Ulimaanisha ukata? maana ukwasi ni kuwa na fedha ya kutoshaKuna jamaa zangu wanafanya kazi udsm jinsi wanavyolalamika na ukwasi uliopo hapo udsm kiasi kwamba wanafikiria kuacha kazi. Ukiangalia story nzima wanamlalamikia huyo jamaa, na kama ndio anafanya ufisadi wa namna hiyo basi hafai kuwepo hapo ili kukinusuru hicho chuo. mbona wakati wa luhanga mambo yalikuwa mazuri!!!.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Prof.Rwekaza Sympho Mukandala amefanya kufuru kimatumizi UDSM.Katika safari yake ya kutembelea Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Mkwawa Iringa almaarufu kama MUCE,Prof.Mukandala amekodi ndege ndogo ya kumpeleka huko yeye na msaidizi wake mmoja kwa thamani ya takribani shilingi milioni nne.
Kama hiyo haitoshi,Prof.Mukandala aliagiza magari yake mawili ya kifahari aina ya V8 kutangulia Iringa kumpokea yakiwa 'full tank' na bila mtu yeyote ndani yake.Fedha zote anazozitumia ni mali ya UDSM.Nchi hii yaelekea wapi jamani?
UDSM kilikuwa cha maana enzi za Kuhanga..
unampenda dume mwenzio?Haaahaa! Jamaa nampenda kwa kujipenda na kufanya mazoezi karibu kila asubuhi....ila mambo mengine namshangaa sana. Toka akiwa REDET mpaka leo hii namshangaa sana huyu bwana mkubwa,lol!
UDSM kilikuwa cha maana enzi za Kuhanga..
Wait a minute, assuming uliyondika hapa ni kweli, je hizo V8 zilitumwa zikiwa kwenye auto pilot mode?
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Prof.Rwekaza Sympho Mukandala amefanya kufuru kimatumizi UDSM.Katika safari yake ya kutembelea Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Mkwawa Iringa almaarufu kama MUCE,Prof.Mukandala amekodi ndege ndogo ya kumpeleka huko yeye na msaidizi wake mmoja kwa thamani ya takribani shilingi milioni nne.
Kama hiyo haitoshi,Prof.Mukandala aliagiza magari yake mawili ya kifahari aina ya V8 kutangulia Iringa kumpokea yakiwa 'full tank' na bila mtu yeyote ndani yake.Fedha zote anazozitumia ni mali ya UDSM.Nchi hii yaelekea wapi jamani?
Luhanga mkuu!
chukua "LIKE" mkuu NYANI
UDSM kilikuwa cha maana enzi za Kuhanga..
Sidhani kama mtu anayeitwa KUHANGA amewahi kuwa VC pale UDSM since 1961 chuo kilipoanzishwa. Hebu NN kaperuzi upya taratibu kwa ufasaha
Milton Mahanga naye alikuwa udsm!
Ndiyo nani huyo?
Unaona sasa....wewe umezaliwa lini kwani?
Kutoka mwaka 1980 - 1988 vice chancellor wa UDSM alikuwa Nicholas Kuhanga! Bonyeza hapa uongeze ufahamu wako.
Dah,kumbe NN umekula chumvi ya kutosha.