Prof Kitila: Magufuli usiteue Wahadhiri

Yaani tz upinzani hamna na watanzania wengi waropokaji na x waongeaji maana mtu ambaye anashindwa kusimamia maneno yake na kuweka tumbo mbele ni mropokaji na x kwa kitila tu yoyote hapo akiteuli atakubali tu maana hata mkulu nae hajawahi kusimamia maneno yake
 
Kitila ni Mtumishi wa umma na hii ni post ya ndani ya utumishi wa umma angechukuliwa kwenda kuwa katibu mkuu wa CCM hapo sawa mngekuwa na haki ya kusema
Umeelewa hoja iliyoko mezani kweli? Hata hivyo, mtumishi wa serikali anaruhusiwa kushiriki siasa za moja kwa moja kama alivyokuwa Prof Kitila? Unafahamu kilichowakuta akina Prof. Baregu, Dr Lwaitama?
 
Umeelewa hoja iliyoko mezani kweli? Hata hivyo, mtumishi wa serikali anaruhusiwa kushiriki siasa za moja kwa moja kama alivyokuwa Prof Kitila? Unafahamu kilichowakuta akina Prof. Baregu, Dr Lwaitama?
Kama unabisha Kitila si Mtumishi wa umma bhasi sina cha kuongea bt nenda kaulize wenzio Kitila alikuwa Mtumishi wa wapi kama si wa umma?
 
lengo la kuanza kwa swali hilo ninataka kujua kama maneno ya wanataaluma wetu wanamisimamo na wanavyo vitu wanavyo vi-zungumz. katika sehemu mbili zilimnukuu Prof. Kitila Mkumbo akisema "Huu utaratibu wa kuwateua wasomi tu ambao ni walimu na wanataaluma kutoka vyuo vikuu hasa Chuo kikuu cha Dar es salaam si mzuri maana rais haoneshi kuwaandaa wengine kuchukua nafasi zao, tuachwe wasomi tufanye kazi za kitafiti na kitaaluma" hiyo ilikua ni 17/4/2016 source ilikua ni ITV

Pia Tanzania Daima liliandika hivi:
"Mhadhiri Muandamizi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Kitila Mkumbo amemshauri Mh Rais Magufuli aache kuteua Wahadhiri katika nafasi za kisiasa ama majukumu mengine kwa kuwa vyuo vikuu vimeanza kukabiliwa na uhaba wa wahadhiri baada ya wengi wao kupewa teuzi mbalimbali.

Aidha Prof Kitila amesema vyuo vikuu vilivyoathirika zaidi baada ya wengi wa wahadhiri wake kuteuliwa ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).

Chanzo: Tanzania Daima January 20,2017"


sasa swali ni je yeye mbona hajakataa hiyo nafasi ya ukatibu ukuu

Alichokisema ni ukweli na kina maana hadi sasa. Kama wewe ni mtu wa haki, tueleze tangu ametoa ushauri huo wameteiliwa PhDs and Professors wangapi? Labda kama una ushahidi wa Prof. Kitila kumuomba Mhe. Rais ampe hiyo nafasi. Alitoa ushauri nadhani umekataliwa. Prof. Kitila sio Yesu wa Tanzania, Rais ameona anafaa kwa nafasi hiyo.
 
Kama unabisha Kitila si Mtumishi wa umma bhasi sina cha kuongea bt nenda kaulize wenzio Kitila alikuwa Mtumishi wa wapi kama si wa umma?
Utakuwa hujanielewa. Sijabisha kwamba Kitila hakuwa mtumishi wa umma, bali nilichofanya ni kukuongezea wewe tafakuri: Sasa twende pamoja: Kitila alikuwa kada wa Chadema lakini huku akiwa mwajiriwa serikalini akifundisha UDSM, baadaye akahamia ACT Wazalendo huku akiendelea kufundisha UDM hadi jana alipoteuliwa kuwa KM. Profesa Baregu na Dr Lwaitama nao walikuwa wakifundisha UDM kama ilivyokuwa kwa Prof. Kitila, lakini walipoamua kuwa makada wa Chadema "wakashughulikiwa" na serikali kwa hoja kwamba kama waajiriwa wa serikali hawapaswi kujishirikisha na vyama vya siasa. kama utapenda utafakari hili...
 
Nimeona tweet yake chezea chakula kudadadeki hakyanani chakula kinaziba mdomo
Plasta full cross kama msalaba mdomoni. Eti hawezi kukataa kwa vile anapandishwa cheo na kwamba anaenda kutumika umma. Alilalama nini wakati wenzie wanateuliwa? Tatizo ni hapo tu. Angekaa kimya watu wasingehoji.
 
5bfec471cae44aa8116a704a21b07fdb.jpg

Mhadhiri kakubali kuteuliwa kiroho safi najua katengua ile kauli yake ya raisi asiteue waadhiri
Ndio maana nyerere alisema tusiwe na raisi anayeshauriwa na mke wake... Hii issue ya kitila ina maana yeye hawakuzungumza Kabla ya uteuzi....
 
Kwani hivyo vyuo havina SUCCESSION PLAN? Haviandai watu wa kushika nafasi iwapo mmoja akiondoka aliye chini apande? Hivyo vyuo vina tabia ya one man show kwenye vitivo ?
hapana YEHODAYA. succession plan zipo ila baraka ndo hazipati.
nakupa mfano mdogo tuu wahadhiri wapya walioko vyuoni ni wale tu ambao wakati wa mradi wa stehp walipata nafasi ya kwenda masomoni na hivyo wakaja kuwa wahadhiri.

wale ambao walisoma nje ya mpango huo na kurudi sasa kutaka kuajiriwa -(manake pia vyo haviwez kumudu kusomesha wahadhiri wote bila wengine kujisomesha wenyewe)- hawapati ajira kwani mpaka sasa hawana fungu la kuajiri
 
Ndio ishatokea tena hivi sasa anafunga mizigo kuhamia nyumba mpya!
Tena itakayosheni furniture zote na magari ya kifahari mengi, safari za nje, marupurupu, ofisi ya kiyoyozi, bila kusahau walinzi, FFU, bure bure kibao, imetoka, jamaa kaula, mdomo fyuu atapotea kama Bw. Polepole..
 
Tena itakayosheni furniture zote na magari ya kifahari mengi, safari za nje, marupurupu, ofisi ya kiyoyozi, bila kusahau walinzi, FFU, bure bure kibao, imetoka, jamaa kaula, mdomo fyuu atapotea kama Bw. Polepole..
watu wanaangalia tamati"
 
Asipoangalia anaelekea kuwa kama prof li pumbavuz!..
Bahati mbaya sana jina lake linareflect huko alikoitwa...
 
Kuna tofauti gani waliomtangaza lowassa kwenye list of shame kwa miaka 8 mfulilizo na wakaja mkanusha na kumpigia kifua. Au kunya anye kuku akinya bata ttzo??
So hitimisho lako ni nin?
 
Back
Top Bottom