Prof Issa Shivji: They are blinded by power and protected by walls, but they will go down eventually

Prof Issa Shivji: They are blinded by power and protected by walls, but they will go down eventually

BTW hakuna hata Mtanzania moja anayemwabudu JPM huo ni uongo na ulaghai wa hali ya juu, hivi huu uongo ndio unaopelekea Max kupata tuzo? Kama ni hivyo basi hata muktada wa kuongoza Serikali utakuwa hauna maana kwa sababu wengi wanafikiria majungu zaidi.

Baada ya 2025 tutakumbushana humu JF jinsi 2015 ilivokuwa ie alipoikuta Tanzania iliyoachwa na JK na mahali atakapotufikisha JPM inshallah 2025, miaka minne tu mafanikio ya JPM yanawafanya wengi wakose usingizi maana, kwanza hakuna hata moja anayeweza kusema anaweza kumuhonga rais wala anayeweza kusema anaweza kumshawishi JPM kwa jambo lolote. Hiyo ndio heshima ya kuwa rais. Shida zenu binafsi tatueni nyinyi wenyewe binafsi msimsukumizie rais. JPM ana kazi moja tu na ni mkataba wake na Watanzania, nyinyi wengine mlie tu hadi chozi la damu liwatoke.

JPM piga kazi kelele za mlango zisikukoseshe usingizi Watanzania wengi tupo nyuma yako na kuku-support.
Wengi wangapi??usikute ni wewe peke yako hata ndani ya familia yako hawako nae wote.
 
Prof Shivji na Richard S Mabala; Mabeberu wamechachamaaaa. Wanashangaa mweusi anawapeleka puta,hawaamini.,wamepoteana.
 
BTW hakuna hata Mtanzania moja anayemwabudu JPM huo ni uongo na ulaghai wa hali ya juu, hivi huu uongo ndio unaopelekea Max kupata tuzo? Kama ni hivyo basi hata muktada wa kuongoza Serikali utakuwa hauna maana kwa sababu wengi wanafikiria majungu zaidi.

Baada ya 2025 tutakumbushana humu JF jinsi 2015 ilivokuwa ie alipoikuta Tanzania iliyoachwa na JK na mahali atakapotufikisha JPM inshallah 2025, miaka minne tu mafanikio ya JPM yanawafanya wengi wakose usingizi maana, kwanza hakuna hata moja anayeweza kusema anaweza kumuhonga rais wala anayeweza kusema anaweza kumshawishi JPM kwa jambo lolote. Hiyo ndio heshima ya kuwa rais. Shida zenu binafsi tatueni nyinyi wenyewe binafsi msimsukumizie rais. JPM ana kazi moja tu na ni mkataba wake na Watanzania, nyinyi wengine mlie tu hadi chozi la damu liwatoke.

JPM piga kazi kelele za mlango zisikukoseshe usingizi Watanzania wengi tupo nyuma yako na kuku-support.
Nikweli 100%ila akiba ya maneno muhim...
 
Wakishaachia madaraka ndio wanaaza toba na kutunga vitabu "Mahakama zisiingiliwe na wana siasa,kuwe na tume huru,kuwe na katiba mpya,wapinzani washikishwe kwenye kuhesabu kura..........majuto mjukuu sasa hivi wanaweka pamba masikioni muda utasema tu.
 
Wamepewa Huawei na bando wanajaziwa ili wahare mitandaoni!!
Hivyo vyote ni vya muda tu,itafika muda watu wote tutaongea lugha moja.ndio sababu mimi napenda tuende hivi hivi ili hata ile mizumbukuku ya kutupa iamke usingizini.
 
Wewe unaukumbuka "mkataba" aliopewa wa kuwakandamiza na kuwanyima haki waTanzania?

Mkuu mkataba ndio huo aliopewa katika kipindi cha miaka 5 kuongoza kufuatia ridhaa ya wananchi kupitia ilani ya chama chake Cha Mapinduzi. Utekelezaji wa ilani hiyo ndio umewezesha miradi mingi kutekelezwa katika kipindi hiki cha miaka minne.

