Profesa Mchome afutwe kazi

Profesa Mchome afutwe kazi

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
25,867
Reaction score
25,193
Wiki iliyopita Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, profesa Sifuni Mchome, aliweka hadharani muundo mpya wa upangaji wa madaraja ambapo alitangaza kufuta daraja la sifuri na kuanzisha daraja la tano.

Baadaye aliibuka Naibu Waziri wa Elimu,Philip Mulugo na kumkana Prof Mchome--kwamba ni muongo--hayo madaraja amejitungia mwenyewe akiwa na mkewe nyumbani kwake, kwa hiyo hakuna kitu kama hicho kilichotangazwa na Profesa!

Mh. William Lukuvi alimtetea vikali sana Mulugo (Serikali) kwamba yuko sahihi na kuonya kuwa Prof Mchome (Raia) ni muongo mkubwa! Lukuvi aliwataka wananchi wamuamini Mulugo kwa kuwa yeye ni Serikali tofauti na Prof Mchome ambaye ni raia wa kawaida. Hii inaleta picha kwamba madaraja mapya yaliyotangazwa na Prof Mchome ni mawazo yake binafsi na hayajawahi kujadiliwa na mtu yeyote ndani ya Wizara ya Elimu.

Kufuatia sintofahamu na kizungumkuti hiki, Profesa Mchome anapaswa kuachia ngazi kwa kulitangazia Taifa uongo kwa sababu anazozijua yeye. Yaani Profesa huyu aketi nyumbani na mkewe waamue kutunga madaraja mapya ya ufaulu na kuutangazia umma wa watanzania kinyume cha sheria halafu aachwe aendelee kuongoza wizara hii nyeti? Haiwezekani hata kidogo-- anapaswa kuachia ngazi mara moja.

Hatuwezi kukubali kuona Wizara ya Elimu ikiongozwa na profesa uchwara kama huyu Mchome.
 
Mimi sitaki kuamini kwamba Mchome alitudanganya, najua hili lilijadiliwa na ushahidi upo wakati hizi tafiti zikifanyika. Mulungo alikuja na hoja ya kupiga siku moja baadae kwani alishapata picha halisi ya mwitikio wa watu yaani jamii.

Ninavyoamini mimi ni kwamba Mulungo kwa makusudi kabisa inawezekana waliketi na baraza la mawaziri, wakajadili hili over the night kesho yake akaenda kulisema bungeni akijua kwamba mabadiliko haya hayatamhusu katibu mkuu.

Note Prof Mchome ni mtaalam wa elimu wala hana longolongo hizi ambazo huyu mzee wa div 4 analeta.
Ushauri wangu serikali ijipange upya imekurupuka.
 
Waswahili walisema"ndege wa rangi moja huruka pamoja" le profeseri atachagua kundi lake
 
Kwa hilo tusi kuendelea kukalia hcho kiti le profeseri anajidhalilisha...siasa zikiingia mahali lazima panuke.
 
Mkuu TARIMO WA ROMBO ndo wewe uliyemaliza pale SUA mwaka jana course ya FOREST?
 
Kuna viongozi wanapenda kuwafanya wenzao chambo na baadae kupima upepo wa mwitikio wa wananchi.
Haiwezekani katibu mkuu akatangaza maamuzi mazito kama haya bila waziri husika asifahamu. Hapa tunadanganyana tu.

Hii ni kukosa umakini katika kufanya maamuzi yenye madhara hata kwa vizazi vijavyo.

SHAME ON THEM
 
Wiki iliyopita Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, profesa Sifuni Mchome, aliweka hadharani muundo mpya wa upangaji wa madaraja ambapo alitangaza kufuta daraja la sifuri na kuanzisha daraja la tano.

Baadaye aliibuka Naibu Waziri wa Elimu,Philip Mulugo na kumkana Prof Mchome--kwamba ni muongo--hayo madaraja amejitungia mwenyewe akiwa na mkewe nyumbani kwake, kwa hiyo hakuna kitu kama hicho kilichotangazwa na Profesa!

Mh. William Lukuvi alimtetea vikali sana Mulugo (Serikali) kwamba yuko sahihi na kuonya kuwa Prof Mchome (Raia) ni muongo mkubwa! Lukuvi aliwataka wananchi wamuamini Mulugo kwa kuwa yeye ni Serikali tofauti na Prof Mchome ambaye ni raia wa kawaida. Hii inaleta picha kwamba madaraja mapya yaliyotangazwa na Prof Mchome ni mawazo yake binafsi na hayajawahi kujadiliwa na mtu yeyote ndani ya Wizara ya Elimu.

Kufuatia sintofahamu na kizungumkuti hiki, Profesa Mchome anapaswa kuachia ngazi kwa kulitangazia Taifa uongo kwa sababu anazozijua yeye. Yaani Profesa huyu aketi nyumbani na mkewe waamue kutunga madaraja mapya ya ufaulu na kuutangazia umma wa watanzania kinyume cha sheria halafu aachwe aendelee kuongoza wizara hii nyeti? Haiwezekani hata kidogo-- anapaswa kuachia ngazi mara moja.

