Prof. Lipumba arejea nchini

Prof. Lipumba arejea nchini

Hakubalina na UKAWA, hivyo anakubaliana na ccm!!!
 
kaka ametega muda mzuri sana, hakuna kipindi ana thamani kama hiki, kikipita basi.......nani wa kutoa baada ya 25th
 
Thamani yake mpaka sasa ni TSHS 5.1bn alizopokea akiwa Kigali kutoka kwa rafiki wa familia ya Kikwete.
 
Harakati zote za Ukombozi huambatana na mamluki, wasaliti nk ,: wakati huu ni wakati wa mapambano haitakiwi kuhangaika na wanao rudi nyuma

Kumbe alisafiri?....manake alivyo kosa MVUTOoo.......hajulikani alipo.
 
Prof. alishajijengea utaratibu wa kutukana mafisadi, na alishamwambia Lowassa ' hufai kugombea uraisi unatakiwa uwe jela''..
 
Huyo ni Prof ana uwezo wa kuishi nchi yoyote na kufanyakazi pahala popote dunia na ana heshima yake zaidi ya siasa uchwara za tanzania


but ndoto yake kuu ni kua rais wa jamuhuri yetu hio ndoto imeota mbawa. Usipotimiza ndoto yako technically u ar a senior looser
 
Sisi Wtz tuna matatizo. Unamkebehi lipumba unamshangilia fisadi lowassa?

Ata wewe una matatizo mana katika List ya mafisad ata mkuu wa nchi yumo na mgombea urais wa CCM pia yumo lakini unawashangilia hao unambeza Lowassa.

Uwe mkweli tu, lowassa alipojiunga na ukawa umeumia sana na ni pigo kwa ccm hiyo ndio reality

Ata prof. lipumba ameumia kwa kuja mtu siku 2 tu akaweza kubeba dhamana kubwa na kuikosa yeye dhamana hiyo kwa vile amekitumikia chama kwa mda mwingwi huu ndio ukweli.
 
Huyo Prof wa kweli maana ameweza on hatari iliyopo mbele ya Ukawa, kaona bora ajiweke kando kuliko kuidhalilisha taaluma yake kwa tamaa ya wachache, hivyo bado naona kabisa bado vyama vya upinzani hawajawa tayari kushika dola, na watazidi kuishika kwa hisia tu mpaka atapo kuwa tayari kwa kuweka wazalendo wenye nia na dhamila ya kweli na si dhamila iliyobebwa na mengine nyuma ya pazia, hongera prof. I.Lipumba na wengine wote waliona hatari kabla ya hatari

Je bado ana nia ya kuitoa CCM madarakani? Msimamo wake ni UPI sasa?
 
Lipumba kweli watu wameshamchoka hakuna mtu alienda kumpokea hata wanafiki wenzake wamemsusia ?
 
Amefuata Nini?Huwezi Kufanya Utafiti Kwa Wiki Moja Ukiwa Sheraton.Hastahili Hata Kuitwa Profesa
 
Mbona hawajamuuliza alikuwa anafanya nini na yule "kijana wa Kikwete"?
 
Mnakomboa nini?

Ukiisoma historia ya Ulutheri utakuta kuwa neno kujikomboa na mageuzi kutoka Vatikan lilitumika sana kuonesha kama vile wanadhalilishwa na Kanisa Katoliki lakini ilikuwa ni uchu tu wa madaraka.

Hilo neno halitumiki kwa bahati mbaya ni mfumo kamili na wanaelewa kwanini wanalitumia.

Chama kikubwa na wafadhili wakubwa wa chadomo ni cha Kidemokrasia cha Ujerumani CDU (Walutheri).

Lowassa? Kaskazini?

Jiulize, Slaa yuko wapi? Na kwanini?
 
hana ishu huyo! hata asiporudi poa tu!
bora tuendelee kumwomba Dr. slaa arejee kazini kuliko kupoteza muda kumzungumzia Lipumba
 
Ujinga hauna mwenyewe. Hata prefesa anaweza kuwa mjinga.Watu vigeu geu ni hatari sana katika jamii. Jamaa hata aibu hana. Yaani kashiriki katika ngazi zote kumleta Lowassa halafu anawaruka wenzake mchana kweupe! Amenikatisha tamaa hata kusoma mpaka nifikie uprofesa maana sioni tofauti tena hata profesa Maji marefu naona ana nafuu kabisa!
 
Back
Top Bottom