Prof. Haroub Othman Afariki Dunia

Mungu ametwaa mtu wake na amesimamia katika mema yote sisi Kama Watanzania watakukumbuka Daima
 
Ni mmoja wa walimu wachache chuo kikuu ambao walikuwa wakisema wazi wanayofikiri bila kuumauma. Taifa limepoteza mtu muhimu aliyependa kuona maendeleo yake. Hakuwa shabiki wa kusambartisha muungano.Alinifundisha development studies miaka hiyoo. Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya Huyu Prof Othman.Amen
 
Mimi personally, Prof. Othmani alinifundisha DS. He was a prolific writer and orator. Mungu amuweke mahala pema peponi.

Lakini moja ya tatizo langu na nchi zetu za kiafrika..hivi mtu kama Prof. Haroub..nchi yetu imemtumia vipi? Mzee kafanya kazi mataifa mbali mbali na mashirika mbali mbali ya kimataifa..lakini sijawahi ona pale ambapo..serikali yetu imechota hata ujuzi wa huyu marehemu. Zaidi ya kumuona critic wa kila kitu na hatimaye kumtenga. To me huyu mzee angepewa hata opportunity ya kumediate muungano..maana angewasaidia hata mawaziri wetu wanaobwabwaja tuu..siasa bila substance katika swala zima la muungano.

Mi napenda kuiasa serikali yetu..ijitahidi kuwatumia hawa wasomi..."it should swallow its pride" itambue kwamba hawa jamaa ni vichwa na wanaweza kusaidia kusukuma gurudumu la maendeleo la nchi yetu. Jamani wote tunajenga nyumba moja..kwa nini tugombanie fito? Juzi nilifarijika kuona Prof. Peter Maina wa sheria alipendekezwa na jamhuri yetu kuwa member wa UN Committee moja kule Geneva..atleast hata mzee akitoa mchango mle..watanzania tunaonekana tuko inchanrge wa maisha yetu.....Watu kama wakina Shivji, Maina, Muhongo, nk..wanafahamika na kuheshimika nje ya Tanzania..yet..sisi tunawahitaji lakini kwa ajiri ya kiburi na kujiona wajanja..tunawatenga hawa wasomi..wakifa ndo tunaweka eurology kibao..Its doesnt help.

RIP Prof. May God bless your soul.

NB; Ila serikali ianze kufikiria namna ya kuwatumia hawa wazee waliosoma kwa kodi zetu. They can contribute immensely for all we are strivin to achieve.
Baadala ya kujaza kurasa tukiwalilia..yet walipokuwa na uhai wa kutusaidia kama taifa hatukuwajali.

Masanja,
 
Ama kwa hakika kifo cha Prof. Haroub Kimnistusha sana. Kimekuwa cha ghafla mno. Haroub was a man of substance. Alijua anaongea ama kuandika nini. Cha ajabu alikuwa mpole sana. He never shout. alikuwa a ki argue kwa point makini na kwa upole. Alikuwa hapayukipayuki. Haroub alikuwa Kichwa has akatika masuala ya demokrasia na haki za binadamu. Alikuwa na extensive knowledge. Wengi waliopitia Mlimani watakubaliana nami kuwa Haroub alikuwa ni miongoni mwa Profs walioheshimika sana. Hata Nkrurumah akisimama Haroub ukumbi kimya!!!! IDS alikuwa ni mhimili mkuu. Taifa limepoteza kichwa! Poleni sana wafiwa. RIP Haroub
 
Ina Lilah Waina Ilayhi Raj'un.

RIP Prof..
Wanabodi kama kuna mtu anayo namba ya Tahir mtoto wa marehemu naomba ani PM...
 
RIP Prof Haroub Othman.
Death is always shocking but more shocking when its sudden death. Tumesikitishwa na kifo hiki cha ghafla lakini hatuna budi kukubali, wote tunaelekea huko huko.

Pole Nyingi kwa familia ya marehemu na pole kwetu sote kwa kupoteza nuru hii.
 
Naomba nijumuike kwenye kuambiana POLE hapa.

Profesa alinifundisha UDSM. Kabla ya hapo niligundua kwamba alikuwa mtu asiye na makuu. Nikiwa mwanafunzi wa Kidato Cha Sita Mkwawa nilimwandikia barua ndefu kuhusu Malcom X (baada ya mimi mwenyewe kufundishwa kuhusu huyo bwana na Shirazi Ramji). Profesa alijishusha na kuniandikia.

God is MERCY. We entrust Professor Haroub Othman into His hands.
 
Ni simanzi, ni huzuni, ni sikitiko, ameondoka gwiji, guru na mwanazuoni mbobevu Prof. Haroub Othman. Sina mengi ya kusema ulikuwa mwalimu wangu, upole wako na sauti yako ya chini lakini yenye ushawishi mkubwa itakumbukwa daima dumu.
.......Umetutangulia tu nasi twaja muda si mrefu, si mbali ulikoenda ni karibu mno, ni kweli utakwenda kuonana na hawa watu Mwl. Nyerere, Prof. Chachage, Abdulrahamni Babu, Yasser Arafat na wengineo. Waambie haya yafuatayo

