Prof. Kabudi aieleza Jumuiya ya Kimataifa kuwa Tanzania haijawahi kushindwa vita ya aina yoyote

Aliyoainisha Mhe Palamagamba Kabudi ni sahihi kabisa kwa upande mmoja wa sarafu lkn kwa mwenye akili aweza kuchambua hotuba ktk maeneo kadhaa kama ifuatavyo:-

(i). Kuhusu Mwl Nyerere kurudisha fedha kwa Uingereza na Ujerumani miaka ya 60 ilikuwa sawa - sasa kwa miaka hii ya 2020 ni sahihi kurudisha fedha sababu ya kulalamikiwa juu ya uchaguzi kughubikwa na mauaji, kutesa, na kukamata wapinzani?
Sawa ameeleza kuwa duniani kote huwa hakuna uchaguzi huru wala haki kwa standards ya 100 lkn amejiuliza kwa nini katiba ilitungwa, amejiuliza kwa nini Sheria zilitungwa? - Ni kwamba viwe vipimo vyetu ktk utendaji wa kila siku;

(ii). Madai ya kero za uchaguzi (kabla, wakati na baada ya uchaguzi). Hivi tumefika hatua ya kubariki mauaji, unyanyaswaji na ukandamizaji wa kidemokrasia kiasi cha kutambia dunia! Mie nilidhani kwamba angeeleza umma kuwa mambo yaliyojitokeza kwenye uchaguzi yanaendelea kushughulikiwa na mamlaka za ndani na kuahidi kupata suluhu kwa njia za mazungumzo na makundi yanayovutana - sasa chukulia mfano fedha za misaada zizuiliwe - hivi tutakuwa ni ukoo wa binadamu gani?

(iii). Viongozi, ndio wenye maslahi makubwa ya kitaifa sasa wasitengene njia za kuikosesha nchi misaada sababu bado tunaihitaji dunia, bado tuna changamoto kwenye afya, elimu, maji, kilimo, usafiri na usafirishaji, huduma za kiuchumi nk nk - kama tunatofautiana nao tutofautiane kwa sababu zenye uzito kama kukataa ushoga, udini, ukabila au ukanda lkn sababyinayotufanya leo tukosane ni ya kitoto na tunatakiwa kuizuia.

Mhe Palamagamba Kabudi, liangalie taifa hili limejaa watu wenye uhitaji sasa maslahi ya kisiasa kwa kundi dogo si sawa - wanaoathiriwa na kuzuiliwa fedha ni CCM, CDM, ACT, CUF, NCCR na vyama vingine pamoja na wasiokuwa na chama - ninyi mmeapa kutumikia hawa hawa ambao mnataka kuwasitishia misaada - NOT Good at all!

Msakila M Kabende
Kigoma
 
Utu?!

Hata hajui maana ya hilo neno, kutesa, kubambikia watu kesi, kupora wapinzani ushindi wao, hayo hayahusishi utu?

Wameshanganyikiwa, serikali imesha panic, sasa wanarusha mateke hovyo, yaani mshinde kwa kura feki halafu mlete habari za utu?

Acheni utani.
 
Prof. Palamagamba Kabudi amesema Tanzania haifuati sera za kidiplomasia za kujitenga kufanya kazi na Jumuiya za Kimataifa. Hivyo waziri Kabudi amesema Tanzania ipo tayari kukaa ktk meza moja na wadau wa kimataifa kuzungumzia mapungufu yaliyopo lakini si kwa kuburuzwa na mabeberu bila kuwa na facts mezani.
Hiki ni kitu cha Msingi sana naongea na ni FACT.....Naipenda Nchi Yangu Tz

Mapenzi yang kwa LISSU yangu hayawezi zidi Mapenzi yangu kwa NCHI Yangu Tanzania
 
Inatisha viongozi wanapoficha vichwa mchangani ili kuwadanganya raia…. Kamwe usifananishe na Nyerere. Yaani EU ikiuliza 27m Euro zake zimetumiwaje, hiyo ndiyo kuingilia mambo ya nchi? Mlipozichukua na kuzitumia kinyume cha makubaliano….?

Kama wewe mwanadiplomasia, afadhali kuanzia sasa uanze kuyatuliza haya mambo, la sivyo siri nyingi zitafichuka. EU hawashindwi kujua, tena precisely, kiasi gani cha fedha hizo kimetumiwa katika kampeni, kiasi gani kimetumiwa katika 'shughuli' nyingine!
 
Prof. Palamagamba Kabudi ameianza safari hii ya kujaribu kuitetea Tanzania chini ya utawala wa CCM Mpya kwa mguu wa kushoto na kuteleza ki-diplomasia. Kuwaita wabunge wa bunge la Ulaya kuwa ni 'wahuni wachache' basi katika vita hii atashindwa vibaya.

Maana vitani hakuna kumdharau 'adui' yako lazima kwenda vitani kwa weledi mkubwa.
 
Anajua kwamba yeye na familia yake hivyo vikwazo haviwezi kuwaathiri isipokuwa vitawaathiri watanzania wavuja jasho. Sio diplomatic language kama imetumika. Well, I hope ameona mtangulizi wake kwenye hiyo wizara jinsi alivyobadilishwa wizara baada ya kuwa diplomatic. I that regard therefore, lets try to put ourselves in his shoes....
 
Hana ujanja wa kumwambia mzungu yoyote hilo. Huyo ni futuhi kama futuhi nyingine.

Kweli kabisa tunataka Prof Kabudi awafuate huko huko Brussels au amuite mwakilishi wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya EU nchini Tanzania na mabalozi wa nchi wanachama wa EU wenye balozi zao Dar es Salaam awaambie uso kwa uso kuwa wale wabunge wa kamati ya Mambo ya Nje wa Bunge la Umoja wa Ulaya " Ni wahuni wachache" wazandiki wanapata wapi uwezo wa kuijadili nchi yetu dona-kantri na Tanzania haibabaiki.

Hapo ndipo tutajua ujabali wa serikali ya Tanzania kuwa nchi huru na haikubali kuburuzwa na vinchi vidogo matajiri-beberu wakati Prof Kabudi ndiyo anafahamu ukweli kuwa Tanzania siyo nchi ndogo bali ni Taifa Kubwa la kuogopwa.
 
Yeye hatakufa kwa kukosa dawa au kushindwa kununua dawa wala familia yake hawatakosa matibabu.
Hiyo kauli yake ni kwa vile maumivu watapata wale maskini waliompigia kura ndiyo maana anachochea moto kwa kauli zisizo za kidiplomasia.

Bado tuna kumbu kumbu mbaya mno ya maisha ya mwanzo mwa miaka ya 80.Maisha ya kula unga ulioharibika kutoka NMC.Maisha ya kukosa hata dawa ya sikio na badala yake kutumia mafuta ya kuku.Leo kuku wako wapi zaidi ya hawa wa kisasa?

Kwa vijana waliozaliwa miaka ya 90 hawatajua machungu tuliyopitia.
 
Back
Top Bottom