Prof. Kabudi afunika bungeni

Sugu ameingiaje kwenye hoja yako?Usijali umeonesha UNACHOMAANISHA!Ulimwelewaje Lema aliposema'Upande huu ukiwanyika na upande huu mtaligawa Taifa'?
 
Ameongea vizuri ila bahati Mbaya sijui kama ataweza kudumu kwenye utawala wa JPM,inaonyesha ni mtu mwenye msimamo wake na mawazo yake.Sijui kama atasurvive
Ndilo tatizo kubwa awamu ya 5.
Wanatakiwa watu wa aina ya mwakiwembe wenye njaa na kuitikia ndio mzee
 
Leta ushahidi siyo unapiga mayowe kwenye darasa tulivu
 
Yeyote aliye ndani ya ccm ni adui wa maendeleo ya kweli kwa watanzania. Vimaendeleo wanavyofanya ni vya hadaa ya kuombea kura tu kipindi cha uchaguzi. Tunasubiri mtakavyotetea ununuzi wa ndege kwa maendeleo ya Taifa kipindi cha kampeni
Badala ya kusibiria faida itakayoletwa na matumizi ya hizo ndege za taifa, wewe unawaza negativity tu. Endeleeni nyoshea ccm vidole wakati vidole vitatu vinawakanya nyinyi.

Wananchi wengine ni gundu tu nchini
 

Mtaishia kusifia wenzenu tu
 
Njaa kitu kibaya, hatari mno.

Ameongea utani na mipasho ya kutetea serikali.

Kifupi kaulizwa kwa nini sheria zilizopendekezwa zibadilishwe na Tume ya 1980 zipo mpaka leo?

Jibu lake, kasema, kwa anavyojua yeye kama profesa wa sheria, na muelewa wa mambo ya legal anthlopology, ni kwamba sheria zinazohusu mambo ya kimila, kiitikadi, kidini, kijima, hazibadilishwi kwa kukurupuka.

Akaendelea kusema, ndio maana mpaka leo kwao yeye Waziri wanakeketa vitoto vya kike, na pia kwao mbunge muuliza swali, ambae ni Mkurya, wanawake zao hawapendeki bila kupigwa. Kwa hiyo sheria hizi inshallah zitakuja kubadilishwa. Ndio maneno ya waziri hayo.

Hapo kwenye jibu hilo kuna weledi gani wa kusifiwa?
 
Tunasubiri 2020 Kitila Mkumbo achukuwe Iramba baraza la mawaziri litakuwa na timu nzuri sana.
 
Hata kama nilikuwa nampenda vipi! Mtu skishsjiunga na genge la maccm namchukia automatically! Naichukia ccm jamani! Kha! Kujihusisha na kitu chochote cha ccm naons km ni kujinajisi!
 
mlugo bado anaendelea kuonyesha ukilaza wake... eti elimu ya lazima ni chekechea mpaka kidato cha nne!!!

Mulugo yupo sahihi. Wewe ndo hufuatilii mambo. Kwa sasa kidato cha nne ni elimu ya lazima na ndo maana serikali inasema inatoa elimu bure hadi kidato cha nne. Jipe muda kufuatilia
 
..mlinganishe Prof.Kabudi na Mzee wa "catalyst".

..uongozi, haswa wa kisiasa, hauhitaji mtu anayewaza kudhalilisha wenzake wakati wote.

..natumaini ustaarabu na utu uzima wa Prof.Kabudi utalisaidia bunge na serikali.

NB.

..pamoja na ustaarabu wa Prof sijapenda alivyofanyia mzaha suala la wanawake kupigwa. Prof akumbuke matamshi yake bungeni yanarekodiwa kwenye hansard.
 
Mulugo yupo sahihi. Wewe ndo hufuatilii mambo. Kwa sasa kidato cha nne ni elimu ya lazima na ndo maana serikali inasema inatoa elimu bure hadi kidato cha nne. Jipe muda kufuatilia
Sasa wale ambao hawachaguliwi watamalizia wapi hiyo elimu ya lazimaπŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…