Mwl. Nyerere
...Mwambie Uzanzibar na Utanganyika umepamba moto, kila mtu anataka taifa lake,
...Mwambie sio mpasuko tena kwenye muungano ila ni handaki ambalo bila dua zake uko aliko muungano utazama umo na kupotea milele
...Nchi imevemiwa na si wahujumu uchumi tena ila ni mafisadi wanaojibatiza majina wenyewe ya upapa na unyangumi
...Nchi imeoza inanuka, vijana aliowaacha hawafai wameshaiuza kitambo mara tu alipofariki
...Nchi inatawaliwa na mabepari aliowakataa enzi zake, wajanja wa kujitajirisha wenyewe na familia zao
...Ardhi aliyoilinda kwa faida ya wote sasa iko mikononi mwa mabepari wachache uchwara wa ndani na nje ya nchi,
...Usisahau kumwambia pia kuwa punde si punde Butiama itakuwa wilaya

Prof. Chachage
... Mwambie wale makuhadi wa soko huria wamekuwa moto, hakuna tena wa kuwaponda na kuwasema wazi,
...Mwambie wale wanafunzi wa vyuo vikuu aliowatetea hasa UDSM siku hizi hawana mtetezi tenz wanafukuzwa kwa memo kama manamba kwenye mashamba ya mkonge, hamna tena wa kuwatetea, UDASA ya sasa siyo ile ulioyoiacha, ina maprofesa waoga kama kunguru wa Zanzibar

Yasser Arafat
...Mwambie bado wapalestina hajakombolewa, ni danadana kila siku
...Mwambie bado muisraeli mmoja anafidiwa na wapalestina 1000
...Mwambie mauaji ndi yanapamba moto ukanda wa Gaza, mwambie wanawake na watoto wa KIpalestina wanauawa kila kuchapo hawana tena msemaje kama yeye

Adlrahamani Babu
...Mwambie Muungano unasuasua kutokana na maslahi binafsi
...Mwambie upinzani ndio kabisa unafifia hakuna jipya tena
...Mwambie Wazanzibar wanmkumbuka sana na kamwe hawawezi kumsahau

Usisahu kuwasalimia Kwame Nkrumah, na kumwambia muungano wa Afrika imekuwa ndoto za abunuwasi. Wasalimie pia akina Mwanawasa, Jomo Kenyatta, na wanamapinduzi wengineo wote waliokwisha tangulia mbele za haki. Amen

RIP Prof. Haroub Othmani
 
Aaaaaah..mbona hivi jamani?? yaani wale ambao tunawahitaji sanaaa wanatutoka!! yanabaki yale majizi tuuuu.. !!! I am speechless!!

Mwalimu wangu nitakukumbuka sana hasa kwenye msimamo wako mkubwa kwenye Human rights!!!!..Tanzania na Afrika bado inawahitaji sana wapigania haki za binadamu.

Pole sana Tahir ..na familia yako yote..

Mungu amlaze mahali pema peponi Prof.

-Wembemkali.
 
Ni simanzi, ni huzuni, ni sikitiko, ameondoka gwiji, guru na mwanazuoni mbobevu Prof. Haroub Othman. Sina mengi ya kusema ulikuwa mwalimu wangu, upole wako na suti yako ya chini lakini yenye ushawishi mkubwa itakumbukwa daima dumu.
.......Umetutangulia, ni kweli utakwenda kuonana na hawa watu Mwl. Nyerere, Prof. Chachage, Abdulrahamni Babu, Yasser Arafat na wengineo. Waambie haya yafuatayo

Mwl. Nyerere
...Mwambie Uzanzibar na Utanganyika umepamba moto, kila mtu anataka taifa lake,
...Mwambie sio mpasuko tena kwenye muungano ila ni handaki ambalo bila dua zake uko aliko muungano utazaa umo na kupotea milele
...Nchi imevemiwa na si wahujumu uchumi tena ila ni mafisadi wanaojibatiza majina ya upapa na unyangumi
...Nchi imeoza inanuka, vijana aliowaacha hawafai wameshaiuza kitambo mara tu ulipofariki
...Nchi inatawaliwa na mabepari uliowakataa enzi zako, wajanja wa kujitajirisha wenyewe
...Ardhi aliyoilinda kwa faida ya wote sasa iko mikononi mwa mabepari wachache wa ndani na nje ya nchi,

Prof. Chachage
... Mwambie wale makuhadi wa soko huria wamekuwa moto, hakuna tena wa kuwaponda na kuwasema wazi,
...Mwambie wale wanafunzi wa vyuo vikuu aliowatetea hasa UDSM siku hizi hawana mtetezi tenz wanafukuzwa kwa memo kama manamba kwenye mashamba ya mkonge, hamna tena wa kuwatetea, UDASA ya sasa siyo ile ulioyoiacha, ina maprofesa waoga kama kunguru wa Zanzibar

Yasser Arafat
...Mwambie bado wapalestina hajakombolewa, ni danadana kila siku
...Mwambie bado muisraeli mmoja anafidiwa na wapalestina 1000
...Mwambie mauaji ndi yanapamba moto ukanda wa Gaza, mwambie wanawake na watoto wa KIpalestina wanauawa kila kuchapo hawana tena msemaje kama yeye

Adlrahamani Babu
...Mwambie Muungano unasuasua kutokana na maslahi binafsi
...Mwambie upinzani ndio kabisa unafifia hakuna jipya tena
...Mwambie Wazanzibar wanmkumbuka sana na kamwe hawawezi kumsahau

Usisahu kuwasalimia Kwame Nkrumah, na kumwambia muungano wa Afrika imekuwa ndoto za abunuwasi. Wasalimie pia akina Mwanawasa, Jomo Kenyatta, na wanamapinduzi wengineo wote waliokwisha tangulia mbele za haki. Amen

RIP Prof. Haroub Othmani
 
Back
Top Bottom