Prof. Lipumba akerwa na Zitto Mtwara

Prof. Lipumba akerwa na Zitto Mtwara

Chuki kwa ACT ni upuuzi wa mijitu isiyo fahamu maana pana ya demokrasia! Ni mijitu ya chadema ambayo inataka demokrasia isikue hapa Tanzania! Iacheni ACT kama itakataliwa na Watanzania ila sio wachawi kuipinga na kuichulia,kwani ninyi chadema uhalali wa kisiasa mnatoa wapi ACT wasiwe nao!???? Acheni ujinga wenu Chadema

Yan we wa ajabu kweli.... Chadema imeingiaje hapo??
 
Sala zenu chadema mnaomba kila siku vyama vyooote vya upinzani vife ili mpate madaraka. Chadema ni hatari kwa demokrasia ya kweli, naamini hata mkipata madaraka hamtakubali kupisha upinzani wa kweli kama ilivyowapa nafasi ccm mpaka mkajulikana. Chadema ni janga la demokrasia nchini.

Hata siku moja CCM haijawahi kuipa nafasi CHADEMA. Kamuulize wasira atakuambia. Ndoto yake ni chadema ife kabla ya 2014.
 
watanzania wengi si wafuatiliaji makini .escrow ilikuwa imdhalilishe zitto vibaya, anapaswa aheshimu utu wa wanachadema . alifanya hivyo ila akishakutana na wanafiki wakamsifia anasahau.mi naamini inalikuwa mbowe amebanwa vile zitto asingalimuokoa kwenye kamba. Imagine siku ya kwanza na yapili ya mjadala, angalilia kisi gani ,jama walivyokuwa mbogo .Mbowe akawa anawachomole document baada ya nyingine

Mh ... Wew umendika nin sasa mbowe anahusikaje katika kumuokoa ZITTO . ZITTO Alikuwa na TUHUMA gan hadi aokolewe na mbowe
Swala la kuchangia positively /negatively ni Ustashi wa mtu mwenyewe.
 
Zitto haishiwi waliokuwa hawamtambui sasa huyu ndio bwana Zitto Kabwe
 
Last edited by a moderator:
Mkuu,
Alichokifanya Lipumba ni sawa kabisa kuhoji juu ya uwepo wa chama cha ACT katika mkutano wake.

Lipumba alitambua, atapeleka picha mbaya kwa washirika wake wa UKAWA. Kama wangeona ushiriki wa ACT na siyo CHADEMA wala NCCR.

Ni kitu cha ajabu kwa Lipumba, kwa nini hakuwaalika washirika wake. Hatukuona bendera za NLD wala wana UKAWA.

Na Zitto alifanya jitihada sahihi kuwalipia hao wanachama, akitumaini awe na watu wake mapema ndani ya ACT. Kwa sababu uchaguzi mkuu ndani ya chama hicho.
yaa , here you are. lipumba kamaliza jambo kiungwana ,tofauti na hapo balaa ya ukawa ilikuwa inakuja
 
mtoa mada uko fasta umejiunga leo na leo hii umetumwagia mzigo wa zitto
 
Vijana wa chadema mnalipwa nin kumsakama ZITTO mbona yuko kimya nyie mnahangaika na njia

Sasa hizo TUHUMA zinaweza kuandikwa na mtu yeyote mwenye chuki na ZITTO maana hazina uthibitisho wowote .
Nyie ndo mtakao vuruga hata muungano wetu wa ukawa kwa kushinda kwenye mtandao mkipiga majungu badala Ya kuhangaika namna Ya kuidhoofisha CCM mnahangaika namna Ya kumdhoofisha ZITTO kwa juhudi zozote zile
Kesho na Kesho kutwa mtaanza tena na Lipumba kwa propaganda chafu hatimaye muungano wa ukawa unakufa.

Tangu lini ww ulikuwa UKAWA?
 
