Nasakadoo
JF-Expert Member
- Sep 18, 2014
- 343
- 169
Uongo Mtakatifu
Maana yake ukweli
Uongo Mtakatifu
Huyu bwana ni hatari na afadhali ametoka CDM mapema kwani tangu mwanzo nilishaona angeleta matatizo cdm. Pia siasa za udini zinatamalaki Tz kwa sasa inavyoonekana na Zito anataka kuinuka kwa kutumia udini zaidi, ili atashindwa vibaya kwa hilo[/ZITO KABWE NI MCHOCHEZI; SERIKALI ISIMNYAMAZIE
Zito ni mchochezi kama wachochezi wa uasi kwa Serikali kabisaa na ni kwa makusudi haya amekwenda kuyasemea Mtwara na Lindi ambako anajua ni rahisi kutibua nyongo zao na kuibua hasira dhidi ya Serikali wakati akijua anasema uongo. Inashangaza kabisa kwamba Serikali inaumacha aendelee kuichonganisha na wananchi.
Kudhihirisha kwamba Zito ni mchochezi, kwenye Ripoti yake ya PAC iliyopo kwenye tovuti ya Bunge la Tanzania, ukurasa wa 21 inakiri kwamba fedha waliyolipwa PAP ni Sh. 203.1billioni na kwamba fedha iliyotakiwa kuwa kwenye Escrow Account ni Sh. 306,675,081,939/=
Kumbe inaelekea hiki ndicho Zito na wapinzani hata waliomo ndani ya CCM walichokuwa wakiogopa kisijulikane pale Rais alipoagiza Ripoti ya CAG iwekwe wazi wananchi tuisome. Pamoja na Rais kutolea ufafanuzi suala hilo bado Zito anaendelea na upotoshaji! Maadili tu ya kawaida ya ki-Afrika hayaruhusu hili kutokea. Hii inatia mashaka hata malezi na makuzi ya Zito.
Lakini kwa makusudi kabisa na kwa kuongozwa na nia ya uchochezi ukurasa wa 47 Maoni na Mapendekezo ya Kamati, Ripoti ya PAC umetumia maneno makali ya uchochezi tofauti na ukweli waliouandika wenyewe ukurasa wa 21, ninanukuu "Mfumo mzima wa Serikali ulipata ganzi au uliganzishwa ili kuwezesha zaidi ya shilingi bilioni 306 kuporwa kutoka Benki Kuu ya Tanzania na kutakatishwa kupitia benki mbili hapa nchini"
Kwa mtu yeyote mwenye akili ya kawaida tu, atagundua kwamba kubadilisha matumizi ya neno "iliyolipwa" ukurasa wa 21 kuwa "kuporwa" ukurasa wa 47 na kuamua kutumia kiasi cha fedha ambazo hazikuwemo kwenye Escrow Account, ni mbinu ya kufanya propaganda ya uchochezi.
Zito, alitumia wadhifa wake kama M/Kiti wa PAC vibaya na labda kwa kuhongwa au kuingia kwenye dili chafu ya Standard Chartered Bank iliyotaka kinyemela kuiba fedha za IPTL kwenye Escrow Account kwa kutumiwa na Mkono.
PAC kutolea maamuzi ya uhalali wa SCB wakati kesi ziko mahakamani na kumuandama Mh. Masele, Naibu Waziri wa Nishati na Nadini kwa kumkemea Balozi wa Uingereza kutojiingiza kwenye mambo ya Wizara yake, ni ushahidi tosha kwamba Zito, alikuwa anaongozwa na dhamira ovu na maslahi binafsi, hakutumia hata chembe ya busara. PAC lini imekuwa juu ya Mahakama? Na je, Mh. Masele ni kosa lipi alilokuwa amelifanya kwa kumkumbusha Balozi wa Uingereza kuheshimu mipaka yake ya kazi?
Ni vyema kabisa Serikali ikamuangalia vizuri na kudhibiti hila zake chafu ambazo ziko dhahiri kabisa. Bunge linapaswa kuiangalia kwa makini Kamati ya PAC kwa ilichokifanya kuleta taharuki isiyokuwa na sababu kutokana na uzushi wa Zito. Huyu ni mtu hatari kama Hitla, asipodhibitiwa ataliangamiza taifa.
Tufikirie kwa makini, Zito leo hii ni Mbunge wa mahakama, kwa nini ametengwa na chama chake? Na kama siyo mahakama, basi leo Zito asingelikuwa mbunge CHADEMA waliishamvua nyadhifa zote, ilibaki tu afukuzwe. Hivi kweli huyu ni mtu anayestahili kuaminiwa? Tuache mzaha, Zito hafai katika jamii ya watu Wastaarabu ni mzushi, mchochezi na msaliti.
HII ILIKUA BAADA YA MKUTANO View attachment 216352HII ILIKUA BAADA YA MKUTANO
Mh ZITTO KABWE akijadiliana jambo na Prof Lipumba Mara tu Baada ya kumalizika Mkutano Wa MTWARA .
Sijaona dhalili za Utovu aw Nidhamu Kama ilivyopostiwa kwenye baadhi ya Mitandao ya Kijamii.
Kushoto kwako msomaji ni Muandishi wa Habari Ezekiel Kamwaga