Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 5,807
- 12,216
Prof. Lipumba ambaye ni wenyekiti wa chama cha wananchi Cuf amekerwa na tabia isiyo ya kinidhamu wala staha iliyofanywa na mbunge wa kigoma kasikazini Bwana Zitto Kabwe,
Katika kikao cha dharula alichokiitisha usiku ule wa mkutano baada ya kumaliza kuhutubia, alitufokea viongozi wa Mtwara kuhusu alichokiona katika mkutano, alisema aliwaona wanachama wa ACT-Tanzania wakiwa na mavazi yao na bendera zao akahoji kwanini tuliwaalika wakaja wakiwa na bendera zao na kuzichomeka hewani?
Mmoja wetu aliinuka na kujibu vizuri kuwa wale vijana tuliwakamata baada ya kuwaona na bendera hizo katika viwanja vyetu, tulipotaka kuwapeleka polisi mmoja wao aliyejitambulisha kwa jina la Kaila alisema yeye ni afsa habari wa chama chao taifa,
Akadai kuwa walialikwa na zitto kuhudhuria mkutano ule,na wamekuja kwa gari lake alilowapatia waje nalo, Mh Mwenyekiti tunakuomba radhi sana kwa uliyoyaona pale uwanjani, wale vijana hatukuwaita sie, aliyewaleta toka dar es salaam ni swahiba wako uliyeongozana nae Zitto Kabwe, hata gari walilokuja nalo ni lake kawapatia
Lakini pia prof. lipumba alidai kuwa zitto hana heshima hata kidogo kwa sababu tumemwalika sisi katika jukwaa la chama chetu, amekosa jukwaa la kuhutubia siku nyingi, leo tumempa fadhila lakini ametufanyia vitimbi, amekodi mpaka waandishi wa habri wake bila hata kuniambia, kumbe hata wafuasi wake amewagharamikia waje wakiwa na bendera na mavazi ya chama kingine katika mkutano wetu?alihoji Prof. Lipumba
Mbona asitumie jukwaa la hicho chama cha wapambe wake? ikiwa ana unafiki wa namana hii basi hafai kupewa hifadhi kabisa alimalizia Prof. Lipumba
Tarehe 31/12/2014 chama cha wananchi cuf kilifanya mkutano wake katika viwanja vya mashujaa hapa mjini Mtwara ambapo zitto kabwe alikuwa mgeni mwalikwa, pia watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa zitto walivamia mkutano huo wakiwa na bendera na mashati yenye chama kingine ambacho hakikuwa na makubaliano ya kufanya mkutano pamoja na cuf..
una VATAR ngapi mpaka sasa? maana hii umeifungua maalum kwa ajili hii.. halafu unajichangia maoni kujiunga mkono. kwa mtu mgeni asingeweza kuja na habar kama hii