Prof. Lipumba akerwa na Zitto Mtwara

Prof. Lipumba akerwa na Zitto Mtwara

Prof. Lipumba akerwa na Zitto Mtwara.
Prof. Lipumba ambaye ni wenyekiti wa chama cha wananchi Cuf amekerwa na tabia isiyo ya kinidhamu wala staha iliyofanywa na mbunge wa kigoma kasikazini Bwana Zitto Kabwe,


Katika kikao cha dharula alichokiitisha usiku ule wa mkutano baada ya kumaliza kuhutubia, alitufokea viongozi wa Mtwara kuhusu alichokiona katika mkutano, alisema aliwaona wanachama wa ACT-Tanzania wakiwa na mavazi yao na bendera zao akahoji kwanini tuliwaalika wakaja wakiwa na bendera zao na kuzichomeka hewani?


Mmoja wetu aliinuka na kujibu vizuri kuwa wale vijana tuliwakamata baada ya kuwaona na bendera hizo katika viwanja vyetu, tulipotaka kuwapeleka polisi mmoja wao aliyejitambulisha kwa jina la Kaila alisema yeye ni afsa habari wa chama chao taifa,


Akadai kuwa walialikwa na zitto kuhudhuria mkutano ule,na wamekuja kwa gari lake alilowapatia waje nalo, ‘’Mh Mwenyekiti tunakuomba radhi sana kwa uliyoyaona pale uwanjani, wale vijana hatukuwaita sie, aliyewaleta toka dar es salaam ni swahiba wako uliyeongozana nae Zitto Kabwe, hata gari walilokuja nalo ni lake kawapatia’’


Lakini pia prof. lipumba alidai kuwa ‘’zitto hana heshima hata kidogo kwa sababu tumemwalika sisi katika jukwaa la chama chetu, amekosa jukwaa la kuhutubia siku nyingi, leo tumempa fadhila lakini ametufanyia vitimbi, amekodi mpaka waandishi wa habri wake bila hata kuniambia, kumbe hata wafuasi wake amewagharamikia waje wakiwa na bendera na mavazi ya chama kingine katika mkutano wetu”?alihoji Prof. Lipumba


‘Mbona asitumie jukwaa la hicho chama cha wapambe wake? ikiwa ana unafiki wa namana hii basi hafai kupewa hifadhi kabisa’ alimalizia Prof. Lipumba


Tarehe 31/12/2014 chama cha wananchi cuf kilifanya mkutano wake katika viwanja vya mashujaa hapa mjini Mtwara ambapo zitto kabwe alikuwa mgeni mwalikwa, pia watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa zitto walivamia mkutano huo wakiwa na bendera na mashati yenye chama kingine ambacho hakikuwa na makubaliano ya kufanya mkutano pamoja na cuf..


Hii inaweza kuwa mbaya katika ustawi wake pale unapotamalaki kila kitu kiwe kwa kiasi
 
Nilidhani ZZK yupo makini hasa baada ya misukosuko katika safar yake ya kisiasa iliyompata kumbe bado utot na kutaka sifa binafsi kuamuandama

Fahari aachi asili jamaa yangu kama hata Prof kachemka basi.
 
Chuki kwa ACT ni upuuzi wa mijitu isiyo fahamu maana pana ya demokrasia! Ni mijitu ya chadema ambayo inataka demokrasia isikue hapa Tanzania! Iacheni ACT kama itakataliwa na Watanzania ila sio wachawi kuipinga na kuichulia,kwani ninyi chadema uhalali wa kisiasa mnatoa wapi ACT wasiwe nao!???? Acheni ujinga wenu Chadema
 
Chuki kwa ACT ni upuuzi wa mijitu isiyo fahamu maana pana ya demokrasia! Ni mijitu ya chadema ambayo inataka demokrasia isikue hapa Tanzania! Iacheni ACT kama itakataliwa na Watanzania ila sio wachawi kuipinga na kuichulia,kwani ninyi chadema uhalali wa kisiasa mnatoa wapi ACT wasiwe nao!???? Acheni ujinga wenu Chadema

Sasa Mkuu Chadema wamwameingiaje hapa? Hicho Kilicho andikwa ni uongo? Tujielekeze kwenye hoja na tusifiche udhaifu wetu kwa kusingizia watu
 
Oooh! My brother Zitto unafanya nini sasa!!!?
 
