Prof. Ibrahim Lipumba yuko wapi jamani?

Truly, CUF RIP at last!!

Hivi kaka unategemea lolote jipya kutoka CUF? Wenzio wako kwenye mahaba mazito na CCM wewe unataka kuingilia mambo ya watu. Upinzani wa kweli hautakaa utoke CUF hii ya sasa; labda wajipange upya tena wajipange haswa.

Walivyokuwa wanakaa kwenye vikao vyao vya miafaka kwa kificho wenye akili zao walionya na kupiga kelele, CUF wakaona wanaonewa gere kumbe ndio hivyo chama kilikuwa kinaelekea kaburini kwa faida ya wachache. Inahuzinisha lakini hakuna neno jingine zaidi ya R.I.P. CUF.
 
Katika gogoro la CUF linaloendelea tungepewa unafuu kujua ustadi wa Prof. Mapumba katika uongozi kama angesema kitu katika ugomvi wa Maalim (mnywa whisky ikulu) na Hamad Rashid (Mpambanaji) lakini guess what Prof. Lipumba yuko kimyaaa kama mtu aliye katika kiharusi! Je huyu ndiye yule wana CUF huwa wanamsifia ati ana PHD ya uongozi ilhali akishindwa hata kuitisha kikao cha dharura cha NEC kusuluhisha gogoro hili? changanya na zako kupembenua Seif ni Mkubwa zaidi ya chama....ni hilo tu!
 
seif shariff hamad kasema urais ni zamu ya znz mwaka 2015 huoni kwamba Lipumba hatakiwi? unataka Lipumba asuluhishe nini kama sio kufurahia anguko la seif
 
Yuko USA kama mwanauchumi mahiri anafanyakaz huko. Wanaujua umuhimu wake wanamtumia
 
Lipumba kakalia kuti kavu kashindwa mara kadhaa kwenye mbio za Urais sidhani kama CUF wanamuhitaji tena
 
kama yuko USA hahusiki tena na chama basi aachie ngazi hakuna maana ya kuwa na mwenyekiti kutoka kwa Obama
 
mbona Asha Rose Migiro bado anakuja na kutoa mchango wake nyumbani kwani yeye ni Rais wa marekani?
 
Hierrachy ya Uongozi CUF
  1. Maalim sefu
  2. CUF (chama)
  3. Lipumba
  4. Wengineo
 
Lipumba kakalia kuti kavu kashindwa mara kadhaa kwenye mbio za Urais sidhani kama CUF wanamuhitaji tena
CHADEMA wanamhitaji akaongeze nguvu! Kulikataa vuguvugu la mabadiliko si uungwana ajiunge na chama chenye mshiko
 
Lipumba ni accidental politician.....
deep down sio mwanasiasa.....na wala hana imani kuwa ataingia ikulu...
anachokifanya ni kama kuondoa lawama tu na kutoa msaada kwa makundi fulani hapa TZ
hana njaa wala haja na siasa za Tz....anaombwa tu kuwepo.
 
Katika gogoro la CUF linaloendelea tungepewa unafuu kujua ustadi wa Prof. Mapumba katika uongozi kama angesema kitu katika ugomvi wa Maalim (mnywa whisky ikulu) na Hamad Rashid (Mpambanaji) lakini guess what Prof. Lipumba yuko kimyaaa kama mtu aliye katika kiharusi! Je huyu ndiye yule wana CUF huwa wanamsifia ati ana PHD ya uongozi ilhali akishindwa hata kuitisha kikao cha dharura cha NEC kusuluhisha gogoro hili? changanya na zako kupembenua Seif ni Mkubwa zaidi ya chama....ni hilo tu!

Ndugu mbona unajiuliza na kujijibu mwenyewe?
 
World bank na cuf wapi na wapi unataka lipumba aje aanze kupiga chafya kwa watu wasiojua kuoga? Unikome babu we
 
CUF wakivuka salama kwenye huu mgogoro watakuwa wamekomaa kisiasa, we are watching them
 
Back
Top Bottom