Baada ya Zitto kuaga rasmi Bungeni na kutangaza kujiunga na chama kipya cha ACT-Tanzania, mwachama wa CHADEMA, Mzee Mweisigwa Baregu ameibuka na kumponda Mwanasiasa huyo kijana na machachari kuwa ni hovyo huku akikiri kuwa pamoja na Mama yake ZITTO marehemu Shida Salum(R.I.P) yeye(BAREGU) ndiye aliyekabidhiwa jukumu la kumlea Zitto kisiasa.
Said Kubenea anaandika alichokisema Baregu:
PROFESA Mwesiga Baregu, mmoja wa watu wanaoheshimika nchini amesema, aliyepata kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, anaponzwa na kibuli cha kujiona hakuna zaidi ya yeye. Anandika Saed Kubenea … (endelea).
Amesema, Zitto ambaye alikuwa naibu katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tanzania Bara na naibu kiongozi wa upinzani bungeni, anafanya kazi asiyoifahamu na ambayo haina mavuno.
"Ninamfahamu vizuri. Wakati tuhuma hizi za usaliti zilipoanza kuibuka, Kamati Kuu ilinikabidhi jukumu la kumsaidia mama yake mzazi kumlea kijana huyu."
Kauli ya Baregu ilitolewa siku moja baada ya Zitto kujiondoa bungeni na baadaye kujiunga na Chama cha ACT – Tanzania.
Prof. Baregu aliwahi kuwa "mlezi wa Zitto" ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Alikabidhiwa jukumu hilo na Shida Salum, mama mzazi wa Zitto (marehemu), baada ya mama huyo kuiomba Kamati Kuu (CC) ya chama hicho "kusaidia k
Ikumbukwe kuwa siku chache baada ya Mwanasheria wa CHADEMA, TUNDU ANTIPAS LISSU kutangaza kuwa Zitto siyo mwanachama wa CHADEMA kufuatia hukumu ya Mahakama, Ni MWEISIGWA BAREGU huyuhuyu alisikika kupitia shirika la habari la Ujerumani akisema kuna haja ZTTO na CHAMA chake cha CHADEMA kufikia muafaka kwa vile kuondoka kwake kutakuwa na athari kubwa kwa chama kwa vile ana watu wengi nyuma yake.
Hoja ya msingi hapa ni kuwa huenda U-HOVYO wa ZITTO unatokana na MALEZI ya HOVYO aliyoyapqta kutoka kwa MLEZI WA HOVYO.
BEREGU anapaswa kujitathmini kama anapaswa kupewa nafasi tena siku nyingine kumlea kijana kisiasa.
Source: Tanzania CLASSIC.blogspot.com