Last edited by a moderator:
Huyu ndo anayedaiwa kuwa hazina ya taifa! Huyu ni mshenzi kupita washenzi wote kwenye siasa. We umealikwa halafu na wewe unaalika wanachama wa chama ambacho unajifichaficha kuwa mwanachama wake! Shame on you! Ni kama mtu umealikwa kwenye sherehe kwa kadi ya single halafi wewe unabeba na mchepuko kwenda nao! Huu ni upumbavu! Nadhani lipumba aliyekuwa anataka chadema wasuluhishane na zzk ameona kumbe kunguru hafugiki na chadema wamevumilia sana kuwa na type ya kishenzi kama hiyo. Nadhan prof hata amejionea mwenyewe jinsi chadema walivyohangaika na mzigo huo
 
Chuki kwa ACT ni upuuzi wa mijitu isiyo fahamu maana pana ya demokrasia! Ni mijitu ya chadema ambayo inataka demokrasia isikue hapa Tanzania! Iacheni ACT kama itakataliwa na Watanzania ila sio wachawi kuipinga na kuichulia,kwani ninyi chadema uhalali wa kisiasa mnatoa wapi ACT wasiwe nao!???? Acheni ujinga wenu Chadema

Mkuu mi nadhani mtoa mada au mada inayozungumziwa hapa inahusu ACT- TZ na CUF. Ebu nijulishe chadema imeingiaje hapa hata wewe ukaona ndo mhusika mkuu ktk comment yako? Turumbane kwa hoja plz
 
Upuuzi huo watafuteni wapuuz wa kuuamin

WATU WANAPIGA KAZI KUPAMBANA NA UFISADI NYINYI MNAENDELEZA PROPAGANDA ZA KIFEDHULI

WAPUUZ WAKUBWA,BADALA YA KUTUPIA MACHO KWA WEZI WALIOWAIBIA FEDHA ZENU NYINYI MNATUPIA MACHO SIASA ZA MAJITAKA
Lazima tuwaeleze mmeolewa na mume gani maana ukipenda hata chongo unaita kengeza
 
Tusubiri kauli ya Lipumba. Walikuwa wanataka kumtumia Zitto kisiasa kwa manufaa yao ya kisiasa
Kwa hiyo Zitto akawawai kwa kuwaleta wapambe wake wa ACT pamoja na waandishi wa habari wa kumremba.?
 
Niliona kiburi na dharau yake pale alipokuwa anasalimiana na Lipumba huku hajachomeka shati,Baadae anahutubia hajavaa mkanda,ile ni jeuri tu ya kitoto. Ana marafiki wengi wa face book watoto wa f2,3,4 nae yupo hivo.Akasema mbowe akiniomba nitamsaidia issue ya bomba la gesi. Hivi yeye alimuomba mbowe amsaide issue ya escrow na ripoti yake nyepesi.Huyo ndie litaka uraisi na uenyekiti wa chama kubwa
 
Sasa Mkuu Chadema wamwameingiaje hapa? Hicho Kilicho andikwa ni uongo? Tujielekeze kwenye hoja na tusifiche udhaifu wetu kwa kusingizia watu

Umbea huu ni wa kutoka mitaa ya ufipa-chadema
 
Vijana wa chadema mnalipwa nin kumsakama ZITTO mbona yuko kimya nyie mnahangaika na njia

Sasa hizo TUHUMA zinaweza kuandikwa na mtu yeyote mwenye chuki na ZITTO maana hazina uthibitisho wowote .
Nyie ndo mtakao vuruga hata muungano wetu wa ukawa kwa kushinda kwenye mtandao mkipiga majungu badala Ya kuhangaika namna Ya kuidhoofisha CCM mnahangaika namna Ya kumdhoofisha ZITTO kwa juhudi zozote zile
Kesho na Kesho kutwa mtaanza tena na Lipumba kwa propaganda chafu hatimaye muungano wa ukawa unakufa.
 
Nilishasema, ZZK nje ya CHADEMA ni kama chui wa karatasi. Hapo alipo yuko kwenye dilemma kuhusu future yake kisiasa. Kama ni mwanaume kweli mbona bado anashindwa kujitokeza hadharani na ACT yake?
Ni ajabu hata hao CUF kumpa platform. Zito ni msaliti wa MAGEUZI CAUSE. Haiwezekani wote tuko kwenye mashua baharini halafu mwenzetu anaanza kuutoboa. Kwa ujumla wetu tutapambana naye kumzuia na kama anaendelea uamuzi muafaka ni kumtosa baharini na kutuacha sisi tuendelee na safari Yetu.
amezidi kujianika.
 
Back
Top Bottom