Swala la ukandamizaji wa haki kwa Watanzania, ni haki ipi hiyo ambayo imekandamizwa au kunyimwa? Labda mie ndio nina makengeza hebu nifafanulie hapo ili niweze kuona haki hizo ambazo wewe pamoja na wachangiaji wengine wanazisema. Kwa sababu ninavyofahamu mimi hii katiba ambayo inatumika sasa JPM hakuitunga ameikuta sasa iweje leo hii hiyo hiyo misingi ya utawala bora iwe mibaya kwa JPM lakini awamu zote 4 ziilikuwa zinaitumia?
 
Ni kiongozi yupi hakuwahi kuwa na watu wanaomsupport? Nyie mnaotegemea madaraka yake kuendesha maisha yenu ndio mnaomsujudia, kibaya zaidi mnataka watu wote wamsujudie. Haya maendeleo yanayoonekana kila rais ambaye angetaka kukopa na kujenga miundombinu tu angeweza, kama hutoi ajira na mishahara hupandishi na kukopa sana, utashindwa kufanya hayo? Tena sio kufanya tu, utakubali hata ukaguzi wa hayo unayoyafanya sambamba na kuacha mihimili na mifumo ifanye kazi kwa uhuru na weledi.

Una uhakika mimi maisha yangu yanategemea JPM kuwa madarakani? Una uhakika gani mimi namsujudia? JK na BMW pamoja na Mwinyi wamekiri wao wenyewe kwamba JPM ni jasiri sio siri. Sasa wewe tindo I mean honestly tindo tena unatumia jina bandia hapa JF unataka Watanzania wakuamini wewe ambaye hata hatuwezi kufahamu unaishi wapi?

Ukaguzi upi ambao unataka ufanyike? Wewe kwako imekuwa nongwa ATCL isikaguliwe? Vipi ndiko ulikuwa unashibia? Wewe hufanyi Serikalini sasa nyongeza za mishahara zina utaratibu wake huwezi kuongeza tu mishahara kama njugu, economy ya nchi lazima iangaliwe kabla ya kuongeza mishahara nk. JPM mwenyewe alishawaambia wafanyakazi ukifika muda mishahara itaongezwa. Who the hell are you ambaye unatumia jina bandia huna hata hadhi ya kuwa mkuu wa nyumba yako unayokaa unafikiri kuongoza Watanzania millioni zaidi ya 50 ni chandimu? BTW you know nothing and you should shut up. Unaitia aibu JF.
 
Baba wa taifa ni nani mpaka useme akimdharau mtu basi wote tutamdharau?

Na wewe ni nani kama sio kinyago tu! Hata avatar tu inaonyesha kwamba wewe ni Kinyago.
 
Mkuu mkataba ndio huo aliopewa katika kipindi cha miaka 5 kuongoza kufuatia ridhaa ya wananchi kupitia ilani ya chama chake Cha Mapinduzi. Utekelezaji wa ilani hiyo ndio umewezesha miradi mingi kutekelezwa katika kipindi hiki cha miaka minne.

Swala la ukandamizaji wa haki kwa Watanzania, ni haki ipi hiyo ambayo imekandamizwa au kunyimwa? Labda mie ndio nina makengeza hebu nifafanulie hapo ili niweze kuona haki hizo ambazo wewe pamoja na wachangiaji wengine wanazisema. Kwa sababu ninavyofahamu mimi hii katiba ambayo inatumika sasa JPM hakuitunga ameikuta sasa iweje leo hii hiyo hiyo misingi ya utawala bora iwe mibaya kwa JPM lakini awamu zote 4 ziilikuwa zinaitumia?
Hiyo katiba inakuonyesha kwamba waTanzania hawana haki na uhuru wa kuwachagua viongozi wao bila ya mizengwe?
Kiufupi ni kwamba wewe kweli "una makengeza"kama ulivyojieleza hapo juu. Mimi siwezi kuwa 'surgeon' wa kurekebisha hayo makengeza yako.
Kaa nayo hivyo hivyo, tukibahatiwa, tutawaondoa mkizidi kung'ang'ania kutuburuza.
 
Back
Top Bottom