Prof. Lipumba arejea nchini

Prof. Lipumba arejea nchini

Kwenye vita,askari akifa wenzake ndo morari onaongezeka. Tusonge mbele tusirudi nyuma,mapambazuko yako karibu sana.
 
Alifikiri atakuwa na impact kama lowasa alivyo ondoka ccm inakufa .ukawa ipo imara nasema naendee tuu.
 
Wenye CUF yao wamemshitukia mapema, jamaa alitaka kuendelea kuvi-install vi-particles vya udini ndani ya UKAWA.

Tutashuhudia mengi wakati MBUYU ukielekea kuanguka!!
 
aibu yake aibu yetu?...aibu yake mwenyeweeeeeee....
 
Jana jioni nilileta uzi hapa kuwa Prof Lipumba arejea nchini..nilisema nilikuwa mmoja wa watu waliopanda ndege ya Shirika la RwandAir toka Kigali kuja Dsm,ndege aina ya CRJ900,Flight number WB442 yenye usajili wa 9XR-WI...ilifika hapa Dsm majira ya Saa 15:50 alasiri.

Katika kushuka kwenye ndege Profesa alikuwa ameandaliwa gari la VIP,niliona lina maandishi yameandikwa Swissport,lkn cha kushangaza Prof alikataa kupanda na kuamua kupanda basi la abiria wa kawaida,ukiingalia hata hii picha utaona anatoka nje kupitia geti la abiria wanaowasili la watu wa kawaida na si watu mashuhuri au "VIP"
@Moderators wakaufutilia mbali uzi wangu bila hata huruma...lkn nilikuwa nasema habari nilizokuwa na uhakika nazo,nashukuru mleta picha umethibitisha kuwa mimi sikuwa muongo
Cc😡Invisible mtoto wa Peramiho Major kwa baba Titus Amigu

ImageUploadedByJamiiForums1439539000.892747.jpg
 
lipumba.jpg
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Rwanda jana. Picha na Said Khamis

Kwa ufupi

Asisitiza kutokubaliana na uamuzi wa Ukawa kumsimamisha Lowassa kugombea urais.

By Goodluck Eliona, MwananchiDar es Salaam. Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba alirejea nchini jana jioni akitokea Kigali, Rwanda alikokwenda mara tu baada ya kujiuzulu wadhifa huo siku nane zilizopita.

Profesa Lipumba aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) saa 10.10 jioni kwa ndege ya Rwanda Air.

Akihojiwa na Azam Tv kwa simu akiwa Kigali, siku tatu baada ya kuondoka nchini, Profesa Lipumba alisema alikuwa nchini humo akifanya utafiti kuona namna gani Tanzania inaweza kujifunza mambo ya kiuchumi kutokana na nchi hiyo kupiga hatua kubwa katika sekta hiyo.

Alipoulizwa jana, Profesa Lipumba alisema akiwa huko alikuwa na mazungumzo na Bodi ya Maendeleo ya Rwanda (RDB), wadau wa masuala ya rushwa, waziri wa fedha wa nchi hiyo na makamu mwenyekiti wa Bodi ya Utawala.

"Wenzetu wamepiga hatua kubwa katika kukuza uchumi ndani ya kipindi kifupi, hivyo safari yangu ilikuwa ya kujifunza mbinu walizotumia kufikia malengo yao," alisema.

Akizungumzia hatima yake kisiasa, licha ya kusema ataendelea kuwa mwanachama wa CUF, alisema hatashiriki kufanya kampeni kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa kuwa umoja huo umemsimamisha mwanachana wa CCM, Edward Lowassa.

"Kisiasa hatima yangu ni kama ya Mtanzania mwingine yeyote, Ukawa tuna mgombea kutoka CCM, amehama juzi tu, pia mle ndani ya Bunge la Katiba hakuunga mkongo Rasimu ya Katiba na ndiyo maana nikasema dhamira yangu inanisuta," alisema Profesa Lipumba.

Alisema wanachama wa CUF hawana sababu ya kuona kama amewaacha kwa kuwa bado yupo nchini.

Awali, akitangaza kujiuzulu, nguli huyo wa uchumi, alisema alifikia uamuzi huo kutokana na Ukawa kumkaribisha Lowassa kugombea urais kupitia umoja huo, hivyo dhamira yake inamsuta.


Chanzo;
Mwananchi

 
Back
Top Bottom