Prof. Muhongo umetisha

Kumbe bado ujaijua vizuri serikali hii! Kuanzia baba mpaka watoto waongo alafu wana sahau walicho ongopa. Tatizo sio tanesco bali serikali yetu. Mi naona bora tutawaliwe tena bado akili za viongozi wa ccm zinafanana kama minyoo.
 
Mkuu wa kaya dhaifu!, serikari yake dhaifu, Mawadhiri wa magamba dhaifuu akiwemo huyo mu-hongo
 
acha uongo mkuu huyu ni mwana geolojia si mwana siasa kamwe kama una yako ulotumwa kayajadili na mkeo sio kusingizia watu makini kama professor muhongo . ndo maana hajawahi kuomba ubunge mahala popote na amesema kuwa asiposikilizwa anrudi kufundisha.
I see, wewe unaishi dunia gani? Mawaziri wangapi wameingia madarakani na mkwara mbuzi wakaishia kuwa waongo na wazandiki kama wengine tu? Kwani Magufuli anapiga kelele kiasi gani na kutoa maagizo kiasi gani? Utekelezaji upo wapi? Halafu issue za JF zina uhusiano gani na mke wangu? Nafikiri ufike wakati sifa mojawapo ya kujiunga na JF iwe ni umri maana hawa watoto wa sekondari wanaandika chochote tu wanachoona wanaweza kuandika. Hawatumii hata sekunde kufikiria.
 
Hilo mbona lilikuwepo tangu zamani? tatizo ni utekelezaji. Usikubali kuridhishwa na hao wanasiasa tena wa CCM
 
Nimetoka muda si mrefu kumsikiliza waziri wa nishati na madini na amefafanua kwa kifupi baadhi ya mambo ambayo ameamua kuyabadili kwenye utendaji kazi wa Tanesco. Kwa maelezo yake amesema kuanzia Mei 2012 mtu yeyote atayeomba kuunganishwa na Tanesco kupata umeme, anatakiwa kupatiwa huduma hiyo ndani ya mwezi mmoja.

Nadhani amefanya uamuzi wa busara, si tu kwetu wananchi bali atasaidia hata Takururu kwa upungufu wa rushwa kwenye kuunganisha umeme.

Kwa umeo wangu mdogo nafikiri huyu waziri atafanya mambo makubwa sana kama tu mipango yale ni kweli itatekerezeka kama inavoonekana.

Asante Muhongo
Hizi ndo pure Musoma products siyo kama ile Masatu iliyozaliwa Musoma kwa bahati mbaya. Hii nchi haitanyooka hadi mura ingine itakapo weka maskani pale magogoni
 
Atueleze jinsi watakavyo fanya juu ya vyanzo vya nishati ya umeme? Na sikutegemea maji ambayo hayapo! Badala ya kufikiri jinsi ya kupata chakula anafikiri jinsi ya lula.magamba wengine bwana.
 
. Kwa maelezo yake amesema kuanzia Mei 2012 mtu yeyote atayeomba kuunganishwa na Tanesco kupata umeme, anatakiwa kupatiwa huduma hiyo ndani ya mwezi mmoja].



Kama kuanzia mwezi Mei 2012, basi tayari mwezi na ushee umeshapita. Tunataka ripoti ya utekelezaji maana Juni inakatika angalau tujue wangapi katika mwezi Mei wamehudumiwa kwa kufuata agizo la waziri. Wala hakuna haja ya kusubiri miezi tisa kama anavyopendekeza rafiki yangu. Agizo la serikali makini linatekelezeka na linatekelezwa kama lilivyotolewa na la kwake ndani ya mwezi mmoja kuanzia Mei. Hii ni Juni nayo inayoyoma! Ripoti Prof?

Kinyume cha hapo ni longolongo ileile tuliyoizoea kutoka serikali ileile inayoongozwa na chama kilekile. Tusutegemee mabadiliko. LOL!
 
Back
Top Bottom