Prof Mchembe: Wanaoruhusiwa kutoa taarifa za Afya ni Waganga wa Mikoa na Wilaya siyo Wanasiasa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
41,736
2,000
Katibu mkuu wa wizara ya afya Prof Mchembe amesema kuanzia sasa wasemaji wa maswala ya afya ni RMO kwa level ya mkoa na DMO kwa level ya wilaya.

Prof Mchembe amesema waganga wa mikoa na wilaya wana timu za wataalamu na amewataka wanasiasa kutojiingiza kwenye maswala nyeti ya afya.

Kadhalika Prof Mchembe amesema Corona ni ugonjwa wa mlipuko wa maambukizi kwa njia ya hewa kama ilivyo chorela kwa mfumo wa chakula.

Chanzo: ITV habari.

Maendeleo hayana vyama!
 

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
8,559
2,000
Kumbe fukuto la Waziri wa Afya kumtimua Daktari wa Wliaya Chunya limechukua sura nyingine.

Profesa Mchembe, Katibu Mkuu Wizara ya Afya amesema rasmi kuwa ni jukumu la madaktari wa Wilaya na Mkoa kutoa taarifa za magonjwa ya milipuko ndani ya maeneo yao na si wanasiasa, akimaanisha Waziri.

Tamko hilo la Serikali ni kama kumweka katika nafasi yake Dr Dorothy Gwajima kuwa alivurunda kwa kumtimua Daktari wa Wilaya ya Chunya.
 

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
3,663
2,000
Prof.
Heshima kuu kwako!! Nina maswali machache ambayo naomba kama una wasaa utusaidie na ikiwezekana nawe unisikilize labda naweza kukufaa kwa leo.

Kwanza binafsi na kwa uelewa wangu na elimu kidogo niliyo nayo kuliza swali kuwa corona ipo au haipo kwa Tanzania ni kama kuuliza "mama mkwe kavaa nguo ya ndani ya rangi gani",hivyo sitauliza swali hilo.
  1. WHO wasema kuwa hamjatoa takwimu za corona tangu May 2020.Kama ni kweli ni sababu zipi ambazo zimefanya tusitoe takwimu hizo"
  2. Corona ni ugonjwa wa mlipuko lakini mpaka sasa tuna terminology mbili zimezuka,Pneumonia kali na changamoto za upumuaji.Magonjwa haya mawili yana uhusiano wowote na corona?
  3. Tuchukulie kwa mfano wewe kama Prof unaita waandishi wa habari na unasema haya yafuatayo,je utapata hasara gani?Maneno yenyewe ni haya,"Tanzania hatuna corona lakini corona ipo nchi jirani.Kwa kuwa tuna muingiliano na mataifa haya naagiza yafuatayo,abiria ndani ya vyombo vya usafiri vya watu wengi wavae barakoa,kila nyumba iwe na maji tiririka na sabuni....................."
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom