Prof. Mukandala aongezewa mwaka mmoja kuwa Makamu Mkuu wa UDSM

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Dr. Jakaya Mrisho Kikwete,kupitia kwa Baraza la Chuo na mashauriano na Rais John P. J. Magufuli, amemuongezea mwaka mmoja uongozini Makamu Mkuu wa Chuo hicho,Prof. Rwekaza Sympho Mukandala.

Prof. Mukandala,jana,alitarajiwa kumaliza kipindi chake cha pili cha miaka mitano. Aliteuliwa kuwa Makamu Mkuu wa UDSM mwaka 2006. Sasa atahudumu hadi Disemba 4 mwaka 2017.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM.pdf
 
Anyway labda hayupo wa kufanana na "kasi" ya Mkuu wa chuo hicho ama na kasi ya serikali hii ya awamu ya tano!! Kila la kheri Mukandala.
 
 

Attachments

  • index.jpg
    64.5 KB · Views: 70
Teuzi zifanywe na Rais mkataba unaongzwa na Baraza .....................!!
 
Retired, ukubwa dawa.
Wanasiasa wanakera, anahubiri kujiajili, mbona yeye anabaki? Si aondoke akajiajili kama ni virahisi hivyo!Hakuna wa kufanya utawala anaoufanya? Angekuwa daktari wa upasuaji ubongo, moyo ningelimuelewa, lakini hizi blah blah za utawala, everybody can manage particularly those so called Professors at his place!
 
Kwa mtizamo wangu inawezekana Maprofesa wetu wanastaafu katika umri mdogo (sijasema siyo wazee) na wakitoka hapo hawana kazi wanayokwenda kufanya zaidi ya kunywa Whisky na kulea wajukuu.
Sasa waache blah blah za vijana mjiajili, let then shut their mouths! Let nature take its course!
 
Mwacheni Mshaija amalize projects zilizoanza nae kama hostel n.k ili hata kama kutakua na majipu yamtumbukie mwenyewe
 
Mkuu cha kushangaza Maprofessa wengi waliostaafu kwenye Public Universities sasa wako kwenye Private Universities.Vibabu vipo uko mpaka unashangaa nini maana ya kustaafu!! Kibaya zaidi kwenye miaka ya tisini na mwanzoni mwa miaka ya 2000 walikuwa wanabana sana watu wasiwakaribie, matokeo yake kukawa na gap, ambayo ndio inajazwa jazwa sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…