ITEGAMATWI
JF-Expert Member
- Jan 26, 2012
- 5,310
- 4,040
Njaa haina adabu, leo anayakana maneno yake
Kwani hivyo vyuo havina SUCCESSION PLAN? Haviandai watu wa kushika nafasi iwapo mmoja akiondoka aliye chini apande? Hivyo vyuo vina tabia ya one man show kwenye vitivo ?
Njaa haina adabu, leo anayakana maneno yake
ExactlyAkili haijawahi kuishinda njaa
Kuna maswali mengine, majibu yote A & B ni sahihi,lengo la kuanza kwa swali hilo ninataka kujua kama maneno ya wanataaluma wetu wanamisimamo na wanavyo vitu wanavyo vi-zungumz. katika sehemu mbili zilimnukuu Prof. Kitila Mkumbo akisema "Huu utaratibu wa kuwateua wasomi tu ambao ni walimu na wanataaluma kutoka vyuo vikuu hasa Chuo kikuu cha Dar es salaam si mzuri maana rais haoneshi kuwaandaa wengine kuchukua nafasi zao, tuachwe wasomi tufanye kazi za kitafiti na kitaaluma" hiyo ilikua ni 17/4/2016 source ilikua ni ITV
Pia Tanzania Daima liliandika hivi:
"Mhadhiri Muandamizi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Kitila Mkumbo amemshauri Mh Rais Magufuli aache kuteua Wahadhiri katika nafasi za kisiasa ama majukumu mengine kwa kuwa vyuo vikuu vimeanza kukabiliwa na uhaba wa wahadhiri baada ya wengi wao kupewa teuzi mbalimbali.
Aidha Prof Kitila amesema vyuo vikuu vilivyoathirika zaidi baada ya wengi wa wahadhiri wake kuteuliwa ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).
Chanzo: Tanzania Daima January 20,2017"
sasa swali ni je yeye mbona hajakataa hiyo nafasi ya ukatibu ukuu
Mbatia kwani alishawahi kuponda uteuzi wa aina yake kabla yake??MBNA uteuzi wa mbatia mlikaa kimya