TANZIA Prof. Mathew Luhanga, aliyekuwa Makamu Mkuu wa UDSM kuanzia 1991 hadi 2006 afariki dunia

Michewen

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
24,560
32,202
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye anasikitika kutangaza kifo cha PROF. MATTHEW LUHANGA, aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia 1991 hadi 2006, kilichotokea jioni ya leo tarehe 16.09. 2021. Tunatoa pole kwa familia, Chuo chetu na Tanzania kwa ujumla. Taarifa zaidi tutaendelea kujulishana. Tumwombee apumzike kwa Amani. Amina.

Dkt. Dotto P. Kuhenga, Mratibu wa Mawasiliano na Habari, UDSM.

Profesa Matthew Luhanga alikuwa ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe.

20210916_221248.jpg

Luhanga.jpg

=======

Professor Matthew Luhanga ndie Mwanasayansi wa Zama hizi mwenye historia iliyotukuka duniani
 
Professor Matthew Luhanga ndie Mwanasayansi wa Zama hizi mwenye historia iliyotukuka duniani
Hajatokea wa kufananishwa nae. Ndio alihakikisha TTCL college Kijitonyama iwe sehemu ya UDSM (akiwa Mwenyekiti wa Bodi TTCL) na ndio hii inaitwa CoICT vijana wanapata maarifa kwa viwango vya kimataifa hapa hapa si nchini tu Bali ulimwenguni Ile ITP inatajwa Kama reform kubwa kwa Elimu ya juu duniani .

Professor wa kweli alieacha legacy katika Uongozi wa vyuo vikuu.
**Wanataaluma mna mengi ya kuiga kutoka kwa Professor Luhanga. Yaani Kuna Viprofesa ukiviangalia havimfikii huyu jamaa hata robo.
 
Profesa Mathew Luhanga, aliyewahi kuwa makamu mkuu wa chuo UDSM afariki dunia

tutamkumbuka msomi huyu kwa kubobea katika telecommunications, linguistics and environmental engineering!
“Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.”
— Ufunuo wa Yohana 14:13 (Biblia Takatifu)
 
Back
Top Bottom