Prof. wa Kenya awaumbua wabunge wa TANZANIA

Acheni kujidhalilisha,

kenya nako kuna watu kibao hawawezi kuelewa kingereza vizuri. Hawa jamaa mnawapa sifa wasizokuwa nazo.
Kwani hata nyie waTZ mnaokijua kingereza huwa mnasoma hizo sheria. Hatuishi kwa kusoma sheria kila siku, utasoma ngapi bana.
 
Wapo wabunge wetu hata ulete muswada kwa kiswahili au lugha yao ya kikabila bado hawataelewa.Tunawachagua kwa ushabiki sio uwezo na gharama yake inakula kwetu.Katika EAC sisi ndio mazoba,hata kama neno hilo ni la kuuzi lakini ndio ukweli


Mnajikatisha tamaa bure, tembea uone. matatizo yako usiyafanye ni ya waTZ wote.
Watu tuko vizuri wewe bakia na woga wako
 
Bitabo na Wana JF,
Tatizo limeanzia kwa watawala wetu, hawakuchukua muda kutafakari kuhusu hili suala la lugha ya kingereza, walipaswa kuendelea na kiswahili chetu na kujivunia lugha yetu, mifano Nchi zilizoendelea France, Ujerumani, Hispania, Japan zinadumisha lugha zao, na ukienda kufanya kazi au kusoma unapaswa kujua otherwise utakuwa mgeni kila siku.
maadam, toka mwanzo na wengi wetu tumekulia kwa kiswahili ilipaswa kiswahili kiendeleee kutumia mpaka hapo lugha ya kingereza itakaposhika kasi, maana ukweli asilimia kubwa kingereza kinawapiga chenga,
My take: Kiswahili kwanza halafu lugha zingine baadae
Nawakilisha



Kwenye kikao cha kujadili report ya APRM leo jijini Dar es Salaam, Prof. mmoja wa kenya amewauliza wabunge wetu ni kwa nini wanatunga sheria kwa Kiingereza wakati watekelezaji na wasimamizi wa sheria hizo hawajui Kiingereza wanajua Kiswahili. Na swali limeulizwa kwa Kiswahili lakini cha ajabu Kamati ya sheria na katiba kupitia kwa Mh. Angela Kairuki akajibu kuwa wameshaliona tatizo na sasa wameishauri wizara ya sheria na mambo ya katiba kuhakikisha wanaprint sheria kwa lugha zote mbili, Kiswahili na Kiingereza. japo alitoa jibu hilo kwa Kiingereza.\

Source: Startv News saa mbili usiku

Je, ina maana tatizo hili ndo limeonekana sasa wakati hata wabunge wenyewe Kiingereza kinawapa kazi kujieleza???
Kama Mtanzania nimeona aibu kwa swali hili kutoka kwa majirani zetu
 
We dont like to maintain our culture, like wachina. Our intention is to immutate others' traditions and norms.
 
Acheni kujidhalilisha, kenya nako kuna watu kibao hawawezi kuelewa kingereza vizuri. Hawa jamaa mnawapa sifa wasizokuwa nazo. Kwani hata nyie waTZ mnaokijua kingereza huwa mnasoma hizo sheria. Hatuishi kwa kusoma sheria kila siku, utasoma ngapi bana.
Hivi kwenye ile mikataba yetu ya madini serikali ilisemaje? haikuja kuonekana kuwa wale waliopewa jukumu la kupitia mikataba na kusign wana uelewa mdogo wa hizo sheria ndo maana wakatuingiza chocho? Hivi nikuulize wale madiwani na VEO wanajua kiingereza ili kuweza kusimamia sheria zinazotungwa na bunge? Ila sishangai maana hii ni nchi ya kusadikika na kushangaa.
 
Hivi na katiba mpya itaandikwa kwa Kiingereza? Mnawaambia wananchi watoe maoni yao kwa kiswahili halafu mtaenda kuwaletea katiba kwa lugha ipi??? Kazi ndo iko hapo.
 
..wa-Tanzania tulifanya makosa kutokutilia mkazo lugha ya kiingereza.

..sasa wenetu wanageuzwa wapagazi ktk nchi yao wenyewe.

hatukufanya makosa mkuu!lugha si kitu katika kuleta maendeleo, tatizo ni kwamba sisi mpaka sasa si wa moto wala baridi bali tupo vuguvugu!
#changeTanzania
 
hahaaaaaaaa mnashangaa mahakamani Mwogozo wa kodi tanzania kutoka TRA umeandikwa kingereza wakati hata hao wafanyakazi wa TRA wenyewe kingereza hawajua achilia mbali walipa kodi wenyewe amabo ni kama 95% hawajui kabisa kingereza hii nchi tunabuluzana tu.
 
mkuu kwani kingereza ndo maisha? Nenda kenya uone pamoja na kuongea kingetreza watu wana maisha duni sana

wachina wa kariakoo mbona hawajui kingereza na wanapiga business?

unaposema mbona kenya wanaishi maishi magumu mbona husemi ni asilimia ngapi? ndugu yangu, pamoja kenyatta alikuwa hana kidomo kidomo cja kujifanya anataka kuikomboa Africa, lakini huyo mzee kawajengea maisha bora wakenya kuliko nchi yeyote kusini mwa jangwa la sahala.

Kiingereza ni lugha muhimu sana ili kuwasiliana na wenzako nje ya mipaka. Ona sasa wakenya wamepata ujiko wa kuitangaza CCTV-Africa. hii yote ni kwa sababu ya kujua kiingereza. Ona sasa wanachukua kazi ambazo watanzania wangezifanya nchini mwao kama wangejua kiingereza.

kwenye kufuta kiingereza mashuleni, ni lazima tukiri wazi kuwa Nyerere hakututendea haki kabisaa. leo hii ingawa tunazidi kusema zidumu fikira sahihi za mwenyekiti wa CCM, ni usemi potofu kabisaa.
 
Back
Top Bottom