Profesa Mchome afutwe kazi

Profesa Mchome afutwe kazi

Sijajua hii wizara ya Elimu ilipata wapi ujasiri wa kutangaza huu UOZO.Inasikitisha sana!
 
Sijajua hii wizara ya Elimu ilipata wapi ujasiri wa kutangaza huu UOZO.Inasikitisha sana!
Mkuu ujasiri huo wanaupata toka kwa Kamishna wa Elimu Prof Bhalalusesa. Huyo ndiyo kimara wa sera za kupanua mogoli badala ya kuboresha elimu. Alipoingia wizara ya elimu tu kazi ya kwanza ilikuwa ni kushauri wanaojiunga na kidato cha kwanza alama zao zishushwe toka 40% hadi 28%. Sasa hapa anajihami anapanua magoli ya Kidato cha Nne ili udhaifu wa maamuzi yake usije kuonekana hao vijana watakapomaliza kidato cha nne.

Fikiria Prof Bhalalusesa Kwenye huo UOZO uliotangazwa wameweka utaratibu eti mwanafunzi akifanya QT alama zake ndiyo ziitwe Continuous assessment kwa masomo yote atakayofanya Kidato cha Nne kama mtahiniwa wa Kujitegemea. Eti unazi copy alama za QT na ku-paste kwa kila somo. Kwa hiyo waziri na Katibu Mkuu watapata UOZO mwingi sana maana hao yote yanaokana na ushauri wa Kamishna Prof Bhalalusesa mtaaluma Mkuu wa elimu nchini.
 
Hata ingekuwa wewe huwezi kuachia ngazi maana kila mtu sasa anapenda pesa na maisha mazuri na kingine serikali yetu ni ya usanii maana haioni aibu hata kukana maamuzi yake yenyewe! Hivi unadhani jamaa ni mjinga kiasi hicho hapo walipokuwa wanajibu ni sehemu ya siasa ila ukweli serikali inao maana hii ingepita wangemsifu sana kwa ubunifu wa kuiokoa serikali ya chama tawala dhidi ya maafa ya wanaofeli kila mwaka.

Kwa vile wawakilishi wa wananchi wamejitahidi kuona kwa kiasi chao basi serikali inasema ni uongo kwa hiyo yenyewe inafanyia kazi taarifa za mfanyakazi moja kwa moja! Je baraza la mawaziri halikuwa na taarifa hii? Huu ni usanii tu maana hawawezi kumwajibisha kwa vile ukweli wanaujua maana huenda kuna barua ya kuruhusiwa kufanya hivyo na waziri husika!
 
Kuna mtu humu kama tungemuelewa tungemuunga mkono kitaambo , maana alishamkataa huyo jamaa kabla hata hajaanza kazi .
 
kuna mtu humu kama tungemuelewa tungemuunga mkono kitaambo , maana alishamkataa huyo jamaa kabla hata hajaanza kazi .
Kweli Mkuu jamaa alipinga uteuzi wake mapema, na ukiangalia hata mambo yanavyooenda wizarani yaani combination ua Prof Mchome + Prof Bhalalusesajumlisha Kawamwa + Mulugo = JANGA LA ELIMU
 
Screenshot_2023-08-16-23-57-56-1.jpg
 
Back
Top Bottom