Prof. Kabudi aieleza Jumuiya ya Kimataifa kuwa Tanzania haijawahi kushindwa vita ya aina yoyote

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,213
24,076


WAZIRI WA MAMBO YA NJE TANZANIA PROFESA PALAMAGAMBA KABUDI AWAJIBU MABEBERU, HATUJAWAHI KUPIGISHWA MAGOTI, UCHAGUZI ULIKUWA HURU NA HAKI

Waziri wa Mambo ya Nje Prof. Palamagamba Kabudi aijibu EU - Umoja wa Ulaya kufuatia kikao cha bunge hilo la ulaya huko makao makuu ya EU kutishia uwezekano wa vikwazo kupitia Kamati yake Mambo ya Nje ya Bunge la Umoja wa Ulaya kujadili uwezekano wa kuibana Tanzania kwa vikwazo vya aina mbalimbali ikiwemo kusitisha msaada wa kuifadhili bajeti ya Maendeleo ya Tanzania.

Prof. Palamagamba Kabudi ameomba msaada wa vyombo vya habari nchini kuisaidia serikali ya Tanzania kwa kujitokeza na kuieleza Jumuiya ya Kimataifa ukweli wa mambo. Na kueleza Nyerere aliwahi kuwadindia Germany na United Kingdom na kukataa misaada na fedha zao. Prof. Palamagamba Kabudi anashangaa waTanzania kuanza kutetemeka ktk mitandao ya kijamaii kuhusu nchi yetu kuwekewa vikwazo.

Prof. Palamagamba Kabudi amesema Tanzania haifuati sera za kidiplomasia za kujitenga kufanya kazi na Jumuiya za Kimataifa. Hivyo waziri Prof. Kabudi amesema Tanzania ipo tayari kukaa ktk meza moja na wadau wa kimataifa kuzungumzia mapungufu yaliyopo lakini si kwa kuburuzwa na mabeberu bila kuwa na facts mezani.

Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa watu wahuni wachache wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Ulaya EU hawawezi kuitisha na kuidhalilisha Tanzania na watambue Tanzania ni nchi huru.

Prof. Palamagamba Kabudi amesema maneno hayo mazito akiongea na Wafanyakazi wa Wizara hiyo muhimu ya Mambo ya Nje akatumia fursa hiyo kujibu uvumi kuwa Tanzania itanyimwa misaada na kuwakumbusha wafanyakazi hao kutembea vifua mbele kwani Tanzania siyo nchi ndogo kidiplomasia, kimsimamo, kiji-Geopolitiki na kiushawishi kimataifa.

.....................................................

EU Parliament Committee on Foreign Affairs discussion on Tanzania​

Tujikumbushe walioitwa "wahuni wachache" na Prof. Kabudi, tarehe 19 November 2020 jijini Brussels kwa dakika 45 mfululizo walisema nini kuhusu Tanzania ktk kikao cha Kamati ya Mambo ya Nje cha Bunge la Jumuiya ya EU
Tazama / sikiliza dakika 45 za mjadala ktk kamati hiyo:

 
Huyu jamaa alinifanya nihairishe kusomea PHD pamoja na kuchaguliwa kusomea kozi hiyo Mlimani.

Yaani ukimuangalia machoni unaona kabisa anaongea aliyotumwa akaseme Prof. mzima unalazimishwa kuongea "pumba" kwa ajili ya kulinda ajira yako! Shame on you Sir
 
Ngoja tuone kama dunia ya 2020 ni kama ya 1965. Mwaka 1965 kulikuwa na USSR. 2020 kuna Russia tu.

Heshima gani inaongelewa hapa? Yaani heshima ndio hiyo tuliyoiona 27 Okt 2020 na 28 Okt 2020? Yaani utu wa Mtanzania (nikiwemo mimi) ni CCM kushinda uchaguzi kwa nguvu kwa kura za mabegi meusi na vikapu vya sokoni na wapinzani kutekwa ili CCM wapite bila kupingwa? Mawakala wa vyama vingine kufukuzwa katika vituo, ndio heshima na utu wa Mtanzania huo? Kweli tunadili na watu waliotoka jalalani!

Haya endeleeni kujimwambafai. Ningependa kujua hao wapiga makofi ni akina nani. Bila shaka watakuwa ni akina Bia yetu, Johnthebaptist, magu2016, Jane Lowassa, mama D.... Nchi yaani ina watu wengi sana wasiojitambua. Wako kama mbwa. Wakipata chakula tu basi kazi yao ni kutikisa mkia tu kila wanapomwona anayewapa chakula!
 
Naona tunazidi kulikoroga, hakuna lugha ya kidiplomasia kabisa..

Halafu mbona Lissu mwenyewe ameonyesha kutaka maridhiano, Sefu nae anataka maridhiano ilikuwa ni kuwapiga lugha ya kidplomasia tu mabeberu wangeelewa.

Sijui kwa nini nimemkumbuka Dr Mahiga, angepiga mstari mmoja tu wa maana jamaa wangeelewa.

Lakini kwa kauli hizi za paniki tutakaoumia ni sisi Watanzania wa kawaida.

Halafu sioni Kabudi akimaliza miaka mitano ya Uwaziri, mbinyo ukizidi yeye ndio atakaetolewa kafara.
 
Back
Top Bottom