Prof. wa Kenya awaumbua wabunge wa TANZANIA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof. wa Kenya awaumbua wabunge wa TANZANIA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bitabo, Mar 17, 2012.

 1. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Kwenye kikao cha kujadili report ya APRM leo jijini Dar es Salaam, Prof. mmoja wa kenya amewauliza wabunge wetu ni kwa nini wanatunga sheria kwa Kiingereza wakati watekelezaji na wasimamizi wa sheria hizo hawajui Kiingereza wanajua Kiswahili. Na swali limeulizwa kwa Kiswahili lakini cha ajabu Kamati ya sheria na katiba kupitia kwa Mh. Angela Kairuki akajibu kuwa wameshaliona tatizo na sasa wameishauri wizara ya sheria na mambo ya katiba kuhakikisha wanaprint sheria kwa lugha zote mbili, Kiswahili na Kiingereza. japo alitoa jibu hilo kwa Kiingereza.\

  Source: Startv News saa mbili usiku

  Je, ina maana tatizo hili ndo limeonekana sasa wakati hata wabunge wenyewe Kiingereza kinawapa kazi kujieleza???
  Kama Mtanzania nimeona aibu kwa swali hili kutoka kwa majirani zetu
   
 2. J

  JokaKuu Platinum Member

  #2
  Mar 17, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  ..wa-Tanzania tulifanya makosa kutokutilia mkazo lugha ya kiingereza.

  ..sasa wenetu wanageuzwa wapagazi ktk nchi yao wenyewe.
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Tukisubiri wabunge (na hasa wabunge wa ccm) kufanya jambo la maana hii nchi itafutika. Hakuna cha lugha mbili, lugha ya Taifa ni Kiswahili na kila mtu anafahamu hii lugha, sasa kwa nini bunge linaongelea habari ya kuchapisha miswada/sheria kwa lugha mbili? Kama Tanzania haitasimamia lugha yake yenyewe nani afanye hivyo?
   
 4. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  swali zuri mi nachofurahia wakenya ni kwamba wanatuamsha sasa tukiamua kuendelea kulala then we are doomed tukiamka tutaenda nao sawa na hapo sasa ndio watatuelewa na kutusoma. tuamke tuwe watu wakusoma, kuipenda nchi yetu kiukweli, watu wenye maono, na zaidi tuargue na enough heavy points, na kubwa tujae ujasiri kwamba tukisema waziri toka atoke tena siku hiyo hiyo.
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Mar 17, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  FJM,

  ..hiyo ni kwasababu watoto wa viongozi wa CCM na serikali hawajui kusoma na kuandika Kiswahili.

  ..Kiswahili wanachokijua wao ni cha kuombea maji tu.
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Na hapo ndipo wanapotumaliza hawa wakubwa. Zaidi ya nusu ya wabunge hawaelewi kiingereza. Sasa wanapitishaje miswada iliyoandikwa kwa kiingereza? Hii kwa kweli ni scandal ya karne! Yaani wachina wapitishe miswada iliyoandikwa kwa kifaransa? au hata kiingereza huku nusu wa wajumbe wa baraza lao wakiwa hawaelewi nini kimeandikwa? Haiweze tokea, lakini hapa kwetu wabunge wanasaka posho tu, wameelewa au hawajelewa miswada inasema nini kwao sio kitu!
   
 7. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #7
  Mar 17, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  mkuu kwani kingereza ndo maisha? Nenda kenya uone pamoja na kuongea kingetreza watu wana maisha duni sana

  wachina wa kariakoo mbona hawajui kingereza na wanapiga business?
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  Mar 17, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hahahahaaaa! Mimi hili jambo nimeshalipigia sana kelele. Sheria ni za Watanzania - sasa kwa nini zitungwe katika lugha ya kigeni?

  Kwangu haiingii akilini kabisa na ni ujinga na upumbavu wa hali ya juu. Watetezi utawasikia wanasema 'oh eti Kiswahili hakina misamiati ya kutosha' na upuuzi mwingine kama huo.

  Nami huwa nawauliza kwani Kiingereza kina misamiati ya kutosha? Ni maneno mangapi ambayo Kiingereza imeazima toka lugha zingine? Kiingereza kimeazima hadi kwenye Kiswahili.

  Halafu kwenye misamiati ya sheria Kiingereza hicho hicho kimeazima sana toka kwenye Kilatini sasa iweje Kiswahili kisiwe na misamiati ya kutosha?

  Lugha hukuzwa na kupanuliwa na watumiaji wake. Mimi nakataa katakata hiyo dhana ya eti Kiswahili hakijitoshelezi. Kama hakijitoshelezi kwa nini tusitengeneze misamiati mipya? Au kwa nini tusiazime misamiati mingine zaidi?

  Hakuna sababu yoyote ile ya msingi zaidi ya uvivu na hali ya kujiona hatuwezi.
   