Sala zenu chadema mnaomba kila siku vyama vyooote vya upinzani vife ili mpate madaraka. Chadema ni hatari kwa demokrasia ya kweli, naamini hata mkipata madaraka hamtakubali kupisha upinzani wa kweli kama ilivyowapa nafasi ccm mpaka mkajulikana. Chadema ni janga la demokrasia nchini.

Wangejiunga na vyama vingine kuunda Ukawa?
 
Chadema hawakupenda Prof Lipumba kumwalika Zitto! Poor Chadema
 
Prof. Lipumba ambaye ni wenyekiti wa chama cha wananchi Cuf amekerwa na tabia isiyo ya kinidhamu wala staha iliyofanywa na mbunge wa kigoma kasikazini Bwana Zitto Kabwe,


Katika kikao cha dharula alichokiitisha usiku ule wa mkutano baada ya kumaliza kuhutubia, alitufokea viongozi wa Mtwara kuhusu alichokiona katika mkutano, alisema aliwaona wanachama wa ACT-Tanzania wakiwa na mavazi yao na bendera zao akahoji kwanini tuliwaalika wakaja wakiwa na bendera zao na kuzichomeka hewani?

Mmoja wetu aliinuka na kujibu vizuri kuwa wale vijana tuliwakamata baada ya kuwaona na bendera hizo katika viwanja vyetu, tulipotaka kuwapeleka polisi mmoja wao aliyejitambulisha kwa jina la Kaila alisema yeye ni afsa habari wa chama chao taifa,

Akadai kuwa walialikwa na zitto kuhudhuria mkutano ule,na wamekuja kwa gari lake alilowapatia waje nalo, ‘’Mh Mwenyekiti tunakuomba radhi sana kwa uliyoyaona pale uwanjani, wale vijana hatukuwaita sie, aliyewaleta toka dar es salaam ni swahiba wako uliyeongozana nae Zitto Kabwe, hata gari walilokuja nalo ni lake kawapatia’’

Lakini pia prof. lipumba alidai kuwa ‘’zitto hana heshima hata kidogo kwa sababu tumemwalika sisi katika jukwaa la chama chetu, amekosa jukwaa la kuhutubia siku nyingi, leo tumempa fadhila lakini ametufanyia vitimbi, amekodi mpaka waandishi wa habri wake bila hata kuniambia, kumbe hata wafuasi wake amewagharamikia waje wakiwa na bendera na mavazi ya chama kingine katika mkutano wetu”?alihoji Prof. Lipumba

‘Mbona asitumie jukwaa la hicho chama cha wapambe wake? ikiwa ana unafiki wa namana hii basi hafai kupewa hifadhi kabisa’ alimalizia Prof. Lipumba

Tarehe 31/12/2014 chama cha wananchi cuf kilifanya mkutano wake katika viwanja vya mashujaa hapa mjini Mtwara ambapo zitto kabwe alikuwa mgeni mwalikwa, pia watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa zitto walivamia mkutano huo wakiwa na bendera na mashati yenye chama kingine ambacho hakikuwa na makubaliano ya kufanya mkutano pamoja na cuf..

Weka picha yenye tarehe sio mbwela tu.
 
Mtahangaika sana kumchafua zitto na mada za kijinga zisizokuwa na kichwa wala miguu kama hii lakin zzk anangozi ngumu na kamwe hamumuweziZitto

Hivi visifa vya watoto wa shule ya msingi ndivyo vinavyomharibiaga Zitto akisoma mitandaoni
 
Last edited by a moderator:
VIOL. SHULE ULIYOSOMA inatakiwa ifungwe NA MWALIMU ALIYEKUFUNDISHA aachishwe kazi. Kama una watoto ni hasara na wewe mwenyewe ni hasara kwa taifa. Huwezi Generalize kwa sababu ya mtu mmoja.
KASOME SAIKOLOJIA YA MAKUZI YA MTOTO labda unaweza kuelewa kidogo.

Imekuingia lakini Voil kasema ukweli kwa wakati mwafaka
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom