Prof. Tibaijuka Kikaangoni, CCM Waitana

Prof. Tibaijuka Kikaangoni, CCM Waitana

1954tanu

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2013
Posts
1,038
Reaction score
487
Bajeti ya Wizara ya Ardhi na Makaazi iko katika ati ati ya kupitishwa na bungeni leo hii. CCM baada ya kupima upepo wameita wabunge wao mapema wakutane baadae ili kuokoa jahazi.

Hotuba ya waziri prof..Tibaijuka ambayo imekuwa tofauti kabisa na ile ya kamati ya bunge juu ya wizara hiyo. Hotuba ya kamati imekuwa chungu mno.Imeibusha uozo mwingi ndani ya wizara.

Aidha, kama haitoshi hotuba ya waziri kivuli kwa wizara hiyo mh.H.Mdee imeanika ufisadi mkubwa ndani ya wizara hiyo,hususan kwenye suala la kigamboni na chasimba mkoani Dar es Salaam.

Pia,wabunge wengi wanaosimama wanasema hawaungi mkono hoja ya waziri. Kwa jumla,prof.Tibaijuka leo maji yamemfika shingoni.

Hata hivyo,kwa kuwa wabunge watetezi wa ufisadi na wanafiki wameitana basi wote tunatarajia wataufyata.Mikia yao wataiweka katikati ya miguu kama mbwa mwoga afanyavyo.
 
Ufisadi gani ulioibuliwa zaidi ya malalamiko ya kisauti?
Mhhhh!!!!!!!!!! Sijawahi fungua huku nikakukosa. Kila post iwe udaku wewe upo tu. CCM wamekupa tenda nn mamaa ili na mm nijiunge angalau naweza badilisha upepo wa maisha.
 
Ardhi in a migogoro mingi kupindukia
 
Mhhhh!!!!!!!!!! Sijawahi fungua huku nikakukosa. Kila post iwe udaku wewe upo tu. CCM wamekupa tenda nn mamaa ili na mm nijiunge angalau naweza badilisha upepo wa maisha.

Mkuu uko sahihi, mwanzoni nilipokuwa nasikia kuna watu wanalipwa buku 7 kwa kushinda humu nilikuwa napinga, lakini sasa naamini kwani kuna watu muda wote wapo hapa na mbaya zaidi wanatetea mambo ya kifisadi. Haiwezekani uwe uko hapa 24 hrs! huna kazi ya kufanya? unapata wapi pesa ya kifurushi kama hata kazi hufanyi? wewe umekuwa mods?
 
Wenye akili huwa hatupati shida na huyo mhuni. Turudi kwenye mada
 
Mhhhh!!!!!!!!!! Sijawahi fungua huku nikakukosa. Kila post iwe udaku wewe upo tu. CCM wamekupa tenda nn mamaa ili na mm nijiunge angalau naweza badilisha upepo wa maisha.
unabishana na official ID ya Lumumba?
 
Mwanaume lumumba ni Ally kessy tu, jana kawaonyesha zanzibar njia nyeupeeee!!!! Hahahaaa sasa hizo serikali mbili sijui zitapatikanaje zanzibar ikisepa? Mi ccm ni mizigo.
 
Mkuu uko sahihi, mwanzoni nilipokuwa nasikia kuna watu wanalipwa buku 7 kwa kushinda humu nilikuwa napinga, lakini sasa naamini kwani kuna watu muda wote wapo hapa na mbaya zaidi wanatetea mambo ya kifisadi. Haiwezekani uwe uko hapa 24 hrs! huna kazi ya kufanya? unapata wapi pesa ya kifurushi kama hata kazi hufanyi? wewe umekuwa mods?
Mkuu kuna watu wako kazini hapa kumbe? Mimi naingiaga kwa machale ila kila nikitia mguu yupo kila jukwaa. sasa huyu mtu hana kingine cha kufanya?
 
Back
Top Bottom