Profesa Muhongo awapa somo wabunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Profesa Muhongo awapa somo wabunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 14, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]ALHAMISI, JUNI 14, 2012 06:19 NA BAKARI KIMWANGA, DODOMA  WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, aligeuka kivutio mbele ya Bunge, baada ya kutoa somo kuhusu umuhimu kwa taifa kutumia madini ya Uranium.


  Profesa Muhongo, alilazimika kusimama baada ya swali la nyongeza na la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), ambaye alitaka maelezo ya Serikali kuhusu hatari ya madini ya Uranium, ambapo alipinga matumizi yake kutoharakishwa kwa hofu ya kutokea maafa kama ilivyotokea nchini Japan.


  Waziri huyo, ambaye kitaaluma ni mwanasayansi, alisema jambo hilo halina ukweli, kwani hivi sasa mataifa yote yaliyoendelea yapo katika matumizi ya madini hayo.


  “Si kweli eti Japan ni taifa la kwanza kutumia madini ya Uranium, bali nchi ya kwanza ni Kazakhstan, ambayo hivi sasa imekuwa na maendeleo makubwa,


  “Na ushahidi wa hili, Mheshimiwa Naibu Spika, nimefanya utafiti mbalimbali, lakini hakuna athari kama ambayo imekuwa ikitolewa na baadhi ya watu ambao hawajui, hivi sasa hata nchi jirani ya Malawi, wanatumia madini haya na mgodi wao upo katika eneo la Karonga.


  “Kinachotakiwa ni utashi na maslahi ya taifa, leo mataifa yote kama Ufaransa, Marekani na Canada, umeme wao wanazalishwa na madini haya ya Uranium, kwa nini sisi Tanzania.”


  Katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalum, Getruda Lwakatare (CCM), alitaka kujua tahadhari iliyochukuliwa na Serikali kwa wananchi kuhusu madini hayo.


  Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, alisema hivi sasa Serikali bado haijafikia katika hatua ya uchimbaji wa madini yao

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Japan tatizo lilitokea sababu ya tetemeko la Ardhi na Hurricane... Japan wana karibia Nuclear Power Plant 12 ni Umeme Rahisi kweli na haukatiki katiki; Viwanda Vyetu Vitakuwa haswa.

  USA wana URANIUM Power Plant lakini hawajengi tena wana maintain walivyonavyo wana kama 20 inasaidia Miji Mikubwa kama NY, LOS ANGELES.

  Sisi hatuta hitaji nyingi MOJA tu basi na itatumalizia Matatizo yoote na tutaitunza na kuhakikisha hakuna matatizo hatuna Matetemeko ya Ardhi Makubwa; na Hurricane's kama Japan... na hatutaweka baharini kama za Japan.

  Ndio tunahitaji angalau Moja...
   
 3. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Mbona naona kama hakujibu swali, ameanza siasa tayari eti enh?
   
Loading...