Prof. Ibrahim Lipumba yuko wapi jamani?

Mkuu Tanzaniaist,
Nime-edit title, badala ya kuandikwa "amekitekeleza" nimebadili na kuwa "amekitelekeza!" Nafikiri ndio Kiswahili sanifu!
 
Ipo siku na wengine nao watakimbia tu..... njaa kitu kingine bana! jamaa ana kibarua kinachomlipa vizuri akae CUF pana nini?
 
Hata mimi nahisi ataibukia wakati wa uchaguzi, nasikia kaenda kukusanya nondo za ushindi. This time hashindwi mtu!
 
Asalaam alyekum wana JF..!

Leo nimeona nikitazame Chama cha Wananchi (CUF)..,ambacho kilikuwa kama nguzo kuu ya Upinzani nchini na Tishio kwa chama Tawala CCM na kuweza kuaminiwa ipo siku itachukua Dola! Lakini hali imekuwa tofauti baada ya kuanza kuibuka migogoro pamoja na kukosa imani mbele ya wananchi na inaonekana dhahiri nafasi yao imechukuliwa na CHADEMA..,huku CUF imeanza kufananishwa na SAU au UPDP..na siku hadi siku chama kimekuwa kikipoteza Mvuto pamoja na Kukikimbiwa na Wanachama wake, Huku kikifananishwa na CCM B...!

Napenda nihoji yuko wapi PROFESA IBRAHIM HARUNA LIPUMBA...? Ambaye ndiye Mwenyekiti wa Chama! kumezuka kila aina ya migogoro,na chama kupoteza mvuto na hata kuchemsha vibaya kwenye chaguzi ndogo kama kule Igunga na Uzini...! Naamini kama Prof.Lipumba angelikuwepo angeweza kutuliza Mgogoro kati ya HAMAD RASHID na SEIF SHARIFF, na pia angekipa chama Nguvu kwenye kampeni ndogo kama kule igunga! na vile vile angekuwa anakiweka chama kwenye mwelekeo...!

Lakini sasa hivi ni dhahiri Pengo lake kubwa linaonekana na sasa hivi Chama kinamuhitaji kwenye muda huu CRITICAL ambako CUF kinaonekana kupoteza mwelekeo huku Majukumu makubwa akiachiwa Julius Mtatiro mtu ambaye experience yake ni Ndogo kisiasa kuweza kufanya maamuzi makubwa na kukiendesha Chama...! na tumekuwa tukishuhudia madudu yake kama kashfa ya magari na kuchemsha Igunga...! na hivi majuzi amedai CUF inajipanga Arumeru..,hii ni dhahiri CUF wanazidi kujipigia msumari kwenye Jeneza kabla ya kuingizwa kaburini...!

Ningependa Nishauri kokote kule Prof.Lipumba achukue maamuzi mawili mazito...,Kurudi na Kukifufua chama ama Kujivua Gamba La Uenyekiti na Kumwachia Mtu ambaye ataweza kukiendesha Chama katika Mstari..! kuliko kuwa kimya nchi za nnje...,Na sijuy siku Chama kitakaposarambatika Sura yake Ataiweka wapi ..?
Bwana Yesu asifiwe..
Kama kiongozi wao haonekaniki,members wake hawawezi kujiendesha na chama hakina muda mrefu kitakufa
 
Safari hii anataka kufata nyayo za mrema ktk ubunge,anataka kwenda kugombea ubunge kawe
 
Lipumba ni international figure, as much as anahitajika CUF anahitajika pia kwa faida ya Ulimwengu mzima..

Yuko anasaidia binadamu wengine duniani, CUF ni taasisi inajiendesha vema
 
Mwenyekiti wa chama cha CUF aka CCM B profesa Lipumba hivi yuko wapi? maana chama chake kinazidi kuelekea shimoni,ndoa waliyofunga na CCM inazidi kuwaumiza na wamekataa kutoa talaka wakisema kuwa nyie CUF ndo mlilazimisha kuolewa.Rudi mwenyekiti uone jinsi Ismail Jussa alivyojigeuza katibu mkuu wa CCM B.
 
Wacha wafu wazike wafu wao.

Katibu yupo ikulu nanakula bata mwacheni lipumba ale vitu vilivyopimwa.
Kama ni lichama alishahangaika nalo vya kutosha kwa kufikiri ni chama cha siasa kama kilivyoanzishwa na mapalala kumbe kilishatekwa na maalim ili kimrudishe serikalini na lengo limeshatimia.

Lipumba mtaalamu wa uchumi amewaachia kina nape na uchumi wao unaopaa kwenye makaratasi acha ale bata na wenye akili wenzake kina obama.
 
Prf.Lipumba yuko nchini Marekani. Alishinda na kuchaguliwa kuwa miongoni mwa wachumi wanaoshughulikia uchumi wa dunia na shirika la NED la Marekani. Hawa ni baadhi tu ya lulu tulizotunukiwa nchini Tanzania na tukashindwa kuzitumia,tunakalia siasa za majitaka zinazotuongezea umaskini kila kukicha.

Profesa Lipumba anajulikana kimataifa kwa mchango na uwezo wake kama mchumi aliyebobea kuliko anvyojulikana hapa Tanzania. Shame on this country and its people!

Imagine mtu kama huyu angekuwa Rais wa nchi yetu,tungepiga hatua kubwa kiasi gani kiuchumi?
 
Back
Top Bottom