. Maneno mengi bila utekelezaji....huyu jamaa ni mropokaji sana. Pengine siku hiyo alikuwa naropoka !
 
Ndugu yangu muathirika mwezangu, maneno ya Prof MUHONGO ilikuwa siasa tupu. Sisi tupo KWAMUROMBOO Arusha, kata inayoongozwa na maCCM tukapambana tukimshirikisha DIWANI. Tukidhani watajiosha. Diwani alipoona ngoma nzito akamualika meneja mkoa aje ajibu kero zetu. Tulichoambulia nikukatishwa tamaa jumla, na kwamaelezo yake yule Meneja hakuuma maneno. Namnukuu: ' Ndugu zangu tunauhaba mkubwa wa nguzo kwenye shirika iliyotokana na kushushwa kwa gharama za kuunganisha umeme. Kwa mkoa wetu tu tunahitaji nguzo 20,000. Na waliokwisha lipia tunadaiwa nguzo 2000 hadi Januari 2013. Lakini hadi leo tar 25/5/2013 tumeletewa nguzo 300 tu! Sasa mtaona ni jinsi gani tunapungukiwa, tunaowaomba tu kuweni na subira' Mwenye akili fanya tafakari.
 
Back
Top Bottom