NJOZI
Ni kweli Marekani na Asasi yake ya Kijasusi wana nguvu za kiuchumi, kijasusi na hata kiteknolojia na kwamba pamoja na kusudio la kuhakikisha kuwa Marekani inakuwa nchi yenye maendeleo kwa watu wake, bado agenda ya njozi ya kutaka nchi yao iendelee kuwa ‘kiongozi na askari wa dunia' inawasumbua baadhi ya Wamarekani. Hata inapokuja kwenye kumtafuta nani awe Rais wao, huwa wanapenda kuwauliza wagombea hilo swali la hiyo njozi ingawa kwa namna tofauti tofauti.
HALI HALISI
Pamoja na nguvu na njozi zao, ni imani yangu kuwa nchi nyingine kama za kwetu pamoja na kuonekana ‘wadogo' kwa mataifa hayo ‘makubwa', si kweli kuwa hatuna kabisa sauti juu ya mambo kama haya ya UBADHILIFU wa wazi, maana watu wamekuwa na ulewa mkubwa na haki za binadamu zinatetewa kila mahala hata ndani yanchi ‘zilizoendelea' ambako kuna wananchi wengi sana (nguvu ya umma) ambao hawataki kuona Mataifa yao yajulikane kwa uovu na kuchukiwa na mengine kutokana na uonevu au wizi. Sote tunakumbuka hata suala la RADA likivyoanza kupigiwa kelele Uingereza, kabla ya sisi wenyewe hatujafikia kiasi hicho!
Hata wao si wajinga; wakikumbana na msimamo mkali unatoka kwa mtu mmoja (hata awe Rais au Waziri) au kikundi cha wachache tu basi wanapata nguvu ya kuwashawishi wengine wengi wanaobaki na hakika mwisho wa siku misimamo kama hiyo lazima ishindwe (at least in that material time); lakini wanapogundua kuwa Rais au Waziri anamsimamo mkali na mihimili yote ya dola inamuunga mkono plus wananchi (walio wengi), amini kuwa hakuna cha shirika la kijasusi wala nini hata wao hurudisha siraha nyuma wakiomba dua kusubiria upepo ubadilike!
HATUA:
Kwa vile suala la uzalishaji wa umeme wa nyongeza wa haya majenereta ya Syimbion na mikataba ya huko nyuma toka Richmond haina tija na inatia hasara TANESCO & Taifa letu kwa ujumla waziwazi, nashauri Katibu na Waziri mwenye dhamana kuwapa kazi watathmini wazawa wenye ujuzi na maadili toka hata UDSM & IFM to undertake a in-depth technical & financial appraisal kisha Waziri awasilishe kauli yake kwenye Baraza la Mawaziri na kisha Bungeni juu ya matokeo ya hiyo tathmnini na mapendekezo ya maamuzi magumu ya kuiokoa TANESCO kutokana na makucha ya haya makampuni, mikataba mibovu pia kesi ile kesi isioisha inayosimamiwa na Mh. Mkono & Advocates; halafu wananchi tuone ni nani anayepinga ambaye yuko upande wa hayo makampuni! Kwa kufanya hivi itabidi waamuwe kutupa a fair deal au waondoke, tununue majereta yetu wenyewe! Muda wa kututisha- a sovereign state na kulia lia sasa umekwisha. Kuwekewa vikwazo vya kiuchumi si lazima itangazwe UN, inawezwa kutangazwa kupitia mikataba mibovu, na kampuni kutuwekea mikwara tena ndani ya mipaka ya nchi yetu kwa kutunyima umeme na au kutuuzia kwa bei mbaya na kwa kutafuta support toka kwa wachumia-tumbo wachache wanaofikiri kuwa wanaweza kuwashawishi Wabunge wote kukubaliana na upuuzi huu!
Chukueni hatua sasa!