Prof. Lipumba akerwa na Zitto Mtwara

Prof. Lipumba akerwa na Zitto Mtwara

Though we need reliable source of Info
 
Tuwekeeni picha ya mkutano inayowaonesha wafuasi wa ACT kwenye mkutano huo wa CUF Mtwara. Asanteni
 
narudia kusema tena tuwe na subira kidogo Zito akikua ataacha mambo ya kitoto
 
Chuki kwa ACT ni upuuzi wa mijitu isiyo fahamu maana pana ya demokrasia! Ni mijitu ya chadema ambayo inataka demokrasia isikue hapa Tanzania! Iacheni ACT kama itakataliwa na Watanzania ila sio wachawi kuipinga na kuichulia,kwani ninyi chadema uhalali wa kisiasa mnatoa wapi ACT wasiwe nao!???? Acheni ujinga wenu Chadema

kuwa na utitiri wa vyama hakumaanishi kukua kwa demsrasia, ni ishara ya uchu wa madaraka. vyama vinne vinatosha kuwepo na kushiriki chaguz mbalimbali.

wingi wa vyama vya siasa ni kuchelewesha mabadiliko ya kiutawala maana ccm ananufaika na vyama utitiri.
 
Nilishasema, ZZK nje ya CHADEMA ni kama chui wa karatasi. Hapo alipo yuko kwenye dilemma kuhusu future yake kisiasa. Kama ni mwanaume kweli mbona bado anashindwa kujitokeza hadharani na ACT yake?
Ni ajabu hata hao CUF kumpa platform. Zito ni msaliti wa MAGEUZI CAUSE. Haiwezekani wote tuko kwenye mashua baharini halafu mwenzetu anaanza kuutoboa. Kwa ujumla wetu tutapambana naye kumzuia na kama anaendelea uamuzi muafaka ni kumtosa baharini na kutuacha sisi tuendelee na safari Yetu.
amezidi kujianika.

Kwenye ESROW AKAGEUKA SHUJAA WENU SIYO??

AKILI ZA NGUCHIRO HIZI
 
Japo habari hii ni ya kupika
lakini kama CUF walitaka kumtumia Zitto Kisiasa, halafu hawataki Zitto awatumie Kisiasa basi ni wachoyo!
Hata hivyo, Zitto kazi zake ndani ya bunge ndizo zinazompa heshima mbele ya umma, na si mikutano hii ya kualikwa!
 
Niliona kiburi na dharau yake pale alipokuwa anasalimiana na Lipumba huku hajachomeka shati,Baadae anahutubia hajavaa mkanda,ile ni jeuri tu ya kitoto. Ana marafiki wengi wa face book watoto wa f2,3,4 nae yupo hivo.Akasema mbowe akiniomba nitamsaidia issue ya bomba la gesi. Hivi yeye alimuomba mbowe amsaide issue ya escrow na ripoti yake nyepesi.Huyo ndie litaka uraisi na uenyekiti wa chama kubwa
Zitto anawafanya watanzania kama watoto wewe unakuja na report nyepesi then hapa anasema ati akiombwa kwenye maslai ya taifa anahitaji kuombwa huu ni Upuuzi
 
Last edited by a moderator:
Chuki kwa ACT ni upuuzi wa mijitu isiyo fahamu maana pana ya demokrasia! Ni mijitu ya chadema ambayo inataka demokrasia isikue hapa Tanzania! Iacheni ACT kama itakataliwa na Watanzania ila sio wachawi kuipinga na kuichulia,kwani ninyi chadema uhalali wa kisiasa mnatoa wapi ACT wasiwe nao!???? Acheni ujinga wenu Chadema
Kasema Lipumba, unawachukia CHADEMA! Consult the doctor.
 
Zitto atajwa bosi wa ACT

CHAMA cha Mabadiliko na Uwazi (ACT), kimetangaza rasmi kuwa muasisi wa chama hicho ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema), ambaye kwa sasa bado anatambulika kuwa mwanachama wa Chadema.

