Prof. Mbarawa: Treni hii ya Tanzania siyo high speed train kama zile za vichwa vilivyochongoka, Wananchi eleweni hilo

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,978
141,995
Waziri wa Uchukuzi Prof Mbarawa amewataka Wananchi kutochanganya Treni hii ya Tanzania na zile za high speed zenye vichwa vilivyochongoka.

Prof Mbarawa amesema picha zinazorushwa mitandaoni na watu wasio na nia njema ni zile za high speed zinazotembea zaidi ya km 200 kwa saa.

Za kwetu ni hizi mnazoona tunazipokea na haya ni Mabehewa 14 ya Daraja la tatu(economy) na mwezi February mwakani tutapokea Ya Business class na First class

Mabehewa haya ni kwa ajili ya masafa marefu na yatavutwa na Vichwa vya Umeme lakini yale ya high speed Vichwa vyake vinaunganishwa direct na mabehewa, amesisitiza Mbarawa

Source ITV Habari
 
IMG_0965.jpg

Kwahiyo hao walitutapeli?
 
EMU na DMU zote hutumika zaidi kwemye city trains naona prof hajashauriwa vizuri.

EMU zinafungwa vichwa viwili na behewa kadhaa zinaungana kama mabus ya mwendokasi. Bado zinaenda kwa kasi hadi 150 KPH.
Kuna mchongoko mbele kunasaidia kupunguza matumizi ya nishati husika(umeme au Diesel). Bado tutataka vichwa na mabehewa tuliyoonyeshwa na sio hivi vya sasa
 
Waziri wa Uchukuzi Prof Mbarawa amewataka Wananchi kutochanganya Treni hii ya Tanzania na zile za high speed zenye vichwa vilivyochongoka

Prof Mbarawa amesema picha zinazorushwa mitandaoni na watu wasio na nia njema ni zile za high speed zinazotembea zaidi ya km 200 kwa saa

Za kwetu ni hizi mnazoona tunazipokea na haya ni Mabehewa 14 ya Daraja la tatu( economy) na mwezi February mwakani tutapokea Ya Business class na First class

Mabehewa haya ni kwa ajili ya masafa marefu na yatavutwa na Vichwa vya Umeme lakini yale ya high speed Vichwa vyake vinaunganishwa direct na mabehewa, amesisitiza Mbarawa

Source ITV Habari
Hi nchi Ngumu sanaaa


R.I. P JPM mzalendo wa kweli
 
Sasa kwanza mjue hivyo vichwa vitavyokuja mtaambiwa vina mifumo miwili yaani umeme na mafuta, kwahiyo kwakuwa kuna matengenezo makubwa ya umeme wa uhakika ina maana watatumia mafuta hapo miaka inasogea, wakikaribia uchaguzi italetwa treni tena nyingine ya kuzugia hadi Moro ya umeme itaenda kwa ajili ya kampeni halafu mkiingia kingi kuwapa kura za kishindo story inaishia hapo.
 
Back
Top Bottom