Prof. Muhongo umetisha

ASHA NGEDELE

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
784
326
Nimetoka muda si mrefu kumsikiliza waziri wa nishati na madini na amefafanua kwa kifupi baadhi ya mambo ambayo ameamua kuyabadili kwenye utendaji kazi wa Tanesco. Kwa maelezo yake amesema kuanzia Mei 2012 mtu yeyote atayeomba kuunganishwa na Tanesco kupata umeme, anatakiwa kupatiwa huduma hiyo ndani ya mwezi mmoja.

Nadhani amefanya uamuzi wa busara, si tu kwetu wananchi bali atasaidia hata Takururu kwa upungufu wa rushwa kwenye kuunganisha umeme.

Kwa umeo wangu mdogo nafikiri huyu waziri atafanya mambo makubwa sana kama tu mipango yale ni kweli itatekerezeka kama inavoonekana.

Asante Muhongo
 
Anashindwa nini kutoa maelezo yanayoeleweka kuhusu mgodi wa kiwira .

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Mhungo si ni mwanasiasa tu, anasema ili muone serikali inafanya kazi? Muulize huyo Mhungo ni kwa kiasi gani wameiwezesha TANESCO ili iweze kutekeleza hilo agizo? Maana nguzo tunauziwa, waya na wenyewe tunauziwa. Mara utaambiwa Luku zimeisha. Mtu unaambiwa nguzo lazima ununue halafu wakishakuwekea umeme wanakwambia nguzo si mali yako. Mimi nilinunua nguzo kwa about milioni moja na bado siku chache baadaye majirani wakawa wanaunganisha umeme bure tu kutoka kwenye nguzo yangu. Kuwauliza TANESCO wananambia hakuna mtu anayemiliki nguzo aaarghh! Hakuna serikali niliyowahi kuichukia kama ya Kikwete.
 
Tanesco ilikuwa inauza nguzo tangu enzi za Mkapa, so ungeichukia serikali ya Mkapa kabla ya kikwete au serikali ya ccm kwa ujumla

Huyu waziri anaongea maneno matupu Tanasco hatoiweza... alijaribu Idrisa kuwanyoosha kwasababu ya siasa za kidin waka muondoa..

siasa tupu hamna kitu hapo..
 
Mhungo si ni mwanasiasa tu, anasema ili muone serikali inafanya kazi? Muulize huyo Mhungo ni kwa kiasi gani wameiwezesha TANESCO ili iweze kutekeleza hilo agizo? Maana nguzo tunauziwa, waya na wenyewe tunauziwa. Mara utaambiwa Luku zimeisha. Mtu unaambiwa nguzo lazima ununue halafu wakishakuwekea umeme wanakwambia nguzo si mali yako. Mimi nilinunua nguzo kwa about milioni moja na bado siku chache baadaye majirani wakawa wanaunganisha umeme bure tu kutoka kwenye nguzo yangu. Kuwauliza TANESCO wananambia hakuna mtu anayemiliki nguzo aaarghh! Hakuna serikali niliyowahi kuichukia kama ya Kikwete.
acha uongo mkuu huyu ni mwana geolojia si mwana siasa kamwe kama una yako ulotumwa kayajadili na mkeo sio kusingizia watu makini kama professor muhongo . ndo maana hajawahi kuomba ubunge mahala popote na amesema kuwa asiposikilizwa anrudi kufundisha.
 
Pambafuu..!!hyu mhongo mbona ana mawazo finyu kiasi hki,watu 2meshatapeliwa mpka bac hlo haliwezekan serikali DHAIFU haishiwi porojo kwa wananchi wake..huu ni upuuzi
 
zisije zikawa kerere za chura tu huku tembo akinywa maji kwa kwenda mbele.
 
Je kama mtu atalipa na asiwekewe umeme kwa visingizio vingi tu vya mara nguzo, mara luku, mara nyaya hakuna, atawafukuza kazi au na yeye ashaanza yale yale ya shemeji umeniona?!
 
Mwezi mmoja kuanganishiwa umeme baada ya kulipa ni muda mrefu sana, anagesema hata baada ya wiki mbili ningeelewa.
Kumbuka mteja analipia karibu kila kitu kuunganisha umeme, Tanesco wanatakiwa waje na vifaa na mafundi wa kuanganisha (hata vifaa vingine wanakwambia mteja ununue) halafu bado tena nisubiri kwa mwezi mmoja! Huyo prof atakuwa hayuko serios aisee...!
 
....kwanza atoe maelezo sahihi juu ishu ya Kiwila...vinginevyo bado hajatisha.

Mbona Anna Makinda anamkingia kifua Waziri wa Nishati na Madini? Ningefurahi sana kama bunge letu lingeweza kugeuka bunge la Ukraine hata kwa siku moja tu. Huyu mama ni DHAIFU na kichefuchefu pale bungeni.
 
Back
Top Bottom