Hatuwezi kukubali kuona Wizara ya Elimu ikiongozwa na profesa uchwara kama huyu Mchome.

Ebwana we, cha uongo, yaani uprofesa wa uongo aliupata kwenye chuo kikuu cha masisiemu waongo, serikali yote ya waongo? Pinda mwongo.

Ajabu na kwali
 
Wiki iliyopita Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, profesa Sifuni Mchome, aliweka hadharani muundo mpya wa upangaji wa madaraja ambapo alitangaza kufuta daraja la sifuri na kuanzisha daraja la tano.

Hatuwezi kukubali kuona Wizara ya Elimu ikiongozwa na profesa uchwara kama huyu Mchome.
Kwa serikali hii ya ccm usitegemee kitu kama hicho hii ni serikali kipofu, mambo kama hayo ya kufutwa kazi kwa mtu anayeboronga kazi au kuwajibiga utayaona kuanzia 2015 baada ya chadema kuongoza nchi. hapo ndipo patakuwa na kilio na kusaga meno
 
Kilichofanyika hapo ni Mulugo na Lukuvi kutaka 'kuokoa' jahazi baada ya kuona reaction ya watu kutokana na mfumo mpya uliotangazwa na katibu mkuu mchome.

Itakumbukwa kuwa mchome ndiye aliyeongoza tume ya iliyooundwa na waziri mkuu kuchunguza chanzo cha wanafunzi kutokufanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne mwaka jana. Hata hivyo, ripoti ya tume hiyo haijawahi kutolewa hadharani, bali serikali imekuwa ikitumia baadhi ya vipengele vya ripoti hiyo kufanya maamuzi kama vile ilivyoamua kufuta matokeo ya kidato cha nne 2012 na kuagiza necta ipange upya. Itakumbukwa pia kuwa mmoja wa wajumbe wa tume hiyo aliamua kujiudhuru akilalamikia 'uchakachuaji' uliofanywa kwenye ripoti hasa baada ya kuona yanayotekelezwa si yale waliyokubaliana kwenye tume.

Cha kushangaza zaidi, ni pale mwenyekiti wa tume alipoteuliwa kuwa katibu mkuu wa wizara ili atekeleze yale aliyoyachunguza mwenyewe, au yale 'waliyochakachua'. Na sasa tumeona alivyoanza utelezaji rasmi ya ripoti yake. Kwa kifupi, mchome alitumiwa na wanasiasa na yeye akakubali kuuza 'weledi' wake kwa matakwa ya wanasiasa na kukubali kuficha ukweli. Hata hivyo alisahau kuwa, wanasiasa ni wanasiasa na sio wa kuamini muda wote maana hubadilika kulingana na upepo. Na siku sio nyingi tangu akibali kutumikia matakwa ya wanasiasa, tayari ukweli huu umeanza kudhihirika, kwa Lukuvi kumkana kuwa kauli yake sio kauli ya serikali, bali kauli ya Mulugo ndio kauli ya serikali.

Nilichojifunza, na ninachoendelea kujifunza ni kwa wasomi na watalaam mbalimbali kuwa waangalifu sana wanapodeal na wanasiasa. Wanasiasa wengi ni vigeugeu, hawaaaminiki na wanaweza kukuacha katika hali ya sintonfahamu baada tu ya kufanikisha malengo yao. Katika hili, Lukuvi na Mulugo ni washindi, lakini ni aibu kubwa kwa profesa msomi wa sheria!

Wiki iliyopita Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, profesa Sifuni Mchome, aliweka hadharani muundo mpya wa upangaji wa madaraja ambapo alitangaza kufuta daraja la sifuri na kuanzisha daraja la tano.

Baadaye aliibuka Naibu Waziri wa Elimu,Philip Mulugo na kumkana Prof Mchome--kwamba ni muongo--hayo madaraja amejitungia mwenyewe akiwa na mkewe nyumbani kwake, kwa hiyo hakuna kitu kama hicho kilichotangazwa na Profesa!

Mh. William Lukuvi alimtetea vikali sana Mulugo (Serikali) kwamba yuko sahihi na kuonya kuwa Prof Mchome (Raia) ni muongo mkubwa! Lukuvi aliwataka wananchi wamuamini Mulugo kwa kuwa yeye ni Serikali tofauti na Prof Mchome ambaye ni raia wa kawaida. Hii inaleta picha kwamba madaraja mapya yaliyotangazwa na Prof Mchome ni mawazo yake binafsi na hayajawahi kujadiliwa na mtu yeyote ndani ya Wizara ya Elimu.

Kufuatia sintofahamu na kizungumkuti hiki, Profesa Mchome anapaswa kuachia ngazi kwa kulitangazia Taifa uongo kwa sababu anazozijua yeye. Yaani Profesa huyu aketi nyumbani na mkewe waamue kutunga madaraja mapya ya ufaulu na kuutangazia umma wa watanzania kinyume cha sheria halafu aachwe aendelee kuongoza wizara hii nyeti? Haiwezekani hata kidogo-- anapaswa kuachia ngazi mara moja.

