mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,410
- 4,988
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo amebainisha kuwa Serikali ya awamu ya sita na Chama Cha Mapinduzi Kinathamini uwepo wa Vyombo vya habari imara, katika kukuza uwajibikaji na kuimarisha utawala bora nchini.
Akizungumza na wahariri wa Vyombo vya Habari na wanahabari leo Julai 08, 2025 Mjini Dar Es Salaam kuelezea kuhusu kutamatika kwa mchakato wa uandaaji wa Dira 2050, Prof. Kitila amebainisha kwamba tayari Serikali pia imeanza mchakato wa kuona namna ya kufadhili ruzuku kwa Vyombo vya habari nchini kwa kutumia Kodi za wananchi kama sehemu ya kuviimarisha katika utendajikazi wake.
"Mtu ambaye anadharau Vyombo vya habari ni mtu mpumbavu sana. Vyombo vya habari ni sehemu ya jambo muhimu kwenye jamii yoyote iliyoelimika kwahiyo tuzungumze kuziimarisha kama zipo dhaifu lakini huwezi kudharau media." Amesema Prof. Kitila.
Akisisitiza umuhimu wa Vyombo vya habari kuwa wakweli na kutosita kufanya kazi yake kwa kuzingatia misingi ya taaluma yao bila upendeleo, Kitila amebainisha kuwa Vyombo vya habari kupata ruzuku hiyo haitakuwa sehemu ya kutengeneza upendeleo, akitaka Vyombo vya habari kuwa wakweli bila kuchagua upande ili kuisaidia serikali katika kukuza uwajibikaji na utawala bora serikalini.