 9. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Hivi Prof maji marefu (mfano) anaelewa kweli Ki English? Hapa juzi wakati wanajadili marekebisho ya sheria ya kutunga katiba mpya, hata sikumuona yeye wala Kibajaji wakichangia. lakini ukienda kwenye hansard za bunge utakuta waliunga mkono hoja kwa 100%
   
 10. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,422
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  hata huku mtaani sign boards na matangazo ni kiingereza tu wakati walengwa ni asilimia 95 hawajui kiingereza. Kimsingi nchi yetu tuna tatizo la kasumba.
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  sidhani kama ni kuumbua, mimi nimeona ni kuuliza tu
   
 12. M

  Makupa JF-Expert Member

  #12
  Mar 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  mkuu.we jipe moyo tu kingereza ndio kiswahili cha dunia, wachina wa kariokoo mkuu ni kama wale wapiga debe wa posta , kujua kingereza kwake haimsaidii chochote
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  Mar 17, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Halafu sidhani kabisa kama wabunge wetu wana uwezo wa kujadili mijadala yao kwa Kiingereza mwanzo mwisho huko bungeni. Sidhani kabisa aisee.
   
 14. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,651
  Likes Received: 21,866
  Trophy Points: 280
  Wapo wabunge wetu hata ulete muswada kwa kiswahili au lugha yao ya kikabila bado hawataelewa.Tunawachagua kwa ushabiki sio uwezo na gharama yake inakula kwetu.Katika EAC sisi ndio mazoba,hata kama neno hilo ni la kuuzi lakini ndio ukweli
   
 15. PakiJinja

  PakiJinja JF-Expert Member

  #15
  Mar 17, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 834
  Likes Received: 329
  Trophy Points: 80
  Eti wenyewe munasingizia komoni wesi.
  Wanaacha kula kwa usawa pale kamba zao zinaishia wanataka kula anapokula jirani.
   
 16. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #16
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  tahadhari jamani jamani jamani, umetuzunguka huyu msomi wa kikenya
  nia yake ataingize mkenge, yaani wabongo tuzidi kukumbatia lugha ya shambani (kiswahili) ili tuzarau lungha ya biashara ya dunia nzima na ambayo nchi zisizo jua kabisa wanatuonea wivu sisi makoloni ya england, tizama nchi ngapi hujiunga na umoja wa madola na kuacha asili yao ya labda ureno mfano msumbiji, au ya ufaranza mfano rwanda? jamani kenya inataka kutufanya shamba lake, ili sisi tulime tu, na mazao yapitie kwa wanaojua lugha ya biashara yaani Kenya. professa hatari!!!
   
 17. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #17
  Mar 17, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Sikubaliani na wewe kwa sababu unapozungumzia uzalendo wa wananchi unazungumzia mapenzi yao kwa lugha yao na sisi lugha yetu ni kiswahili!! Haingii akilini wakati wajumbe wanaoomba kuwa wabunge wa bunge la Afrika MashAriki wanalazimishwa kuoomba kura kwa kiingereza toka kwa wabunge wa bunge letu wengi wao hawajui lugha ya kiingereza kwa ufasaha; sio hivyo tu hawa wabunge wanapopiga kura kuwachagua wabunge wa bunge la Afrika mashariki waNAFANYA HIVYO KWA NIABA YA WATANZANIA TAKRIBANI MILLIONI 50 WENGI WAO HAWAJUI KIINGEREZA , HIVYO BASI KWAVILE WAKATI WA UCHAGUZI HUO WANANCHI KWA KUPITIA TEKNOLOJIA WATAKUWA WANAWAONA HAO WATAKAOMBA UTUMISHI NI VYEMA WAKAJIELEZA KWA LUGHA YA KISWAHILI ILI WANANCHI WAWEZE KUJUA KAMA WALE WAWAKILISHI WAO WATAPIGA KURA NA KUWACHAGUA WATU WATAKAOWAKISHA MASLAHI YAO NA SIO MASLAHI YA WATU BINAFFSI
   
 18. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #18
  Mar 17, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  mkuu Chasa ebu acha kujifariji ktk msiba kwamba marehemu ajafariki!
   
 19. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #19
  Mar 17, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Katika mambo ambayo yamekuwa yakinishangaza ni kusikia kwamba lugha rasmi ya kisheria hapa nchini ni kiingereza, yaani ukienda mahakamani hasa mahakama kuu ni kiinglish tuuu hadi mtu unashindwa kuelewa nini maana ya sisi kama nchi kuwa na lugha yetu ya taifa- Kiswahili.

  Kitu kingine cha ajabu sana katika nchi ambayo zaidi ya asilimia 80 hawajui kiingereza, na hata katika hiyo asilimia 20 wanaojua kiingereza ni wachache sana wanaokimudu bado tunaendekeza matumizi ya kiingereza. Serikalini kiingereza, bungeni kiingereza, mahakamani kiingereza, tukihudhuria makongamano/warsha/semiana kiingereza!!
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Mar 17, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Sasa kama mtu hujui Kiingereza huko mahakama kuu utajuaje kama unatendewa haki?

  Halafu basi ni afadhali hata wangekuwa wanaongea Kiingereza kizuri na kilichonyooka manake ukiwasikia...hmmmmm
   
Loading...