Hii imetokea baada ya Mwigulu kuanza kupinga mabadiliko yaliyofanywa na CDM kwenye blog yake akisema" KUVULIWA VYEO ZITTO NI AKILI NDOGO INATAWALA AKILI KUBWA
Soma aliyoandika Mwigulu ambacho kinaonyesha kumkere sana Prof.
MWIGULU NCHEMBA BLOG: KUVULIWA VYEO ZITTO KABWE"NDANI YA CHADEMA AKILI NDOGO INATWALA AKILI KUBWA"
Joseph MbeleMwigulu NchembaKwanza kabisa, zingatia kuwa maamuzi hayo yamefanywa kidemokrasia. Hakuna mtu katika chama makini ambaye yupo juu ya utaratibu huu
Chama kina wanachama maelfu, hao ndio CHADEMA; sio mtu fulani au mtu fulani. Ungekuwa na akili kubwa ungetambua hilo.
Yawezekana umesoma shule, lakini hujaelimika. Uwezo wako wa kuchambua mambo ni mdogo. Unadhani kuwa na vyet na digirii ndio sifa sana.
Ngoja nikueleze. Mimi ninayeandika hapa ni profesa Mtanzania hapa Marekani. Nilihitimu B.A (First Class, UDSM, 1973), M.A. 1978, UDSM) nikiwa nimepata "A" katika masomo yote, Nikahitimu M.A. (1982) na PhD (1986) katika Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison, Marekani, tena niliibuka na tuzo ya mwanafunzi bora.
Nasikitika kueleza yote haya, na sijawahi, isipokuwa kwa sababaau ya maringo unayoleta hapa, kuwadharau watu waliomaliza high school, imebidi nikupe vidonge.
Pamoja na shahada zangu zote, nawaheshimu watu wote, wakiwemo wazee kule kijini, ambao walinilea na wanaendelea kunilea kwa busara zao. Mtu aliyemaliza hiyo high school anaweza akawa kiongozi mzuri na mwenye busara kuliko yule mwenya Masters au PhD.
Kama kweli unaheshimu shahada za vyuoni anza utafiti huko huko CCM uone wenzako ambao wanaringia shahada ambazo zina utata. Kwa mfano Mary Nagu hakusoma chuo na kupata shahada yake katika chuo kinachotambuliwa na taasisi yoyote ya kitaaluma inayotathmini na kuidhinishaa shughuli za vyuo. Hapa Marekani tunaita "accreditation agencies."
Anza kwanza kuisafisha CCM, ambayo ina watu wanaodai wana PhD kumbe hazijatoka kwenye vyuo vyenye sifa.
Unacholeta hapa ni kile kinachoitwa "intellectual arrogance," ambayo kwa mtazamo wangu ni dalili ya kutoelimika.
Mtu aliyeelimika anapaswa kufahamu kuwa elimu haiko vitabuni au shuleni tu. Inapatikana pia kwa wazee vijijini.
Halafu nashangaa mambo ya CHADEMA yanakuhusu nini. Mimi sio mwachama wa chama chochote cha siasa, ila nimeona nirekebishe dosari katika kauli yako.
Kwa kumuongezea Profesa Mbele na wanajamii wajue wana CCM wenye elimu za walakini
1. Emmanuel Nchimbi na Phd feki toka chuo sio accredited
2. Milton Mahanga mbunge wa kulazimisha wa Ukonga phd feki haiko accredited
3. Mary Nagu phd feki
4. Richard Ndassa mbunge wa Sumve vyeti feki
5. Phillipo Mulugo Naibu Waziri wa Elimu vyeti feki
6. William Lukuvi waziri vyeti feki
7. Steven Wassira masters ya kufanyiwa Marekani alitoa pesa afanyiwe home work na paper
apunguze majigambo tuna data zake
8. Anthony Diallo mwenyekiti wa CCM Mwanza na mbunge wa zamani vyeti feki
9. Sophia Simba masters ya kufanyiwa ndio maana uwezo mdogo
MWENYE MAJINA MENGINE ONGEZA ORODHA
Ndio maana viongozi wa CCM uwezo mdogo maana wengi ni vyeti feki hata walio na vyeti walipata darasani elimu zao hazireflects uwezo wao utafikiria walikomea darasa la saba wakapewa wadhifa mkubwa kuliko elimu zao mfano
Mwigulu Mchemba, William Ngeleja, Celina Kombani, Magessa Mulongo mkuu wa mkoa wa Arusha na wengine wengi