Siri hiyo iliwekwa hadharani jana na Makamu Mwenyekiti wa ACT, Shabani Mambo, wakati akinadi kwa wananchi wagombea wa uenyeviti wa serikali za mitaa kupitia chama hicho kipya, katika mitaa ya Majengo pamoja na Nyasubi katika uwanja wa Lumambo.

Kutokana na kauli hiyo, gazeti hili lilimtafuta Zitto atoe ufafanuzi, ambapo alikataa kukiri wala kukanusha madai hayo ya ACT.

Hii si mara ya kwanza kwa Zitto kuhusishwa na chama hicho, ambapo Mei mwaka huu alipohojiwa na kituo cha redio cha Clouds Fm, kiongozi huyo kijana wa Chadema alikaririwa akisema hawezi kukubali au kukanusha kuwa mwanachama wa ACT, mpaka hapo kesi ya msingi dhidi ya uanachama wake Chadema itakapotolewa uamuzi mahakamani.

Aliulizwa swali hilo, baada ya kiongozi ambaye alitimuliwa Chadema pamoja na Zitto, Profesa Kitila Mkumbo, kumtaka rafiki yake Zitto kuhamia ACT na kugombea nafasi ya uenyekiti.

Profesa Mkumbo katika maoni yake kwa Zitto, alikaririwa akisema kiongozi huyo kijana hawezi kupata mafanikio zaidi ya kisiasa ndani ya Chadema, isipokuwa kama ataamua kuhama chama hicho.

Zitto alipohojiwa na Clouds kuhusu kauli ya Profesa Mkumbo, alisema yeye na Profesa Mkumbo wana mrengo wa siasa unaofanana, unaoamini katika maendeleo na maslahi ya jamii kwa ujumla na sio chama wala watu wachache.

Kampeni

Akiendelea na kampeni baada ya kueleza kuwa bosi wao ni Zitto, Mambo alidai watumishi wa Serikali iliyopo madarakani, wamekuwa na jeuri ya fedha kuliko wafanyabiashara hata kama wana mishahara midogo na kuongeza kuwa hali hiyo inatokana na ubadhirifu uliopo katika sehemu zao za kazi.

“Unakuta mfanyakazi mdogo wa halmashauri lakini unakuta anamiliki mali nyingi na huku mshahara wake ukiwa ni mdogo, ukiambiwa unaweza kushangaa hata mfanyabiashara mkubwa anaweza kutokuwa nazo sasa hebu fikiri mtu huyu anatoa wapi fedha hizo?” Alihoji.

Katika Mkutano huo Makamu Mwenyekiti huyo aliwanadi wagombea uenyekiti kupitia ACT kutoka katika ya Majengo Kati, Ali Shango pamoja na mgombea mwingine wa Mtaa wa Nyasubi, Idsam Mapande na kuongeza kuwa chama hicho ambacho ni kipya kimejipanga kuhakikisha kuwa kinashinda viti hivyo
 
Sasa Mkuu Chadema wamwameingiaje hapa? Hicho Kilicho andikwa ni uongo? Tujielekeze kwenye hoja na tusifiche udhaifu wetu kwa kusingizia watu

Sala zenu chadema mnaomba kila siku vyama vyooote vya upinzani vife ili mpate madaraka. Chadema ni hatari kwa demokrasia ya kweli, naamini hata mkipata madaraka hamtakubali kupisha upinzani wa kweli kama ilivyowapa nafasi ccm mpaka mkajulikana. Chadema ni janga la demokrasia nchini.
 
No wonder CCM itaendelea kutawala kwa miongo kadhaa.

Weka na chanzo cha habari yako mkuu isije kuwa yaleyale mambo ya uchonganishi tu.
 
watanzania wengi si wafuatiliaji makini .escrow ilikuwa imdhalilishe zitto vibaya, anapaswa aheshimu utu wa wanachadema . alifanya hivyo ila akishakutana na wanafiki wakamsifia anasahau.mi naamini inalikuwa mbowe amebanwa vile zitto asingalimuokoa kwenye kamba. Imagine siku ya kwanza na yapili ya mjadala, angalilia kisi gani ,jama walivyokuwa mbogo .Mbowe akawa anawachomole document baada ya nyingine
 
kuna mtu aliniambia tender ya kusupply matairi kwn magari ya tanescrow nchi nzima ni yake. hapo nilitaman kuzimia
 