Hatuwezi kukubali kuona Wizara ya Elimu ikiongozwa na profesa uchwara kama huyu Mchome.
 
Hili game litawaumiza zaidi watanzania. Serikali na wizara wakajipange upya waje ni critical analysis.
 
Last edited by a moderator:

mkuu mimi sioni mahali ambapo Lukuvi na Mlugo wameshinda badala yake naona utendaji mbovu usokuwa na tija na tena hauleti maana katika jamii.

ujue tiba ya tatizo sio kulikimbia bali ni kulitatua, Lukuvi na Mlugo walipoona reputation ya wananchi walipaswa kufikiri ni jinsi gani watatue tatizo hilo. Hkukuwa na haja ya kuongopa, wala kuongopa hakujaweza kutatua taizo lililopo bado.

Wenye akili zao wanawaona huyu mlugo wa div 4 ni tatizo na Lukuvi wake ni waoga hasa kwenye mambo ya msingi? Prof alitumia busara sana kusema kweli ya kile ambacho wao waliamua kama tume na kwa ujasiri alisema najua alikuwa nae pia anasubiri comment za wananchi.

Mlugo na Lukuvi kwa woga wakajadiliana na kuja na majibu over the night hii ni aibu kabisa kabisa. tena ningekuwa mimi rais ningewafukuza kazi kwa kuamua maamuzi ambayo ni tata.

watu wengine wanaokosea ni sisi wananchi manake tumekuwa kama gari bovu kwamba tukipelekwa huku tunakwenda tukipelwaka kaule tunakwenda. Imagine hili linakuja kuwaathiri watoto wetu ambao ndio tunategemea waje wajenge taifa hili sasa leo unaambiwa vitu havieleweki halafu tumekaa kimya tu kama mambumbu sasa hapa mjinga ni nani??

tutoke tujipange kwaajili ya elimu ya watoto wetu, kila mmoja aandike iwe ni makala iwe ni barua aipeleke na tu rise aour voices against this. Tukikumbuka Mungai alivyotufanyia 8 yrs ago matokeo yake ndo haya, like wise yale ya Kapuya sasa tutaendela kuvumilia haya hadi lini??

C'MON lets rise our voices tusikike tumechoka kabisa maisha ya elimu kufanywa kama nguo ya mtumba. Bad enough mwanao akiwa best student bado ni best katikati ya vilaza, na kwenye ulimwengu huko bado Tanzania tunakuwa ranked kama nchi ya kwanza yenye alama ndogo sana za ufaulu duniani. tujifikirie in this angle na sio kufanya blah blah.
 
Wiki iliyopita Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, profesa Sifuni Mchome, aliweka hadharani muundo mpya wa upangaji wa madaraja ambapo alitangaza kufuta daraja la sifuri na kuanzisha daraja la tano.

Baadaye aliibuka Naibu Waziri wa Elimu,Philip Mulugo na kumkana Prof Mchome--kwamba ni muongo--hayo madaraja amejitungia mwenyewe akiwa na mkewe nyumbani kwake, kwa hiyo hakuna kitu kama hicho kilichotangazwa na Profesa!

Mh. William Lukuvi alimtetea vikali sana Mulugo (Serikali) kwamba yuko sahihi na kuonya kuwa Prof Mchome (Raia) ni muongo mkubwa! Lukuvi aliwataka wananchi wamuamini Mulugo kwa kuwa yeye ni Serikali tofauti na Prof Mchome ambaye ni raia wa kawaida. Hii inaleta picha kwamba madaraja mapya yaliyotangazwa na Prof Mchome ni mawazo yake binafsi na hayajawahi kujadiliwa na mtu yeyote ndani ya Wizara ya Elimu.

Kufuatia sintofahamu na kizungumkuti hiki, Profesa Mchome anapaswa kuachia ngazi kwa kulitangazia Taifa uongo kwa sababu anazozijua yeye. Yaani Profesa huyu aketi nyumbani na mkewe waamue kutunga madaraja mapya ya ufaulu na kuutangazia umma wa watanzania kinyume cha sheria halafu aachwe aendelee kuongoza wizara hii nyeti? Haiwezekani hata kidogo-- anapaswa kuachia ngazi mara moja.

Hatuwezi kukubali kuona Wizara ya Elimu ikiongozwa na profesa uchwara kama huyu Mchome.

hapo anayepaswakuachia ngazi ni mulugo. Lukuvi alichokifanya ni kutokumtia aibu naibu waziri. Do yo think katibu ana mamlaka ya kutangaza kitu ambacho wakubwa zake hawajui? Waulize mahead masters walipewa madodoso ya mchakato.
Katibu yupo sahihi kabisa kwa mpangilio aioutoa.
 
ivi shukuru kawambwa aliokotwa wapi? mbeleko mpaka inachanika!!! alikua miundombinu kwa vile ile ni wizara nyeti ubovu unaonekana na uchumi unaathirika wakaamua wamtoe wamemleta elimu wa kizan kua huku ndio majuha kama yeye ataweza result ndio izi.... mkuu si lazima umchukue wa homeboy unaharibu nchi!!!
 
Back
Top Bottom