BOWTHRUSTER
JF-Expert Member
- Aug 1, 2014
- 397
- 175
njaa za Lipumba .[/QUOTE]
Lipumba hana njaa mkuu.Sio professor magumashi kama unavyodhani.
Lipumba hana njaa mkuu.Sio professor magumashi kama unavyodhani.
Sawasawa mkuu Izzo.Tatizo la Chadema bado wanajiaminisha wapo juu ilhali tayari ishakuwa CDM nyingine ndembendembe.Chadema ya leo sio ya 2000 wakae wakilijua.Wakubali wakatae Zitto kawamega sana.
Chadema ni wadini na Wana ukabila ndio maana Lipumba kasepa.
Lipumba atawaboa watu kwa kuwa wa kwanza kwenda mpongez amagufuli kabla goli la mkono la Nape halijaingia
Chadema inawatumia cuf na nccr kama condom,hongera sana Lipumba kwa kushtukia mapema
... Nyie Hamjaelewa. Tatizo Siyo Lipumba, Ni Uongozi Wa Cuf Na Wanachama Wake. Labda Lipumba Anajificha Huko.
UKAWA Kama mnataka kushinda teueni mgombea "mpya" hawa kina lipumba na slaa piga chini. Hawakubaliki kiivo kama mnavowapamba.
Chadema ni wadini na Wana ukabila ndio maana Lipumba kasepa.
Chadema inawatumia cuf na nccr kama condom,hongera sana Lipumba kwa kushtukia mapema
Prof. Ibrahimu Haruna Lipumba yaelekea anaweza akavuruga kabisa kambi ya UKAWA na hivo kuisambaratisha ngome ya UKAWA kutokana na tamaa ya Madaraka iliyopitiliza ya kutaka kuwa Rais.
Tangu kuanzishwa kwa mfumo wa Vyama vingi huyu jamaa amekuwa kigombea kila baada ya miaka 5(1995,2000,2005 na 2010) na sasa kwa kupitia UKAWA analazimisha tena ateuliwe kama mgombea Urais kwa tiketi ya UKAWA!
Kwa mtu msomi kwa kiwango cha Uprofesa sikutegemea kabisa akomae na kutaka kuteuliwa awe mgombea wa Urais kwa mwaka huu. Ikumbukwe kuwa katika umoja wa UKAWA kuna makubaliano ya kuachiana majimbo na hili liko wazi na linakubalika. Kitu ambacho sielewi kuhusu Prof. Lipumba na CUF kwa ujumla kwanini hili la kuachiana ugombea wa URAIS wanashindwa kuliona.
Tayari CUF wamepitisha Jina la Maalim Sharrif Hamad kuwa mgombea wa Urais kwa tiketi ya CUF huko Visiwani. Ni jambo lili dhahiri basi CUF wangewaachia wenzao wa vyama vungine vya UKAWA kwa TANZANIA BARA ili wapendekeze jina toka aidha CHADEMA,NCCR au NLD. Haiwezekani CUF peke yao wachukue nafasi za kugombea Uraisi kwa BARA na VISIWANI. Hili halikubaliki asilani.
Lakini hata kama CUF wasingekuwa na mgombea wa Urais Visiwani, bado ilitakiwa busara ya hali ya juu katika kuteua jina la mgombea wa UKAWA. Kila Mtanzania anajua kuwa mwaka 2010 mgombea aliyeng'ara vizuri kiasi cha kutishia Urais wa Rais Kikwete alikuwa ni Dr. W.P.Slaa na alimwacha Lipumba kwa mbali sana.Ili UKAWA washinde Urais ni LAZIMA WAWEKE MTU ANAYEKUBALIKA NDANI YA UKAWA NA NJE YA UKAWA kwa maana ya Watanzania.
Kitendo cha Prof. Lipumba kutaka kung'ang'ania kuteuliwa na UKAWA ili apeperushe bendera kwenye nafasi ya Urais Bara lazima kikemewe na kilaaniwe kwa nguvu zote na Watanzaniua wote wanaotaka mabadiliko.Urais hauji kwa kulazimisha na Waswahili walilonga kuwa CHEMA CHAJIUZA KIBAYA CHAJITEMBEZA.
Chonde chonde Prof. Lipumba na CUF yako tuwakuomba mruhusu mchakato wa kumpata mgombea wa UKAWA kwa maridhiano na si mwingine baali Dr.Slaa, huyu atakuwa ni zaidi ya Pombe Magufuli.
Lipumba haoni mbali...pengine ni makosa ya kichama waliyofanya CUF walipotengeneza uomja wa kitaifa Zenj,wakamwachia Lipumba CUF ktk vast country Tanganyika huku wakiwa hawana ushiwishi tena..huku wakiwa na misimanagement of little fund they had.Kitu kilichopelekea Lipumba kuanza fikiria jinsi ya kupata dili la kutangaza nae huku Bara km mwenzie huko visiwani.Bahati mbaya anaingia mara zote akiwa ng`ombe alaiyekonda ktk kipindi CCM ikiwa na headache CDM.KWa data zilizopo CDM ina wanachama hai wengi kuliko CCM hat abila kutoa kura za Lowasa ambazo ni mamilioni ,na hata ukiacha kura za wazee ambao ni wengie na wameshakufa ktk CCM.CUF will never gain ground again km Lipumba na sera mbaya watabaki.CUF wanahitajia safisha nyumba yao kabisa na kuruhusu watu wapaya fikra mpya, na kufuta hisia za kidini zinazowauza kwa CCM.Hiyo ndiyo hofu yangu; kwamba hata kuwa kuna watu wanawazia Lipumba anaweza au anapaswa kugombea tena inashangaza. Utaweza vipi kumfanya aaminike kuwa hatohujumu tena Uchaguzi Mkuu na hatokuwa wa kwanza kama ulivyosema kukiri kushindwa hata kama mwelekeo wa kura hauendi hivyo kwa sababu tu hataki UKAWA ishinde dhidi ya CCM? Lakini utampitisha mtu vipi ambaye chama chake hakikuwa kikuu cha upinzani tangu 2010?