Mi nafikiri Zito ameishapevuka kisiasa kwanin asianzishe himaya yake mwenyewe?.aondokane na kubebwa na wanasiasa wengine watamtia madoa kila siku
 
Japo habari hii ni ya kupika
lakini kama CUF walitaka kumtumia Zitto Kisiasa, halafu hawataki Zitto awatumie Kisiasa basi ni wachoyo!
Hata hivyo, Zitto kazi zake ndani ya bunge ndizo zinazompa heshima mbele ya umma, na si mikutano hii ya kualikwa!

Acha uongo mkuu, CUF hawahitaji msaada wanapokuwa mtwara ile ni ngome yao ni sawa Na Ccm Dodoma au Cdm Arusha moshi, mwanza na shinyanga.Professor alitaka kuleta suluhu ndani ya upinzani kwa kuutambua ukweli kwamba zitto amekuwa Yatima kisiasa.Kizuri kilichojitokeza ni kwamba prof .ameupata ukweli wa kwa nini CDM hawataki kusikia kitu Zitto.prof sasa amepata ile eye witnessed evidence
 
Mtahangaika sana kumchafua zitto na mada za kijinga zisizokuwa na kichwa wala miguu kama hii lakin zzk anangozi ngumu na kamwe hamumuweziZitto
Prof. Lipumba akerwa na Zitto Mtwara.
Prof. Lipumba ambaye ni wenyekiti wa chama cha wananchi Cuf amekerwa na tabia isiyo ya kinidhamu wala staha iliyofanywa na mbunge wa kigoma kasikazini Bwana Zitto Kabwe,

Katika kikao cha dharula alichokiitisha usiku ule wa mkutano baada ya kumaliza kuhutubia, alitufokea viongozi wa Mtwara kuhusu alichokiona katika mkutano, alisema aliwaona wanachama wa ACT-Tanzania wakiwa na mavazi yao na bendera zao akahoji kwanini tuliwaalika wakaja wakiwa na bendera zao na kuzichomeka hewani?

Mmoja wetu aliinuka na kujibu vizuri kuwa wale vijana tuliwakamata baada ya kuwaona na bendera hizo katika viwanja vyetu, tulipotaka kuwapeleka polisi mmoja wao aliyejitambulisha kwa jina la Kaila alisema yeye ni afsa habari wa chama chao taifa,

Akadai kuwa walialikwa na zitto kuhudhuria mkutano ule,na wamekuja kwa gari lake alilowapatia waje nalo, ‘’Mh Mwenyekiti tunakuomba radhi sana kwa uliyoyaona pale uwanjani, wale vijana hatukuwaita sie, aliyewaleta toka dar es salaam ni swahiba wako uliyeongozana nae Zitto Kabwe, hata gari walilokuja nalo ni lake kawapatia’’

Lakini pia prof. lipumba alidai kuwa ‘’zitto hana heshima hata kidogo kwa sababu tumemwalika sisi katika jukwaa la chama chetu, amekosa jukwaa la kuhutubia siku nyingi, leo tumempa fadhila lakini ametufanyia vitimbi, amekodi mpaka waandishi wa habri wake bila hata kuniambia, kumbe hata wafuasi wake amewagharamikia waje wakiwa na bendera na mavazi ya chama kingine katika mkutano wetu”?alihoji Prof. Lipumba

‘Mbona asitumie jukwaa la hicho chama cha wapambe wake? ikiwa ana unafiki wa namana hii basi hafai kupewa hifadhi kabisa’ alimalizia Prof. Lipumba

Tarehe 31/12/2014 chama cha wananchi cuf kilifanya mkutano wake katika viwanja vya mashujaa hapa mjini Mtwara ambapo zitto kabwe alikuwa mgeni mwalikwa, pia watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa zitto walivamia mkutano huo wakiwa na bendera na mashati yenye chama kingine ambacho hakikuwa na makubaliano ya kufanya mkutano pamoja na cuf..
 
siasa haina kupevuka ,mtu ndie anapevuka kisha anamudu kuishi na watu
 
Back
Top Bottom