TANZIA Profesa James Lwelamira wa Chuo cha Mipango-Dodoma afariki dunia hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma

R.I.P Professor.

Huyu jamaa alikuwa nguli wa Hesabu, ni kichwa hasa.

Natoa tahadhali kwa watumishi wa hicho Chuo maana napitia faili lenye taarifa ya safari yao ya mwezi uliipita.
Wengine wanajiuguza majumbani.
 
Na hii inatokana na research uliyofanya au ? na hata mitaani kuna mtandao ?

Ngoja nikupe research moja ndogo ambayo unaweza ukafanya hata ukiwa kwenye kiti chako.., ulizia mwanasheria yoyote akupe data ya graph ya wenzao kwenye Tasnia (sababu wana database) ni wangapi wameondoka katika hii miaka mitano na hivyo vifo vyote uangalie kama ni average kwa miaka yote hiyo au kwa kipindi hiki imezidi...

Hapo utakuwa umechukua sample kidogo kwa data ambazo zipo available... Hivyo ndivyo wanasayansi au wachunguzi wa mambo wanavyofanya kazi....
Suala la kifo haliangalii, taaluma, jinsia, umri au kada fulani, vifo vinaweza kufululiza kwa watu wa jinsia fulani au taaluma fulani bila kujali Sababu ya kifo, research niliyotumia ni kwa kuangalia mtaani kwetu na mitaa jirani na ktk ukoo na familia rafiki kwa kweli hakuna misiba iliyofululiza au takwimu kupanda kusiko kawaida, ila taarifa za majirani kupata homa za mafua ni nyingi na kwa kweli wengi wanapona tena kwa kutumia dawa ambazo sio sahihi!!!
 
Ni kweli maarufu kwenye kada zao ndio maana wa mtaani hawawekwi ,ingekuwa hadi mtaani wanawekwa ingekuwa balaa.
Hata mtaani takwimu siko kawaida, mie nipo Kahama mtaa wa majengo, kwa kweli sikumbuki Mara ya mwisho lini msiba umetokea hapa mtaani kwetu, labda uje unisaidie kuuliza!
 
Hukubkwetu ilikuwa nadra kuona Costa kutoka huko na mosoba, lkn sasa daily Costa zinaleta misiba mkoani. Kweli dude balaa. Mbaya zaidi linakula watu walio Kitenge naenda majina kwa mida mrefu kama hawa maprof, mask, wanasheria nk. Hatari sana. Wanasanyansi wajitahidi tupate tiba.
 
Hata mtaani takwimu siko kawaida, mie nipo Kahama mtaa wa majengo, kwa kweli sikumbuki Mara ya mwisho lini msiba umetokea hapa mtaani kwetu, labda uje unisaidie kuuliza!

Kwahiyo kama mtaani kwako hakuna misiba ndio mitaa mingine nayo hakuna? Kwakasi hii tuendelee kuchukua tahadhari tu.
 
Nimtazo!msinjenge chuki hi corona inawatafuna watu wazito....mitano tena,bwana Yule Mara pap changamoto za kupumua.....tutapiga fataki na tarumbeta
 
Wasomi wabongo bana sijui bongo zenu zimeingiwa na kamasi la mnyama gani? Yaani hivi vijimafua vimewapanikishi mpaka hamjui nini cha kufanya, kama hivi vijimafua mnaviona ni hatari kwanini mnasubiri mpaka muulekezwe na serikali? Nyie si mna akili sana fanyeni mnachoona ni sahihi, make wengine tukisema misimamo yetu mnaiita siasa!!

Acha ujinga we mtoto.
 
sijaona tanzia ya ajari mkuu kuwa mkweli mambo si mambo alafu inapiga wanazuoni sana sijajua shida nini
MJG.jpg


Wiki hii haijawa njema kwangu. Nimempoteza mjomba wangu, rafiki yangu akampoteza mama na baba yake kwa kufuatana. Kabla sijakaa sawa nikapata taarifa za msiba wa kaka Muksin Mambo, kisha nikapata taarifa za msiba wa dada Tuli Nasa.Kabla sijahamaki tukampoteza mzee Arcado Ntagazwa (Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini Chadema).

Leo najulishwa rafiki yangu Wenseslaus O W Jnr amempoteza baba yake mzazi. Kabla machozi hayajakauka kaka yangu na mwanafamilia mwenzangu wa GIFTED HEART Anthony Mtaka akampoteza mama yake mzazi. Wakati tukijiandaa kwenda kumpumzisha mama yetu huko Musoma, napata taarifa kuwa kaka John W. Jacob amefariki dunia kwa ajali ya gari.

Wakili msomi, John Jacob alikua mwanafamilia active wa GIFTED HEART FAMILY. Hajawahi kuacha kushiriki tukio lolote la kurudisha tabasamu kwa watanzania. Maisha yake yalikua sadaka kwa jamii hasa watu wenye mahitaji. Alijitoa sana kusaidia watu kwa namna mbalimbali. Rafiki yetu mmoja alipopata kesi ya uhujumu uchumi alijitolea kumsaidia bila malipo.

Mwaka jana baadhi ya wanafamilia wa GIFTED HEART tulimtembelea ofisini kwake Manyoni, Singida. Pamoja na mambo mengine tulimpongeza kwa namna alivyokua akijitoa kwa jamii. Kwa muda wote tuliokaa Manyoni alitukirimu kwa viwango vya juu sana.Alikua rafiki mwema sana na asiye na makuu. Mambo makubwa mawili aliyoyapenda sana ni kusoma vitabu na kusaidia wenye mahitaji. Tulishirikiana nae kwa mambo mengi ya kijamii na kuweka mipango mingi ya maendeleo. Bahati mbaya kifo kimekatisha mipango hiyo.

Aliposikia taarifa za msiba wa mama Mtaka aliniuliza kama familia ya GIFTED HEART itatoa uwakilishi wa kwenda msibani Musoma. Nikamwambia Ndio. Akasema yeye hataweza kushiriki lakini akatuma mchango wake wa rambirambi nimsaidie kuwakilisha.Muda mfupi baada ya kutuma rambirambi yake mauti ikammeza kwa ajali. Laiti kama angejua yaliyo mbele yake, pengine angeahirisha safari yake. Eeh Mwenyezi Mungu utusaidie kuzihesabu siku zetu.

Natoa pole za dhati kwa familia yake (mke, watoto, na ndugu) pamoja na familia ya Gifted Heart. Kwaheri kaka yangu John, kwaheri wakili msomi. Tutaonana tena Paradiso. Eeh Mungu tunakushukuru kwa maisha ya ndugu yetu John. Kwa miaka michache ya uhai uliyomjalia aliweka alama kwenye maisha ya wengi.
 
Back
Top Bottom